Friday 29 November 2019

Picha : ABIRIA WANUSURIKA KIFO HIACE IKITEKETEA KWA MOTO STENDI YA MABASI SOKO KUU MJINI SHINYANGA

...

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Abiria ambao idadi yao haijajulikana wamenusurika kuungua baada ya gari aina ya Hiace yenye namba za usajili T998 AAP linalofanya safari zake Shinyanga kwenda Maswa kuteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokeo leo Ijumaa Novemba 29,2019 majira ya saa nane na nusu wakati abiria wakiwa wamepanda kwenye Hiace hiyo wakijiandaa kuanza safari kuelekea Maswa mkoani Simiyu.

Dereva wa Hiace hiyo aliyejulikana kwa jina Basu Gereja amesema chanzo ni kupasuka kwa Betri na kusababisha gari hilo kuwaka moto.

"Chanzo ni Betri kulipuka,tumefanya utaratibu wa kuwatoa abiria kwenye gari kisha kupiga simu Zimamoto kwa ajili ya msaada ambao wamefika na kusaidia kuzima moto huu,gari ilikuwa inatoka Shinyanga kwenda Maswa",amesema Basu.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa dereva alikuwa amewasha gari akijiandaa na safari ndipo ghafla walipoona gari linawaka moto ndipo utaratibu wa kuwatoa abiria ukaanza kufanyika huku abiria wengine wakitokea madirishani kwa sababu mlango uligoma kufunguka.

Mratibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga Edward Lukuba (Afisa Oparesheni Mkoa wa Shinyanga) amesema wamepata taarifa za kuteketea gari kwa kuchelewa na kukuta gari hilo linaungua na kufanikiwa kuzima moto huo huku akiwasisitiza wananchi kujitahidi kuwa wanatoa taarifa mapema pindi majanga yanapotokea.
Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiendelea kuzima moto uliokuwa unateketeza Hiace katika Stendi ya Mabasi Soko Kuu Mjini Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mratibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga Edward Lukuba (Afisa Oparesheni Mkoa wa Shinyanga) akiwa eneo la tukio


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger