Saturday, 5 October 2019

JAMAA AFARIKI AKILA MAINI MABICHI BUCHANI

Wakazi wa eneo la Kapset kaunti ya Bomet nchini Kenya wamepigwa na butwaa kufuatia kisa cha jamaa kufariki dunia baada ya kunigwa na kipande cha maini.

 Inasemekana marehemu aliyetambulika kwa jina la Samuel Towett aliingia katika bucha moja iliyoko eneo hilo na kumuagiza mhudumu kumuuzia nyama, maini na utumbo.

 Polisi walisema marehemu alibugia kipande cha ini na kukila wakati mhudumu wa bucha akimpimia nyama.

Inasemekana alipokea huduma ya kwanza kabla ya kukimbizwa katika zahanati ya Itare Forest ambapo ilitangazwa kuwa tayari alikuwa amekata roho. 

Madaktari walisema marehemu alifariki akiwa njiani.

 Hata hivyo, wakati maafisa wa polisi walipowasili katika zahanati hiyo walikuta tayari jamaa wa marehemu wamepashwa habari na kuundoa mwili wake katika zahanati hiyo. 

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya Kapkatet huku familia yake ikiendelea na mipango ya mazishi. 
Via Tuko
Share:

TEMBO SITA WAANGUKA NA KUFA WAKIJARIBU KUOKOANA KWENYE MTEREMKO WA MAJI

Mamlaka nchini Thailand zinaamini wanama hao walianguka wakijaribu kumsaidia tembo mchanga

Tembo sita wameanguka na kufa nchini Thailand wakijaribu kuokoana katika mteremko hatari wa maji.

Maafisa wanasema kisa hicho kilitokea baada ya tembo mchanga kuteleza na kuanguka ndani ya mteremko wa maji katika mbunga ya kitaifa ya Khao Yai kusini mwa Thailand.

Wawili kati ya tembo hao wameonekana chini ya mlima ulio karibu huku mamlaka nchini humo ikijaribu kuwatoa mahali hapo.

Sio mara ya kwanza tembo kufa katika mteremko huo wa maji unaofahamika na wenyeji kama Haew Narok (Maporomoko ya jehanamu).

Tembo wanane walianguka na kufa katika eneo hilo mwaka 1992.

Maafisa wa kulinda wanyama na mimea wa Kitengo cha mbuga ya kitaifa ya Thailand, walifika katika eneo la tukio mapema Jumamosi baada ya kufahamishwa kuwa kundi la tembo limefunga bara bara karibu na eneo lenye mteremko wa maji.

Saa tatu baadae mzoga wa tembo wa miaka mitatu ulionekana chini ya mteremko wa Haew Narok, na mizoga mingine mitano ikapatikana karibu na hapo.

Edwin Wiek, mwanzilishi wa hazina ya kulinda maslahi ya wanyama pori nchi Thailand, amesema tembo hao hawangeliponea ajali hiyo kwasababu wengi wao hushirikiana kwa ulinzi na kutafuta chakula.

Mkasa huo utawaathiri tembo wengine katika mbuga hiyo.
"Ni sawa na kuondokewa na nusu ya familia yako," Bw. Wiek told aliiambia BBC.

"Hakuna unachoweza kufanya, ndio hali ya dunia," aliongeza.

Karibu tembo 7,000 wa bara Asia wanapatikana nchini Thailand.
Chanzo - BBC
Share:

TPRI YAWAFUNDA WAUZAJI WA VIUATILIFU 52 KUTOKA MIKOA 10 YA TANZANIA

Na Salvatory Ntandu - Biharamulo
Taasisi ya Udhibiti wa Viuatilifu Ukanda wa Kitropikali nchini Tanzania (TPRI) imetoa mafunzo kwa wauzaji na wamiliki wa maduka ya pembejeo yanayouza viuatilifu kwa wakulima ambayo yanalenga kuwawezesha kuzitambua athari zitokanazo na matumizi ya viuatilifu ambavyo havijasajiliwa hapa nchini.

Mafunzo hayo yametolewa kwa Kanda ya ziwa ambapo yamefanyika katika eneo la Nyakanazi wilaya ya Biharamulo mkoani Geita na kujumisha washiriki 52 ambao watapatiwa vyeti na TPRI baada ya kufuzo na kufaulu mitihani ya mwisho.

Akizungumza katika hafla ya kufunga Mafunzo hayo ya siku tano Mchambuzi mwandamizi wa viuatilifu kutoka TPRI Jumanne Rajabu amesema mafunzo hayo yatasaidia kudhibiti uuzaji holela wa viuatilifu visivyosajiliwa na Taasisi yao ambavyo vinatoka nje ya nchi.

Amesema katika ukaguzi walioufanya wamebaini wafanyabiashara wengi wa maduka ya pembejeo za kilimo wanauza viualitifu batili na ambavyo vimekwisha muda wake hali ambayo ni hatari kwa usalama wa mazao ya mkulima kwani wengi wao mazao yao yamekuwa yapata athari mbalimbali.

Kwa upande wake afisa Tarafa ya Rusahunga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa ya kufunga mafunzo hayo Zidikheri Shemsanga amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuacha tabia ya kuwauzia wakulima viauatilifu ambavyo vimekwisha muda wake hali ambayo inaweza kuhatarisha afya za wakulima pindi watakapozitumia.

Amewataka maafisa kilimo wilayani humo kuacha kutoa vibali vya uuzaji wa viuatilifu katika maduka ya pembejeo kabla ya kuwasiliana na TPRI ili kudhibiti uuzaji holela wa viuatilifu katika maduka hayo.

Mafunzo hayo ya siku saba yamejumuisha Jumla ya washiriki 52 kutoka katika mikoa 10 ya Tanzania bara.
Share:

Picha : DC MBONEKO AONGOZA WADAU KUSHEREHEKEA SIKU YA WAZEE KWA KUTOA MSAADA WA MAHITAJI KITUO CHA WAZEE BUSANDA


Wadau wa Maendeleo wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko wamesherehekea Siku ya Wazee Duniani kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 2.5 kwa wazee wanaolelewa katika kituo cha Busanda kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Wadau hao wamefika katika kituo hicho leo Jumamosi Oktoba 5,2019 kusherehekea Siku ya Wazee Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba 1.

Akizungumza katika kituo kinachohudumia kata 20 za wazee akiwa ameongozana na na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM),Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta amesema wameamua kusherekea siku ya wazee duniani katika kituo hicho kwa kuwapatia mahitaji muhimu yanayotakiwa ili kuwapunguzia changamoto zinazowakabili wazee hao.

Mboneko alivitaja vitu vilivyotolewa na Wadau kuwa ni Magodoro 20,shuka,vyandarua,mchele kilo 200,sukari kilo 50,unga wa sembe kilo 225,maharage,sabuni za miche na unga,mafuta ya kupaka na ya kupikia,dagaa,miswaki,dawa za meno,viberiti,juisi na nyanya.

Mkuu huyo wa wilaya amewashukuru wadau waliojitokeza kutoa msaada wa vitu hivyo vilivyogharimu jumla ya shilingi milioni mbili,laki tano na elfu ambao ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Superdoll Seif Said Seif aliyetoa msaada wa magodoro 20,vyandarua na shuka vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni moja na laki nne.

"Kwa namna ya pekee niwashukuru wadau walioguswa kutoa mchango kusaidia wazee wetu hawa.Wadau hawa ni pamoja Mkurugenzi wa Makampuni ya Superdoll,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko,Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal,Watumishi na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Hoja Mahiba na watumishi wa benki ya NBC",alisema Mboneko.

"Wadau wengine ni Kwaya ya Malaika Wakuu,Familia ya Richard Male,Familia ya mama Shane,Mama Mihambo na marafiki zake,Gilitu,Said Makilagi (Musoma Food),Dada Scola na Lightness,waandishi wa habari na wadau wengine ambao sijawataja ambao kwa pamoja wamefanikisha kupatikana kwa mahitaji haya kwa ajili ya wazee wetu",aliongeza Mboneko.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kila mtu ni mzee mtarajiwa hivyo ni vyema tukawapenda na kuwapatia mahitaji wazee huku akisisitiza msaada huo ni kwa ajili ya walengwa tu hivyo kuwataka watu wenye uwezo wafanye kazi ili kujipatia mahitaji yao.

Kwa upande wake,Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad aliahidi kuwalipia Bima ya afya iliyoboreshwa wazee 11 waliopo katika kituo cha Busanda ili wapate huduma za afya bila usumbufu.

Mbunge huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu kwa kujitokeza kugombea na kuchagua viongozi wenye kusaidia jamii.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza baada ya kuwasili katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mahitaji mbalimbali ya wazee katika kituo hicho. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM). Picha zote na Kadama Malunde na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Paroko wa Parokia ya Busanda,Padri Josephat Mahalu akimkaribisha Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mahitaji mbalimbali ya wazee katika kituo hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Nganganulwa kilipo kituo hicho,George Charles akifuatiwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akielezea kuhusu msaada wa vitu mbalimbali pichani vilivyotolewa na wadau wa maendeleo kwa ajili ya kusaidia wazee wanaolelewa  katika kituo cha Busanda.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Kulia ni Paroko wa Parokia ya Busanda,Padri Josephat Mahalu. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kituo cha Kulelea Wazee cha Busanda, Elias Shilanga akielezea kuhusu kituo cha Busanda. 
Sehemu ya vitu vilivyotolewa na wadau wa maendeleo kwa ajili ya wazee wanaolelewa katika kituo cha Busanda.
Wadau wakijiandaa kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya wazee katika kituo cha Busanda.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi unga wa sembe bi Mary Barabara katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Kila mzee alipokea msaada wa unga wa sembe,mchele,sukari,mafuta ya kupaka,mafuta ya kupikia,sabuni,godoro,shuka 2,vyandarua,maharage n.k
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akimkabidhi mafuta ya kupikia bi Mary Barabara katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akikabidhi godoro,shuka,chandarua kwa bibi (kulia).
Zoezi la kukabidhi godoro,shuka na chandarua likiendelea.
Bibi akifurahia baada ya kupokea mahitaji mbalimbali.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi mafuta ya kupikia kwa bibi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akiendelea kugawa mafuta ya kupikia.
Kulia ni Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga akisaidiana na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kubeba mfuko wa nyanya wakati wa kugawa vitu mbalimbali vilivyotolewa na wadau wa maendeleo kwa ajili ya wazee katika kituo cha Busanda.
Zoezi la kuweka sabuni za kufulia kwenye mifuko ili kugawa kwa wazee likiendelea.
Zoezi la kuweka sabuni ya unga kwenye mifuko likiendelea.
Zoezi la kuweka sabuni ya unga kwenye mifuko likiendelea.
Mdau Said Nassoro akigawa sabuni ya unga.
Zoezi la kugawa sabuni likiendelea.
Mzee Zacharia Makaranga akiwashukuru wadau waliotoa msaada kwa wazee wanaolelewa katika kituo cha Busanda.
Bibi akishukuru kwa msaada uliotolewa na wadau.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akiagana na Paroko wa Parokia ya Busanda,Padri Josephat Mahalu  baada ya kukabidhi msaada uliotolewa na wadau wa maendeleo katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akiagana na Paroko wa Parokia ya Busanda,Padri Josephat Mahalu  baada ya kukabidhi msaada uliotolewa na wadau wa maendeleo katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Share:

WANANCHI WASHAURIWA KUJIEPUSHA NA VICHOCHEO VYA MARADHI YA MOYO

Share:

Waziri Mkuu Aagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkalama Achunguzwe ....Agoma Kuweka Jiwe La Msingi La Hospitali Ya Wilaya Hiyo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Singida, Bw. Adili Elinipenda amchunguze Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkalama, Bw. Godfrey Sanga kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.

Baadhi ya tuhuma alizonazo ni kujilipa posho ya safari Machi mwaka huu bila kusafiri, kuwasainisha watumishi wa chini yake vocha na kisha kuwapa ‘asante kidogo’ kwa madai fedha hizo zinaenda mkoani, kujilipa stahiki kabla ya wakati na kuagiza gari liende gereji kwa matengenezo bila nyaraka zozote.

Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumamosi, Oktoba 5, 2019), wakati akizungumza na madiwani na watumishi wa Halmashauri hiyo kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Halmshauri hiyo.

“Kuna watumishi wanne uliwaambia wasaini vocha ya sh. 1,320,000. Hii ni kwa safari iliyopangwa kati ya tarehe 15 na 24 Septemba, mwaka huu; ukawapa asante ya sh. 30,000 ukidai kuwa zinatakiwa mkoani. RAS ni kweli hela hiyo ililetwa mkoani?” Alihoji Waziri Mkuu na kujibiwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Dkt. Anjelina Lutambi kwamba hakutoa hayo maagizo.

Alipoulizwa Mweka Hazina wa Wilaya hiyo, Bw. Peniel Mbula kwamba fedha alilipwa nani, mweka hazina huyo alijibu kwamba alikuwa Dodoma kikazi. Mhasibu aliyekaimu nafasi yake, Bi. Lulu Hamadi aliwataja watumishi hao kuwa ni Stella Mawa, Godfrey Mnubi, Richard Laizer na Method Kafuku.

Waziri Mkuu aliwasimamisha watumishi hao na kuwauliza walilipwa hiyo posho ili waende wapi lakini walikosa majibu. Ndipo akawaeleza kwamba walimkabidhi Mkurugenzi na wakalipwa asante ya sh. 30,000.

Alipoulizwa kuhusu malipo ya sh. 1,090,000 ambayo yalilipwa Septemba 9, mwaka huu yalikuwa ya nini, Mkurugenzi huyo alijibu kuwa ni ya stahiki zake za kila mwezi ambapo kati ya hizo, sh. 600,000/- ni za malipo ya nyumba; sh. 230,000  ni za umeme na sh. 260,000 ni za simu. Lakini hakuweza kujibu ni kwa nini amejilipa kabla mwezi haujaisha.

Kuhusu gari la elimu lenye namba za usajili STK 913 lililopelekwa gereji kupakwa rangi kwa gharama ya sh. milioni saba, Waziri Mkuu alitaka aoneshe dokezo lililotumika kupitisha idhini hiyo na malipo hayo lakini akajibiwa kwamba hakuna utaratibu wa kuandika dokezo pindi magari ya Halmashauri yanapoenda kufanyiwa matengenezo bali wanapeana taarifa kwa mdomo tu.

“Kamanda wa TAKUKURU leta maafisa kutoka mkoani waje wafanye ukaguzi wa kila jambo ambalo limeainishwa. Hatuwezi kuacha Halmashauri iendeshwe kienyeji bila kufuata taratibu. Mkalama inaonekana chafu kumbe tatizo ni mtu mmoja, mnasaini vocha halafu mnamsingizia RAS,” alisema.

“Ajenda ya kikao changu nanyi watumishi wenzangu, nilitaka tuambiane kwamba ni lazima tutunze mali na fedha za Serikali. Waheshimiwa Madiwani ni lazima msimamie Halmashauri yenu na mhoji kila senti imetumika vipi. Kama ni jengo nendeni mkakague, kama ni kisima nendeni mkaangalie,” alisisitiza.

“Pia niwasihi Waheshimiwa Madiwani wenzangu, msikubali kutumika kupitisha matmizi ya fedha ambayo si sahihi,” aliongeza.

Watumishi wa Halmashauri hii mfanye kazi, muache ubabaishaji sababu Serikali hii iko makini sana. Msiishi kwa mazoea, kwa sababu wakati siyo wenyewe na tena muache kutengezeza syndicates,” aliwaonya.

Pia amemuonya Afisa Manunuzi wa wilaya hiyo, Bw. Dickson Mataramba aache kutumika na kufanya kazi kwa mazoea kwa kupandisha bei ya sh. elfu 2000 hadi 3,000 kwenye vifaa wanavyoagiza.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amekataa kuweka jiwe la msingi la Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya kwa sababu lilikataliwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge na uchunguzi wake bado haujakamilika.

“Jiwe la msingi mlilonipangia kuweka leo kwenye hospitali ya wilaya siweki hadi TAKUKURU wakamilishe kazi ya uchunguzi kuhusu mikataba iliyotumika. Mkikamilisha uchunguzi mniite, nitakuja kulizindua likiwa limekamilika,” amesema.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Rais Magufuli Akutanam Na Rais Wa Zambia Edgar Lungu Tunduma Mkoani Songwe Kwa Ajili Ya Ufunguzi Wa Kituo Cha Pamoja Cha Huduma Za Mpakani

Kituo cha huduma za pamoja kati ya Tanzania na Zambia kilichopo mpakani Tunduma kwa Tanzania na Nakonde kwa Zambia, kimefunguliwa rasmi na Marais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na Edgar Lungu wa Zambia.

Baada ya kufungua kituo cha huduma kwa pamoja kati ya Tanzania na Zambia, Marais wa Tanzania Magufuli na Edgar Lungu wa Zambia kila mmoja ameingia kwenye chumba cha nchi yake ishara ya kuanza rasmi kwa matumizi ya kituo hicho.

“Niipongeze Wizara ya Fedha kwa kazi kubwa wanayoifanya lakini zaidi niwapongeze zaidi Mamlka ya Mapato (TRA)’ kwa mwaka huu wamevunja rekodi kwa ukusanyaji wa mapato. “Leo tumefungua kituo cha kihistoria cha kiuchumi na kimuungano kwa nchi zetu mbili za Tanzania na Zambia.

“Serikali ya Tanzania ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Zambia kurudisha reli ya Tazara na kama kuna watu wanakwamisha Mimi nitumbue huku na Rais Lungu atumbue huko kwake.-Rais Magufuli


Share:

Washitakiwa wa Makosa ya Uhujumu Uchumi Waendelea Kumiminika kwa DPP

Washitaki walioandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kukiri makosa ya uhujumu uchumi yanayowakabili, kufuatia msamaha uliotolewa na Rais John Magufuli, wanazidi kujitokeza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Miongoni mwa washitakiwa waliokiri na kuadhibiwa kulipa faini jana katika mahakama hiyo ni Mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) na Polisi watano, ambao wametakiwa kulipa faini ya Sh milioni 7.6 au kutumikia kifungo cha miaka saba jela, baada ya kukiri kuiba mafuta ya ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Mwingine ni raia wa Vietnam, Bui Nhi ambaye amehukumiwa kulipa faini ya zaidi ya Sh milioni 22, baada ya kutiwa hatiani katika mashitaka ya kujihusisha na nyara za serikali bila kibali.

Hata hivyo, washitakiwa wengine ambao wanataka kukiri makosa yao ikiwemo aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura na watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), akiwemo Mkurugenzi Mtendaji, Dickson Maimu na wenzake watafikishwa mahakamani hapo Jumatatu Oktoba 7, mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na mchakato wa kukiri makosa yao.

Kati ya askari waliohukumiwa ni Koplo Shwahiba (38) MT. 74164 SGT, Ally Chibwana (47) wa JWTZ, Konstebo Elidaima Pallangyo (38), Konstebo Simon (28), Konstebo Dickson na Konstebo Hamza, ambao walifutiwa mashtaka ya utakatishaji fedha na kupanga genge la uhalifu na kubaki na mashitaka ya wizi.

Kabla ya kufutiwa mashitaka yao, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Renatus Mkude alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo kuwa wameingia makubaliano na washitakiwa hao kumaliza shauri hilo, hivyo anaiomba makubaliano hayo yawe sehemu ya shauri hilo.

Hakimu Mwaikambo alisema ni lazima mahakama ijiridhishe, kama ni kweli washitakiwa waliweka makubaliano hayo kwa hiari bila kulazimishwa, ambapo walikiri kwamba waliandika makubaliano wenyewe. 

Akitoa adhabu, Hakimu Mwaikambo alisema amezingatia kwamba washitakiwa ni wakosaji wa kwanza na kwa kuzingatia msamaha uliotolewa na Rais wa washitakiwa kukiri makosa yao, hivyo kupunguziwa kiwango cha makosa yao.

“Adhabu kila mshitakiwa atatakiwa kulipa faini ya shilingi 500,000 kila mmoja au kifungo cha miaka saba jela, pia mtatakiwa kulipa thamani yote mliyosababisha hasara ya shilingi 4,647,760. Pia magaloni yote ya mafuta yanataifishwa na kuwa mali ya serikali,” alisema Hakimu Vick.

Wakili Mkude alidai shauri hilo limeingia utaratibu wa makubaliano, hivyo suala la adhabu anaiachia mahakama. Pia aliomba warudishe hasara waliyosababisha na kutaifisha madumu 109 ya mafuta ya ndege.


Share:

Dawa Komesha Ya Maumbile Madogo , Nguvu Za Kiume Na Magonjwa Mengineyo

*NGETWA MIX*/
√Hii ndio dawa bora ya mitishamba kiboko ya maumbile Madogo(KIBAMIA) Hurefusha na kunenepesha maumbile  mafupi pia  yaliyoingia ndani kutokana na kitambi ama kuathirika na punyeto

*📌SUPER MORINGA MIX*/
Ni dawabora ya nguvu za kiume yenye mchanganyiko wa miti shamba 10 yenye maajabu yafuatayo:/
🔖(1)Inatibu upungufu wa nguvu za kiume mara dufu na kuimarisha misuri   ilio legea na kusinyaa wakati wa tendo la ndoa/
🔖(2)Kuongeza hamu ya tendo kukufanya uweze kurudia tendo hadi mara tatu bila kuchoka
🔖(3)Itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15-30 kwa tendo la Kwanza na utakuwa na uwezo wa Kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3-4 bila hamu kuisha na inatibu kabisa/
.
*MATATIZO HAYA HUSABABISHWA NA*/
🔖(1)Tumbo kujaa gesi, na kuunguruma chini ya kitovu/
🔖(2) Choo kuwa kama Cha mbuzi/
🔖(3)Ngiri/
🔖(4)Kama umejichua sana punyeto/
🔖(5)Kisukari/
🔖(6)Presha ya kupanda na kushuka/
🔖(7)Vidonda vya tumbo,/
.
Na haya yote husababisha/
📍Kuishiwa kwa nguvu za kiume 📌/
. _______________________
Bado hujachelewa dawa hizi ni mpya kabisa  ni tofaut na ulizo wahi kutumia pia zimeonesha mafanikio kwa watu wengi sana/

Pia tuna tibu  KISUKARI,PRESHA,VIDONDA VYA TUMBO N.K/
._______________________
DR .SELEMANI OMARY ANAPATIKANA  DAR ES SALAAM , PIA UNAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO  NDANI NA NJE YA NCHI .SIMU NO:/
*📞+255788468114*


Share:

RC Kagera Aongoza Mamia Ya Wananchi Mkoani Humo Kuboresha Taharifa Zao Kwenye Daftari La Wapiga Kura

Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera
Viongozi wa vyama vya siasa,watendaji na wananchi mkoani Kagera  wametakiwa kuweka umakini wa kipekee katika wilaya zote za mpakani ikiwemo Misenyi, Kyerwa, Ngara pamoja na Karagwe kuhakikisha kwamba hakuna mtu asiye na sifa anajipenyeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti jana Oktoba 4, 2019 wakati akikagua  na kujionea hali halisi ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linaloendelea katika  vituo mbalimbali katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti amesema hatarajii kuona mtu yoyote ambaye si raia wa Tanzania akishiriki katika zoezi hilo na endapo itatokea sheria na taratibu zitafuata mkondo wake kwa wote watakao kuwa wamehusika na jambo hilo kutokana na serikali kuwekeza fedha nyingi ili kuhakikisha wananchi wake wanapata fursa hiyo na wanatumia haki yao kikatiba kupata viongozi wanaohitaji kwa maendeleo ya taifa.

Aidha amefurahia muitikio mzuri wa wananchi wanaojitokeza katika uboreshaji wa daftari hilo na kutoa wito kwa wananchi wote katika maeneo yote ambayo yamewekwa vituo hivyo vya maboresho ya taarifa kutumia muda huo vizuri kuhakikisha wote wenye sifa za msingi za kupiga kura wafanye uboreshaji wa taarifa zao ili waweze kustahili kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera pia amefanya uboreshaji wa kumbukumbu zake katika kituo cha kujiandikisha kilichopo katika kata ya Miembeni Manispaa ya Bukoba na kuwahimiza wananchi mkoani Kagera kutumia siku 7 za uboreshaji daftari la wapiga kura Oktoba 3 hadi Oktoba 9  kuhakikisha wamejiandikisha. 
 


Share:

Raia Magufuli Agoma Kumfukuza Mkurugenzi Aliyechongewa na Mbunge

Rais Magufuli amewataka viongozi kuacha malumbano yasiyo na tija na badala ya katika kuwahudumia wananchi wao ambao wamewapa dhamana kubwa ya kuwaletea maendeleo.

Magufuli amesema hayo leo Ijumaa, Oktoba 5, 2019 wakati akizungumza na wananchi a Songwe mara baada ya uzinduzi wa Barabara ya Mpemba – Isongolea mbapo Mbunge wa Ileje (CCM), Janeth Mbene alisimama na kusema Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo hana ushirikiano na viongozi mbalimbali na kusababisha changamoto katika utendaji.

Mbene amesema mkurugenzi huyo amekuwa hatoi ushirikiano kwa wenzake na hatekelezi majukumu yake ipasavyo na kwamba tatizo hilo limekuwa likielezwa kwa viongozi mbalimbali na pia mkoa umelifanyia kazi.

Akijibu tuhuma hizo, Rais Magufuli amesema ‘Kuhusu hili la mkurugenzi unajua kwa watu ambao hawaijui Ileje unaweza ukashangaa, sina uhakika kama dhambi zote hizo ni za mkurugenzi,” amesema na kuongeza

“Taarifa niliyonayo mimi, na Jafo (Waziri wa Tamisemi) ni shahidi kwamba huyu mkurugenzi saa nyingine anaacha kazi zake za ofisini anaenda kufundisha darasani.”


“Sasa mkurugenzi simtoi hadi nipate taarifa zangu mwenyewe, mkurugenzi uko hapa, sikutoi mpaka nipate information zangu mwenyewe, viongozi tuache kuchongeana haya ndiyo yanayotukwamisha,” amesema Rais Magufuli


Share:

Uhakiki Taasisi Za Kidini Na Jumuiya Za Kijamii Kanda Ya Ziwa

Na Mwandishi Wetu, MOHA
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kijamii na Taasisi za Kidini, itaanza kufanya uhakiki wa Jumuiya na Taasisi hizo awamu ya nne. 

Uhakiki huo utahusisha Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni  Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Kagera na Shinyanga kuanzia Oktoba 7-18, mwaka huu. 

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, ilisema uhakiki katika mikoa hiyo utafanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. 

“Katika uhakiki huo, Jumuiya na Taasisi husika zinapaswa kuwasilisha nyaraka mbalimbali, huu ni mchakato endelevu ambao unahusisha mikoa yote nchini,” alisema. 

Alisema nyaraka hizo ni cheti halisi cha usajili na kivuli cha cheti hicho, stakabadhi ya mwisho ya malipo ada iliyolipwa hivi karibuni, katiba ya Jumuiya au Taasisi husika. 

Katiba hiyo ni ile iliyopitishwa na Msajili, barua ambayo inathibitisha uwepo wa Jumuiya, Taasisi husika kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Mtaa, Kata mahali ilipo ofisi ya Jumuiya, Taasisi, taarifa ya Mkutano Mkuu wa Mwaka na fedha ya mwaka. 

“Fomu ya uhakiki inapatikana katika tovuti ya Wizara hiyo sambamba na kwenye kituo cha uhakiki,” alifafanua. 

Meja Jenerali Kingu alisema taasisi ambazo zitashindwa kuhakikiwa kwa mujibu wa ratiba ya eneo husika zitalazimika kwenda Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma kwa ajili ya uhakiki na kama zitashindwa kufanyiwa uhakiki kwa muda uliopangwa zitaondolewa kwenye Daftari la Msajili. 

Alisema Taasisi za dini na Jumuiya ambazo hazijasajiliwa zinatakiwa kufika wakati wa uhakiki ili ziweze kupewa utaratibu wa kupata usajili.


Share:

Waziri Mkuu Akagua Shamba La Korosho Manyoni

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua shamba la mfano la korosho lenye ukubwa ekari 12,000 lililopo kijiji cha Misigati, wilayani Manyoni na kusema kuwa ameridhishwa na uamuzi wa wilaya hiyo kuwa na zao mbadala la biashara.

Akizungumza na wananchi na baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo waliokuwepo eneo hilo jana (Ijumaa, Oktoba 4, 2019), Waziri Mkuu alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi kwa kulibeba wazo hilo na kuhakikisha linatimia.

“Nimpongeze Mkuu wa Mkoa wa kulibeba jambo hili, lakini nikuombe wewe na viongozi wenzako mhamasishe wengine walime zaidi zao hili kwa sababu korosho ni zao kubwa duniani na tena zao hili lina bei nzuri kimataifa,” alisema.

Alisema anatambua kwamba timu ya wataalamu kutoka kituo cha utafiti wa kilimo cha Naliendele, Mtwara imeshawasili Manyoni ili kufanya utafiti za zao hilo na jinsi linavyoweza kuzaa mara mbili kwa mwaka.

“Kwa kawaida, mkorosho mmoja hutoa kilo 40 za korosho kwa msimu mmoja, kwa hiyo kwa misimu miwili mtapata kilo 80. Ninawasii limeni korosho kwa ajili ya watoto wenu ambao wako darasa la pili au la tatu. Mkulima ukianza kuvuna, utaendelea kuvuna kwa miaka 20 mfululizo na kwa hiyo hao watoto hawatahitaji kulipiwa ada wakiwa chuo kikuu sababu korosho itakuwa inawalipia,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wakulima wanaolima zao hilo wilayani Manyoni, waunde Ushirika wao ambao utawasaidia kuagiza dawa kwa pamoja ama kuuza kwa pamoja.

Hivyo, amemwagiza Afisa Ushirika wa Wilaya hiyo, Bi. Yusta Philipo ahakikishe anasimamia jambo hilo kuanzia sasa

Mapema, akitoa taarifa juu ya mradi huo, Meneja wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Kanda ya Kati, Bw. Ray Mtangi alimweleza Waziri Mkuu kwamba mradi wa kilimo cha korosho unajumuisha mashamba makubwa mawili ambapo shamba la Misigati lina ukubwa wa ekari 7,000 na lile la Mikwese lenye ukubwa wa ekari 5,000.

Alisema watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa kitaifa wamekuwa wakifika shambani hapo ili wajifunze mbinu mpya za kuzalisha korosho kwenye maeneo yao. “Wiki mbili zilizopita, Mheshimiwa Spika na madiwani wa Kongwa walipita hapa ili kujifunza zao hili,” alisema.

Pia alisema Halmashuri yao imetenga eneo la ujenzi wa viwanda na kwamba hadi sasa wanazo ekari 50 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya kubangua korosho.

Mapema, Waziri Mkuu alikagua shamba hilo na kujionea hali halisi ya shambani ikoje. Pia alioneshwa mabibo na korosho ambazo zimevunwa kutoka kwenye shamba hilo la mfano, kutoka kwenye mashamba ya wakulima ambao walipanda miche tangu Januari, mwaka jana.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Waziri Mkuu: Wakuu Wa Wilaya, Wakurugenzi Kamateni Watoto Wasiokwenda Shule

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Wilaya za Itigi na Ikungi na Wakurugenzi wao wafanye misako kwenye stendi za mabasi ili kuwabaini watoto wasiokwenda shule.

Ametoa agizo hilo kwa nyakati tofauti jana (Ijumaa, Oktoba 4, 2019) wakati akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza kwenye mikutano ya hadhara aliyoifanya kwenye wilaya hizo.

Alisema Serikali ya awamu ya tano imeondoa michango kwenye sekta ya elimu na kwa maana hiyo watoto wenye umri wa kwenda shule wanapaswa wawe shuleni.

"Michango ya hovyohovyo haipo. Vinginevyo, fedha ambazo wazazi mmeokoa, peleka kwa mtoto. Mnunulie sare, kiatu kizuri, begi la shule na madaftari. Ale vizuri asubuhi na aende shule," alisisitiza Waziri Mkuu.

"Hatutarajii kuona vijana wadogo wanauza biashara kwenye vituo vya mabasi. Mkurugenzi chukua OCD siku moja, nenda kwenye miji yenu midogo, saka watoto wote wanaofanya biashara stendi."

"Watambue wazazi wao, halafu kamata wazazi hao wajieleze ni kwa nini wanawaacha watoto wao waende kuhangaika stendi badala ya kwenda shule. Tunataka kila mtoto wa Kitanzania aende shule," alisisitiza.

Alisema Serikali imetoa maelekezo kwamba kila kijiji kinapaswa kiwe na shule ya msingi na kila shule lazima iwe na darasa la awali ili watoto wenye umri wa miaka minne hadi mitano waanze shule mara moja.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Waziri Mkuu Awasifu DC, DED Wa Wilaya Ya Ikungi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewapongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Justice Kijazi kwa kuamua kuchapa kazi na kuweka mbele maslahi ya wananchi.

“Moja ya Hamashauri zilizotulia ni Ikungi. Hii ni Halmashauri pekee ambayo Mkuu wa Wilaya ya Mkurugenzi wake wanaongea lugha moja. Endelezeni kazi hii nzuri ili viongozi wengine waje kujifunza kwenu,” alisema na kuamsha shangwe miongoni mwa watumishi waliohudhuria mkutano wa hadhara.

Alitoa pongezi hizo jana jioni (Ijumaa, Oktoba 4, 2019), wakati akizungumza na wananchi na watumishi wa Halmashauri hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Ikungi.

Aliwataka watumishi wa Halmashauri hiyo watambue kwamba wako chini ya wananchi na kwamba bila ya uwepo wao, hata wao wasingepata kazi wilayani humo. “Mimi na ninyi sote ni watumishi wa hawa wananchi. Bila wao, tusingekuwa na utumishi hapa. Lazima mtambue kwamba mmeletwa hapa ili muwahudumie wao,” alisisitiza.

“Nendeni vijijini, wahudumieni bila kujali umri wao, dini, rangi au itikadi zao. Wakiuliza masuala ya kilimo au maji au afya, washughulikieni na muwape majibu huko huko. Wananchi wengine wanaishi vijiji vya mbali na hapa, wengine hawana nauli, wengine hawajui hata wakija mjini waanzie wapi,” alisisitiza.

“Nimekuwa nikisisitiza kwamba wakuu wa idara wasikae ofisini kwa wiki nzima. Nendeni vijijini mkawasikilize wananchi. Wakuu wa idara tofauti, jipangeni mtumie gari moja; siku nne kati ya tano za wiki, nendeni vijijini mkasikilize wananchi na siku mbili zilizobakia mje muandike taarifa zenu ofisini,” alisema.

“Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi simamieni hili, kwa sababu ni mojawapo ya matakwa ya Serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo.

Mapema, akitoa salamu, Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. Edward Mpogolo alimweleza Waziri Mkuu kwamba uuzaji wa pamba katika wilaya hiyo unaendelea na hadi sasa wameshauza tani milioni 1.4 kati ya tani milioni 2.5 walizojiwekea malengo.

“Pamba imeendelea kununuliwa kwa bei ya sh. 1,200 kama ilivyoelekezwa na hadi sasa tani milioni 1.4 zenye thamani ya sh. bilioni 1.7 zimenunuliwa viwandani. Tunaishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwawezesha wananchi hawa kupata fedha hiyo,” alisema.

Alisema anaishukru Serikali kwa kuboresha huduma za afya, mikopo kwa wanawake na vijana, umeme na elimu ambapo ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 64 hadi asilimia 83.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Naibu Waziri wa Ardhi Avutiwa Na Kasi Ya Ujenzi Mradi Wa Machinjio Ya Vingunguti

Na Munir Shemweta, WANMM
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametembelea mradi wa ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti na kuvutiwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo inayofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambapo alilitaka shirika hilo kuhakikisha linajenga jengo lenye ubora.

Akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo jana, Dkt Mabula alisema pamoja na mradi huo kutakiwa kukamilika katika kipindi cha miezi mitatu badala ya 12 ya awali lakini hatarajii kuona Shirika la Nyumba linajenga jengo lililo chini ya kiwango.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, NHC ni shirika la umma lenye kila fani katika masuala ya ujenzi hivyo basi ujenzi wa mradi huo ujenge imani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na watanzania kwa kukamalisha mradi huo katika kipindi cha miezi mitatu.

Dkt Mabula alisema, Maelezo ya Rais kuhusiana na mradi wa machinjio ya Vingunguti ubadilishe fikra za Shirika la Nyumba la Taifa katika miradi yake mbalimbali sambamba na kuonesha uwezo katika miradi waliyopewa kwa kujenga kwa kasi na kwa muda mfupi ukilinganisha na makampuni mengine ya ujenzi.

‘’Tuondoke katika fikra tuliyokuwa nayo huko nyuma, tujenge trust kwa mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’’ alisema Dkt Mabula

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Muungano Saguya alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa shirika hilo limejipanga kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha linakamilisha ujenzi katika muda uliopangwa.

Alisema ujenzi wa mradi huo wa machinjio ya Vingunguti umefikia hatua nzuri na ana imani kutokana na jinsi shirika lilivyojipanga katika mradi huo, ujenzi wake utakamilika katika muda uliopangwa kama ilivyoelekezwa na rais.


Share:

TRC Yakanusha Taarifa Zinazosambaa Katika Mitandao Ya Kijamii Kuhusu Fursa Za Ajira Zaidi Ya 200 TRC




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger