Na Salvatory Ntandu - Biharamulo
Taasisi ya Udhibiti wa Viuatilifu Ukanda wa Kitropikali nchini Tanzania (TPRI) imetoa mafunzo kwa wauzaji na wamiliki wa maduka ya pembejeo yanayouza viuatilifu kwa wakulima ambayo yanalenga kuwawezesha kuzitambua athari zitokanazo na matumizi ya viuatilifu ambavyo havijasajiliwa hapa nchini.
Mafunzo hayo yametolewa kwa Kanda ya ziwa ambapo yamefanyika katika eneo la Nyakanazi wilaya ya Biharamulo mkoani Geita na kujumisha washiriki 52 ambao watapatiwa vyeti na TPRI baada ya kufuzo na kufaulu mitihani ya mwisho.
Akizungumza katika hafla ya kufunga Mafunzo hayo ya siku tano Mchambuzi mwandamizi wa viuatilifu kutoka TPRI Jumanne Rajabu amesema mafunzo hayo yatasaidia kudhibiti uuzaji holela wa viuatilifu visivyosajiliwa na Taasisi yao ambavyo vinatoka nje ya nchi.
Amesema katika ukaguzi walioufanya wamebaini wafanyabiashara wengi wa maduka ya pembejeo za kilimo wanauza viualitifu batili na ambavyo vimekwisha muda wake hali ambayo ni hatari kwa usalama wa mazao ya mkulima kwani wengi wao mazao yao yamekuwa yapata athari mbalimbali.
Kwa upande wake afisa Tarafa ya Rusahunga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa ya kufunga mafunzo hayo Zidikheri Shemsanga amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuacha tabia ya kuwauzia wakulima viauatilifu ambavyo vimekwisha muda wake hali ambayo inaweza kuhatarisha afya za wakulima pindi watakapozitumia.
Amewataka maafisa kilimo wilayani humo kuacha kutoa vibali vya uuzaji wa viuatilifu katika maduka ya pembejeo kabla ya kuwasiliana na TPRI ili kudhibiti uuzaji holela wa viuatilifu katika maduka hayo.
Mafunzo hayo ya siku saba yamejumuisha Jumla ya washiriki 52 kutoka katika mikoa 10 ya Tanzania bara.
0 comments:
Post a Comment