Saturday, 3 August 2019
PICHA: Waziri Lugola Aongoza Kikao Cha Tume Ya Utumishi Ya Polisi, Uhamiaji Na Magereza Jijini Dar Es Salaam, Leo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Polisi, Uhamiaji na Magereza wakati wa kikao cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo chini ya Wizara yake.
Kikao hicho kilifanyika jijini Dar es Salaam, leo. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. wapili kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF), Thobias Andengenye, na kushoto ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kikao hicho kilifanyika jijini Dar es Salaam, leo. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. wapili kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF), Thobias Andengenye, na kushoto ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto) akizungumza katika Kikao cha Tume ya Utumishi ya Polisi, Uhamiaji na Magereza cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo katika Wizara hiyo. Kikao hicho kilifanyika jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Polisi, Uhamiaji na Magereza wakati wa kikao cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo chini ya Wizara yake. Kikao hicho kilifanyika jijini Dar es Salaam, leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia meza kuu) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Polisi, Uhamiaji na Magereza wakati wa kikao cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo chini ya Wizara yake. Kikao hicho kilifanyika jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Vyama 18 na wagombea 60 wajitokeza kuchukua Fomu za Uchaguzi Mdogo wa Udiwani Kata 13
Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliutangazia Umma kuhusu Uchaguzi Mdogowa Udiwani katika Kata 13 za Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 17 Agosti mwaka 2019,kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 13 (3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura Na. 292.
Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi huo, Utoaji wa Fomu za wagombea ulipangwa kufanyika kuanzia tarehe 29 Julai hadi 03 Agosti, 2019 na Uteuzi wa wagombea kufanyi katarehe 03 Agosti, 2019.
Hadi kufikia tarehe 02 Agosti, 2019 saa 10:00 jioni jumla ya wagombea 60 kutoka vyama vya siasa 18 wamechukua fomu za uteuzi.
Vyama vilivyochukua fomu hadi sasa na idadi ya wagombea waliochukua fomu kwenye mabano ni Chama cha DEMOKRASIA MAKINI(5) AAFP (5), CCK(3), DP (4), SAU (4), UDP(4) ACT Wazalendo (3), UPDP (5), ADC (2), TLP (1), CCM (12), ADA TADEA (4), CHADEMA (2), CHAUMA (1), NRA (1), NLD (1), CUF (2)na UMD (1).
Vyama vilivyochukua fomu hadi sasa na idadi ya wagombea waliochukua fomu kwenye mabano ni Chama cha DEMOKRASIA MAKINI(5) AAFP (5), CCK(3), DP (4), SAU (4), UDP(4) ACT Wazalendo (3), UPDP (5), ADC (2), TLP (1), CCM (12), ADA TADEA (4), CHADEMA (2), CHAUMA (1), NRA (1), NLD (1), CUF (2)na UMD (1).
Imetolewa leo tarehe 02 Agosti, 2019 na
Hussein Makame
AFISA HABARI
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
WATUMIAJI WA HUDUMA YA MAJI KAHAMA WALIA NA BEI MPYA YA MAJI
SALVATORY NTANDU
Mamlaka ya maji safi na Usafi wa mazingira mjini Kahama (KUWASA) imetakiwa kutumia njia shirikishi wanapotaka kupandisha bei Ankara maji ili kupunguza malalamiko kwa watumiaji wa huduma hiyo pindi bei mpya zinapoanza kutumika.
Baadhi ya watumiaji wa maji wilayani humo wamesema (KUWASA) wamepandisha Ankara za maji kutoka shilingi 1688 kwa uniti moja hadi shilingi 1888 kwa uniti moja bila kuwashirikisha.
Wamesema awali kabla ya akra za maji haziongezeka walikuwa wakilipa shilingi 1015 kwa uniti moja, lakini hapo baadae zikaongezeka hadi shilingi 1688 nakuongeza kwa mwaka huu wa fedha 2019/20 wameongeza tena hadi kufikia kiasi cha shilingi 1888.
Rajabu Shabani ni mmoja wa watumiaji wa maji kutoka kata ya kahama mjini amesema ,hawakatai kuongezeka kwa bili za maji lakini mamlaka ya maji ilipaswa kutoa taarifa kwa wananchi ambao ndio wadau wa maji kabla ya kuanza kutumia kwa bei mpya iliyoongezeka ili kupunguza malalamiko.
Amesema Mwaka jana Mamlaka hiyo ilipandisha Ankara za maji kutoka shilingi 1688 na tulikubaliana nayo japo tulilalamika kwenye mkutano wa mkuu wa mkoa,chakushangaza kabla yakuisha kwa mwaka huu wameongeza tena hadi kufikia kiasi cha shilingi 1888 sawa na ongezeko la shilingi 200.
Sophia Hamisi mkazi wa Malunga nae amesema bei hiyo ni kubwa na inaweza kusababisha wakazi wengi wakaacha kutumia maji kutoka mamlaka hiyo na kuanza kutumia maji ya visima jambo ambalo linaweza likasababisha wakakosa wateja na kupunguza mapato ya taasisi hiyo.
Akijibu Malalamiko hayo Mwenyekiti wa bodi ya kuwasa Meja mstaafu, Bahati Matala amekiri kuongezeka kwa bei hiyo nakuongeza ongezeko hilo linatokana na kikao cha wadau wa maji kiliketi mwaka jana na kukubaliana kuongeza kwa bei ili kutanua mtandao wa maji kwa wananchi.
Amesema kuwa, hapo awali kabla ya kuongeza kwa bei wananchi walikuwa wanatozwa shilingi 1015 kwa uniti moja na ikaongeza hadi kufikia shilingi 1688 na mwaka huu wa fedha 2019/20 bei imeongezeka hadi kufikia kiasi cha shilingi 1888.
Hivi karibuni Waziri wa maji, Prof.Makame Mbarawa alifanya ziara wilayani kahama na kuitaka mamlaka hiyo kukusanja mapato ya maji pamoja na kuongeza mtandao wa maji kwa wananchi wa kata 20 zilizopo mjini kahama ampapo kwa sasa kata 12 pekee ndizo zenye huduma hiyo.
MTANGAZAJI WA IDHAA YA KISWAHILI DW MOHAMMED DAHMAN AFARIKI DUNIA
Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW mjini Bonn Mohammed Dahman,amefariki dunia siku ya Ijumaa (02.08.2019) mjini Cologne, magharibi mwa Ujerumani.
Mohammed alikuwa mwandishi habari mahiri katika nyanja zote, lakini alipendelea sana taarifa ya habari za ulimwengu na makala ya mbiu ya mnyonge.
Asilimia kubwa ya wasikilizaji walizipenda sana makala zake kuhusu masuala ya haki za binadamu na sauti yake ya huruma. Aliwapa sauti wasiokuwa na saut, hakukata tamaa kuwatafuta watu muafaka wa kuwahoji na alikuwa makini sana katika kuhakikisha taarifa zake pamoja na makala haziegemei upande mmoja.
Kama mwandishi, Mohammed alikuwa mfano wa kuigwa kwa wengi wetu. Amekuwa akiugua kwa kipindi cha takriban miaka miwili na muda wote huu hakuweza kufanya kazi. Hata hivyo hatukukata tamaa kwamba angepata afueni na kurejea kazini kujumuika nasi kuendelea na majukumu yake.
Katika wakati huu mgumu wa majaribu, fikra na dua zetu tunazielekeza kwa mke wake, binti yake na familia yake visiwani Zanzibar na ughaibuni. Tunawapa pole na kutoa rambirambi zetu kwa majonzi makubwa, machozi yakitiririka machoni mwetu. Tunawaombea. Tulimpenda, lakini Mungu amempenda zaidi.
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Andrea Schmidt, na wafanyakazi wote wa idhaa hii mjini Bonn tunawapa pole jamaa, marafiki na mashabiki kwa kuondokewa na mpendwa wetu.
(Andrea Schmit; Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ayataja Maonesho Ya Nanenane Kuwa Taswira Chanya Kwa Wakulima
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu
SHEREHE za wakulima maarufu kama Nane Nane zimetajwa kuwa ni darasa huru kwa wakulima, wadau wa kilimo na wananchi kwa ujumla kwani zinatoa nafasi kwao kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kilimo chenye tija, Ufugaji wa kisasa na Uvuvi wenye tija pasina kuharibu rasilimali za serikali.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew J. Mtigumwe wakati akizungumza na mtandao wa Wazo Huru Blog mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi kwenye Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Alisema kuwa serikali inatambua kadhia inayowakabili wakulima nchini ikiwemo pembejeo feki ambazo wakulima wanauziwa, hivyo kupata hasara ikiwamo mazao kidogo na hafifu tofauti na kusudio lao la kujipatia mazao mengi ya biashara na chakula jambo ambalo inalifanyia kazi ili kukabiliana nalo kwa haraka.
Maonyesho haya Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu yatawasaidia wakulima kupata elimu juu ya pembejeo halisi ikiwamo mbegu, dawa (viuatilifu), mbolea kutoka kwa mashirika husika yanayozalisha pembejeo mbali mbali, ili kuwasaidia kuepuka kununua pembejeo feki ambazo huwasababishia hasara na kuwakatisha tamaa.
Sherehe hizi huambatana na maonyesho ya bidhaa za kilimo yanayofanywa na wakulima na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya kilimo, lengo likiwa ni kujitangaza shughuli zao, kubadilishana uzoefu na wataalamu wa kilimo.
Pia wakulima wadogo ambao ni wengi ukilinganisha na wakulima wakubwa watajifunza mbinu mpya za kitaalamu za kilimo zinazoendana na wakati uliopo kwa maana ya mabadiliko ya kiteknolojia na tabia nchi ili wakulima waweze kulima kilimo cha kisasa na kunufaika kiuchumi.
Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa Kwa muda mrefu wakulima wamekuwa wakilima kilimo cha mazoea ambacho hakizingatii kanuni za kitaalamu, jambo lililowasababisha kukata tamaa na kuona kuwa kilimo hakilipi kutokana na mbinu duni walizozitumia.
Alisema kuwa Wizara ya Kilimo inajipambanua zaidi kumkwamua mkulima ili Wakulima nchini waondokane na kilimo cha kubahatisha cha kutegemea mvua na badala yake wajikite katika kilimo cha umwagiliaji ambacho ni cha uhakika, kinachoweza kuyabadilisha maisha yao kiuchumi kutokana na mazao mengi watakayopata.
"Natambua kuwa zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanategemea sekta ya kilimo kama ajira yao Sehemu kubwa ya kilimo ni cha wakulima wadogo wadogo ambao mashamba yao yana ukubwa wa hekta 0.9 na hekta 3.0 kwa kila moja, Karibu asilimia 70 ya ardhi ya kilimo na mazao inalimwa kwa kutumia jembe la mkono, asilimia 20 hutumia maksai na asilimia 10 hutumia trekta Hivyo kama wizara tutajitahidi kadri iwezekanavyo kuwakwamua wananchi ili kuondokana na uduni katika mavuno" Alisema Mtigumwe
Mbali na hayo, kilimo cha Tanzania ni cha kutegemea mvua, uzalishaji wa mazao ya chakula ndio unaongoza katika uchumi wa kilimo. Hekta milioni 5.1 zinalimwa nchi nzima kila mwaka, kati ya hizo asilimia 85 ni kwa ajili ya mazao ya chakula tu, na wanawake ndio wafanyakazi wakubwa mashambani.
Mhandisi Mtigumwe anasema katika maonesho hayo anatarajia wakulima watajifunza mbinu bora na za kisasa za kilimo zitakazowawezesha kupata mazao mengi na kuinua kipato chao.
Aidha ametoa wito kwa wakulima na mashirika kujitokeza katika maonesho hayo kwa sababu watapata fursa ya kujifunza mambo mengi na kubadilishana uzoefu na wataalamu mbalimbali wa kilimo.
MWISHO
Jeshi la Polisi Latoa Mafunzo Kwa Wahudumu Wa Mkutano Wa SADC
Tunapoelekea katika Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC na kuhakikisha mkutano huo unakua wa mafanikio na kuiletea sifa nchi yetu, Jeshi la Polisi Tanzania limepewa fursa ya kutoa mafunzo ya utayari kwa wahudumu watakaoshiriki kutoa huduma za msingi kwa wajumbe wakati mkutano huo ukiendelea ambao unaotarajiwa kuanza tarehe 17 na 18 mwezi huu.
Mkuu wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ali Lugendo amesema mafunzo hayo yanayohusisha wanafunzi 71, yatawasaidia kuwajengea uwezo wa kiuzalendo na nidhamu na kuwa mabalozi wazuri kwa wageni watakaohudhuria katika mkutano huo katika masuala ya utalii.
Naye Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Anthony Rutashuburugukwa alisema kuwa ni heshma kwa Jeshi la Polisi kupata fursa ya kutoa mafunzo kwa wahudumu wa wageni wa kimataifa.
Katika mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam yanahusisha wanafunzi 71 kutoka vyuo mbali mbali hapa nchini vikiwemo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Diplomasia, Chuo Kikuu cha Zanzibar, Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), Chuo cha Uhasibu Arusha pamoja na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI AGOSTI 3,2019
Kiungo wa kati wa kimataifa wa Ureno Bruno Fernandes, anayehusishwa na taarifa za kuhamia Tottenham na Manchester United, ameliambia gazeti la Sporting Lisbon kuwa anataka kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu . Sporting wanaamini atataka euro milioni 70 au pauni £64m kwa ajili ya nahodha huyo mwenye umri wa miaka 24 . (Record, via Mirror)
Manchester United wanasemekana kusaini mkataba na Fernandes baada ya kombe la Super Cup la Portugal . (Express)
Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, mwenye umri wa miaka 25, anataka malipo ya pauni 350,000 kwa wiki ikiwa atajiunga na Manchester United. (Sun)Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, mwenye umri wa miaka 25, anataka malipo ya pauni 350,000
Mlinzi wa zamani wa Liverpool Andrea Dossena, mwenye umri wa miaka 37, ambaye kwa sasa yuko na Piacenza, amemueleza mchezaji mwenzake katika timu ya Palermo Dybala, ni bora ahamie ahamie Anfield kuliko Manchester United. (Liverpool Echo)
Tottenham wanataka mchezaji mbadala wa kukaba nafasi iwapo watamuuza Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, baafda ya muda wa mwisho wa kipindi cha kuhama kwa wachezajii cha waingereza kukamilika Alhamisi. Klabu za Uhispania zina hadi Agosti 31 kusaini mkataba na wachezaji . Pamoja na Fernandes, Spurs wanafanya mazungumzo na Real Betis kwa ajili ya mchezaji wa kimataifa wa Argentina Giovani lo Celso, mwenye umri wa miaka 23. (London Evening Standard)
Arsenal wanatarajia kutoa ofa mpya kwa ajili ya kiungo wa kati- wa Celtic Kieran Tierney katika siku zijazo , baada ya kukataliwa dau mbili za awali kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uskochi mwenye umri wa miaka 22 . (Sky Sports)
kiungo wa kati wa Chelsea na wa timu ya kimataifa ya Ufaransa N'Golo Kante, mwenye umri w amiaka 28, anasisitiza kuwa atakuwa Stamford Bridge msimu huu, licha ya taarifa zinazomuhusisha na Paris St-Germain. (Express)Tottenham wanataka mchezaji mbadala wa kukaba nafasi iwapo watamuuza Christian Eriksen
Hatimae Tottenham wako tayari kukamilisha mkataba wa kikanda wa pauni milioni 30 ili kusaini mkataba na wa muda mrefu na target Ryan Sessegnon mwenye umri wa miaka 19, anayetoka safu wa nyuma-kushoto ya Fulham. (Mail)
Kiungo wa kati wa Ajax m Donny van de Beek, mwenye umri wa miaka 22, amethibitisha kuwa Real Madrid wameonyesha nia kwake. (Goal)
Dau la Manchester City kwa ajili ya mchezaji wa safu ya ulinzi ya Juventus na Ureno Joao Cancelo, mwenye umri wa miaka 25, atakuwa Danilo na kuondoka klabu hiyo . Akiwa na umri wa miaka 28 mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil anaweza kujiunga na Wataliano. (Manchester Evening News)Dau la Manchester City kwa ajili ya mchezaji wa safu ya ulinzi ya Juventus na Ureno Joao Cancelo, mwenye umri wa miaka 25, atakuwa Danilo na kuondoka klabu hiyo
Brighton wanatumai kusaini mkataba na mchezaji wa Brentford wa thamani ya pauni milioni 20 kiwango alichopewa mshambuliaji wa Ufaransa Neal Maupay, mwenye umri wa miaka 22, ambaye pia anafuatiliwa kwa karibu na Sheffield United pamoja na Aston Villa. (London Evening Standard)
Florentin Pogba, mwenye umri wa miaka 28- anayechezea zaidi guu la kushoto katika timu ya kimataifa ya Guinea safu ya kati-nyuma kwa sasa anaangaliwa na MLS Atlanta United ambaye ana kaka yake anayechezea safu ya kati ya mashambulizi ya Manchester United Paul, amepewa nafasi katika timu ya ligi ya pili ya Uhispania Fuenlabrada. (AS)
Hull watapata faida ya pauni milioni £9.45 kutokana na mauzo ya mlinzi wake wa zamani Harry Maguire kutoka kwa Manchester City. The Tigers walikubali mkataba wa 15% juu ya faida ya uhamisho walipomuuza kijana huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa Leicester in 2017. (Hull Daily Mail)Manchester City wamekataa dau la pauni milioni 72 kutoka kwa Bayern Munich kwa ajili ya mshambuliaji wa Leroy Sane raia wa Ujerumani, mwenye umri wa miaka 23. (Metro)Manchester City wamekataa dau la pauni milioni 72 kutoka kwa Bayern Munich kwa ajili ya mshambuliaji wa Leroy Sane
City wanataka walipwe pauni milioni 137 kwa mauzo ya Sane ikiwa hatakuwa na haja ya kusaini mkataba wa kurefusha mkataba wake, unaomalizika Juni 2021. (Telegraph)
Mlizi wa England Harry Maguire, mwenye umri wa miaka 26, ameachwa nje ya kikosi cha Leicester kitakachocheza mechi ya urafiki baina yao na Atalanta Ijumaa kutokana na hali ya sintohfahamu juu ya hali ya yake ya baadae na Foxes wanaotaka mkataba wa pauni milioni 90 ikiwa Manchester United wanasaini mkataba nae. (Telegraph)
Dau la sasa la Manchester United kwa ajili ya Maguire ni la thamani ya pauni milioni 80
Dau la sasa la Manchester United kwa ajili ya Maguire ni la thamani ya pauni milioni 80 na klabu hiyo inaweza kutumia zaidi ya pauni milioni 150 kwa ujumla kabla ya kipindi cha mwisho cha mchakato wa uhamisho kukamilika (Independent)
Manchester United ilikataa fursa ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Juventus mwenye umri wa miaka 19 Moise Kean, na kumruhusu mtaliano huyo kuwa huru kuhamia Everton. (90min).
Chanzo - BBC
Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi mkutano wa SADC
Jeshi la Polisi nchini limeeleza kuwa limejipanga kuimarisha ulinzi wakati wa Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kutoka Makao Makuu ya Polisi, Liberatus Sabas, alisema wamejipanga na tayari wameanzisha operesheni maeneo mbalimbali kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inaimarika wakati wote wa mkutano huo.
Mkutano huo umepangwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia Agosti 17 na utahudhuriwa na wakuu wa nchi 16 wanachama.
Akizungumzia mkutano huo, Sabas alisema Jeshi la Polisi litahakikisha wageni wote wa mkutano huo watakuwa salama wakati wote wa mkutano na wanaondoka salama.
"Tumeanzisha operesheni maeneo mbalimbali kuhakikisha hali ya usalama inaimarika. Mikoa yote ambayo imepakana na Dar es Salaam na nchi kwa ujumla tutahakikisha inakuwa salama.
"Nitoe ujumbe kwa wahalifu, kama unafikiri hiki ni kipindi cha kujipatia, watajikuta wapo sehemu ambayo hawakuitegemea, watafute shughuli halali za kufanya wakati huu wa mkutano na siyo kujipanga kuja kujipatia vipato isivyo halali, wataishia mdomoni mwa simba.
"Ole wao watakaojaribu kwa maana tumejipanga vizuri, natoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mbalimbali za matishio ya kihalifu, tunaahidi kwamba tutazifanyia kazi kwa haraka ili amani na utulivu uendelee," Sabas alisema.
Alisema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vyingine vya ulinzi na usalama wamejipanga kikamilifu kuimarisha ulinzi.
Sheikh Mkuu wa Tanzania atangaza sikukuu ya Idd
Mfanyakazi Tigo kizimbani kwa kuingilia miamala ya fedha za wateja
Hamisi Singa (30), raia wa Burundi na Watanzania wanne wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka saba, likiwemo la kuingilia mfumo wa taarifa za miamala ya fedha za mawakala na kutakatisha fedha Sh26 milioni.
Mbali na Singa ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 72/2019 ni Jailos Joseph, Singa Mnunga, Japhet Mkumbo na Omari Omari.
Washtakiwa hao walipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salim Ally.
Wakisomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, ilidaiwa washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka saba likiwemo moja la kutakatisha fedha.
Washtakiwa hao walipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salim Ally.
Wakisomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, ilidaiwa washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka saba likiwemo moja la kutakatisha fedha.
Alidai katika shtaka la kwanza, washtakiwa wote wanadaiwa tarehe isiyofahamika kati ya Januari na Julai, 2019 maeneo ya Arusha, Manyara na sehemu nyingine nchini walikula njama ya kutenda kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Shtaka la pili washtakiwa wanadaiwa katika kipindi hicho kwa ulaghai walijipatia Sh 26,432,441 kwa kuhamisha fedha hizo kutoka kwa wateja wa Vodacom na Airtel.
Washtakiwa wanadaiwa katika shtaka la tatu walisambaza ujumbe usemao ‘Tuma pesa kwenye namba hii’ huku wakijua ujumbe huo wa uongo wenye nia ya kupotosha umma.
Shtaka la nne kwa washtakiwa wote, wadaiwa kusambaza ujumbe wa uongo kwa watu mbalimbali ukielekeza kutuma fedha kwenye simu iliyosajiliwa kwa majina mengine.
“Mheshimiwa Hakimu shtaka la tano lina wakabili washtakiwa wote wanadaiwa kusambaza ujumbe wa uongo kwa nia ya kujipatia fedha.
“Shtaka la sita linamkabili mshtakiwa Hamis, anadaiwa akiwa mwajiriwa wa Kampuni ya Tigo kwa ulaghai alipata uwezo wa kuingilia miamala ya fedha ya mawakala wa tigo kwa nia ya kujipatia fedha.
“Shtaka la saba kwa washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh 26,432,441 huku wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu,”alidai Wankyo.
Washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote sababu kesi hiyo imefunguliwa chini ya sheria ya Uhujumu Uchumi ambapo mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo. Kesi itatajwa Agosti 15 mwaka huu.
JEZI MPYA ZA NYUMBANI NA UGENINI ZA YANGA SC NI HIZI HAPA
Jezi ya ugenini ya Yanga SC na ya kipa kama zinavyoonekana wakati wa uzinduzi Ijumaa
SERIKALI YATENGA MILIONI 360 ZA MAJI KATA YA IHANJA MKOANI SINGIDA
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Ihanja wilayani Ikungi mkoani Singida jana.
Mbunge Kingu akikagua ujenzi wa matundu ya choo katika Shule ya Sekondari ya Masinda ambapo pia alikagua ujenzi wa madarasa ya shule hiyo na Shule ya Msingi ya Mpangwe.
Mbunge Kingu akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Masinda.
Wasanii wa Kikundi cha Nkunguli wakitoa burudani kwenye mkutano huo.
Mbunge Kingu akicheza sanjari na wasanii wa Kikundi cha Mshikamano.
Mkutano ukiendelea.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Ihanja, Juma Ntandu akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mbunge Kingu akimkabidhi kadi ya CCM Mzee, Abrahaman Moja aliyehamia chama hicho kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Ihanja, Obedi Madai akitoa taarifa ya miradi ya maendeleo iliyofanyika katika kata hiyo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
SERIKALI imetenga sh.milioni 360 kwa ajili ya kupeleka maji Kata ya Ihanja iliyopo Wilayani Ikungi mkoani Singida.
Hayo yalibainishwa jana na Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu wakati akiwahutubia wananchi wa kata hiyo katika mkutano wa hadhara ambao ulikuwa na lengo la kuelezea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanyika katika eneo hilo pamoja na kujua changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.
"Serikali imetupa sh.milioni 360 kwa ajili ya kutuwekea maji katika kata hii ambapo pia tutayafikisha vijiji vya jirani" alisema Kingu.
Kingu alisema hivi sasa kazi inayofanyika ni usanifu wa mradi huo na wakati wowote itaanza kujengwa miundombinu kwa ajili ya kusambaza maji hayo kwenda kwa wananchi.
Alisema katika kata hiyo Serikali imeweza kujenga madaraja saba yaliyopo barabara ya kwenda Kata ya Ndulu, Kituo cha Afya cha kisasa na sasa wanataka kuongeza kujenga madarasa mengine na hosteli katika Shule ya Sekondari ya Masinda ili iwe na kidato cha tano na sita kama itakavyo kuwa katika Tarafa ya Sepuka.
Kingu alisema miradi yote hiyo inafanyika kwa msaada mkubwa wa Rais Dkt. John Magufuli baada ya kuziba mianya ya fedha za serikali ambazo zilizokuwa zikitumika vibaya na mafisadi na kuwa katika jimbo hilo kuna miradi mikubwa ya maji 24.
Aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Rais Dkt.John Magufuli miradi mingi ya maendeleo imefanyika na mingine inaendelea kujengwa.
Kingu aliwahimiza wananchi kutunza miundombinu ya miradi hiyo baada ya kukamilika na kueleza kuwa itakuwa haina maana miradi iliyogharamiwa na serikali kwa fedha nyingi ikaachwa iharibike.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Ihanja, Obedy Madai, alipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali pamoja na mbunge huyo za kuwaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo na kusema miradi yote iliyofanyika katika kata hiyo thamani yake inaweza kufika sh.bilioni moja.
Jeshi la Polisi Morogoro Lakamata Vipodozi Vyenye Sumu
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzana ( TRA), limekamata katoni 230 za aina 11 tofauti ya vipodozi vyenye viambata vya sumu ambavyo vimepigwa marufuku kuingia nchini.
Vipodozi hivyo vilikuwa vikisafirishwa kwa njia ya magendo kwa kuchanganywa na mchanga wa shaba kutoka Zambia kwenda jijini Dar es Salaam.
Kukamatwa kwa shehena hiyo katika eneo la Chamwino katika, Manispaa ya Morogoro, barabara kuu ya Iringa-Morogoro, kumetokana na taarifa zilizopatikana kutoka kwa raia wema kwa polisi waliokuwa doria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, alithibitisha kukamatwa kwa vipodozi hivyo Julai 30, mwaka huu, majira ya saa sita usiku, vikiwa kwenye maboksi yaliyoviringishwa karatasi za nailoni.
Mutafungwa alisema vipodozi hivyo vilikamatwa vikiwa kwenye lori lenye namba za usajili T 367 AXY aina ya Scania, mali ya kampuni ya usafirishaji ya Thornswift ya jijini Dar es Salaam.
"Walichofanya wasafirishaji ni kuchanganya maboksi haya yenye vipodozi vilivyopigwa marufuku na mchanga huo wa shaba uliokuwa kwenye kontena, ambao ulikuwa ukisafirishwa kutoka Zambia kwenda Dar es Salaam na baadaye China," alisema.
Akavitaja vipodozi vilivyokamatwa na kiasi cha katoni kwenye mabano kuwa ni Teint Clair (86), Bronze Tone Cream (31), Perfect White Cream (32), Perfect White Lotion (15) ,sabuni ya Perfect White (12), Carot Cream (18), Diana Lotion (12), Coco Pulp Cream (14), Actif Plus Cream (10) na Extra Clair katoni nane.
Aliwataja waliokamatwa wakihusishwa na tukio hilo kuwa ni dereva wa gari, Sudi Ally (60) mkazi wa Kongowe Mzinga jijini Dar es Salaam, ambaye awali inadaiwa alijaribu kutoroka na kulitelekeza lori hilo, lakini alitiwa mbaroni baada ya kufanyika msako, Samson Mhabe (22) dereva na mkazi wa Tunduma mkoani Songwe, ambaye alikuwa msindikizaji wa mzigo huo uliokamatwa.
"Watuhumiwa walidai vipodozi hivi walivipakia baada ya kuvuka mpaka wa Tunduma upande wa Tanzania na tunawashikilia pamoja na gari lililokamatwa likisafirisha bidhaa hizi kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria ikiwamo kufikishwa mahakamani kwa kushirikiana na TRA na TBS (Shirika la Viwango Tanzania)," alisema.
DANI ALVES AREJEA KWAO BRAZIL
ANAZEEKA na utamu wake kama muwa. Huyo ndiyo Dani Alves, ambaye amemwaga wino wa kuitumikia klabu ya nyumbani kwao Brazil ya Sao Paulo baada ya kumaliza mkataba wake na PSG.
Alves amesaini na miamba hao Brazili mkataba wa hadi Desemba 2022.
Beki huyo wa kulia mwenye umri wa miaka 36 – ambaye alihamia Ulaya kwa mara ya kwanza 2002, aliposajiliwa na Sevilla akitokea Bahia – alikuwa hana timu baada ya kumaliza mkataba wake na PSG baada ya kuitumikia kwa miaka miwili katika Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1.
Alves alihusishwa na klabu yake ya zamani ya Barcelona na klabu nyingine za Ligi Kuu ya England, lakini veteran huyo alichagua kurudi nyumbani Brazil wakati akifukuzia kwenda kwenye Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.
Beki huyo aliiongoza timu ya taifa ya Brazil akiwa nahodha walipotwaa ubingwa wa Copa America kwenye ardhi ya nyumbani Julai – na kufikisha jumla ya makombe aliyotwaa kuwa 40.
Alitangaza kupitia video iliyopostiwa kwenye ukurasa wa Twitter wa klabu ya Sao Paulo, akielezea sababu za kutua katika klabu hiyo aliyokuwa akiishabikia utotoni.
"Ningeweza kuchagua timu yoyote nyingine," Alves alisema. "Lakini nimechagua kurudi Brazil, katika nchi yangu, kwa watu wangu. Kwenye klabu ninayoipenda.
"Ni kama ndoto, lakini niko hapa!"
Chanzo - Mwanaspoti
WANANCHI SINGIDA WATAKIWA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA MBUNGE WAO
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu akivikwa shada la maua baada ya kuwasili Kijiji cha Kitandaa kwa ajili ya kufanya mkutano wa hadhara wilayani Ikungi mkoani Singida jana. Mbunge Kingu alifanya mikutano miwili katika kijiji hicho na makao makuu ya Kata ya Mtunduru.
Wakina mama wa Kijiji cha Kitandaa wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea Kijiji cha Kitandaa.
Mbunge Kingu akisalimiana na wazee wa Kata ya Mtunduru baada ya kuwasili kwa ajili ya kufanya mkutano.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzì (UVCCM) wilaya ya Ikungi, Jafari Dude akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya ya Ikungi, Himid Tweve, akiimbisha wimbo wa viongozi wamechachamaa.
Diwani wa Kata ya Mtunduru Ramadhan Mpakii akizungumza.
Wanawake wa Kata ya Mtunduru wakiwa kwenye mkutano huo.
Mbunge Kingu akihutubia kwenye mkutano huo wa Kata ya Mtunduru.
Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi, Novatus Kibaji akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale, Singida
DIWANI wa Kata ya Mtunduru katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Ramadhani Mpakii amesema jitihada zinazofanywa na Mbunge wao Elibariki Kingu za kuwapelekea miradi ya maendeleo zinapaswa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo wa Jimbo la Singida Magharibi.
Akizungumza kwa nyakati tofauti jana kwenye mikutano ya hadhara aliyoandaa mbunge huyo katika vijiji vya Kitandaa na Mtunduru Mpakii alisema haijawahi kutokea tangu vianzishwe vijiji hivyo kwa kupata maendeleo makubwa katika kipindi cha miaka minne tangu mbunge huyo aingie madarakani.
" Mbunge huyu hana wa kumlinganisha naye ni msikivu na amejitahidi sana kutuletea maendeleo katika Kata yetu ebu tumuache aendelee kututumikia kwa kipindi kingine kwanza umri wake bado ni mdogo " alisema Mpakii.
Alisema katika kata hiyo ameweza kujenga shule, zahanati, na sasa amewaletea mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh.milioni 405 ambao utasambaza maji kwenye vijiji vyote vya kata hiyo.
Mpakii aliongeza kuwa tangu miaka 50 iliyopita hakujawahi kutokea Mbunge kama Kingu kwani kazi iliyofanywa na Rais Dkt.John Magufuli na Mbunge huyo ya kuwapelekea miradi hiyo itawarahisishia upatikanaji wa kupata kura nyingi katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mtaa na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.
" Kwa kazi hii kubwa iliyofanyika hatuna wasiwasi CCM itapata ushindi wa kishindo ambao haujawahi kupatikana katika uchaguzi wowote tuliowahi kuufanya" alisema Mpakii.
Akizungumza katika mkutano huo Kingu aliwashukuru wananchi na kuwaambia maendeleo hayo wanayapata baada ya Rais John Magufuli kuwabana mafisadi na matumizi mabaya ya fedha za Serikali na kuzielekeza kwa wananchi wanyonge kwa kuwapelekea miradi ya maendeleo.
Alisema haijawahi kutokea kwa kipindi chote kilicho pita ndani ya jimbo hilo kufanyika kwa miradi mingi kiasi hicho ikiwemo miradi mikubwa ya maji 24 huku mchakato wa kupata umeme wa REA ukiendelea na kuwa amepata fedha zaidi ya sh. milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika Shule ya Sekondari ya Mtunduru.
Wakati huo huo Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ikungi, Novatus Kibaji, ametoa onyo kwa wanachama wa chama hicho kuanza kujipenyeza kwenye majimbo ili kuwania nafasi za ubunge na udiwani wakati majimbo hayo yakiwa na wawakilishi.