Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Ihanja wilayani Ikungi mkoani Singida jana.
Mbunge Kingu akikagua ujenzi wa matundu ya choo katika Shule ya Sekondari ya Masinda ambapo pia alikagua ujenzi wa madarasa ya shule hiyo na Shule ya Msingi ya Mpangwe.
Mbunge Kingu akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Masinda.
Wasanii wa Kikundi cha Nkunguli wakitoa burudani kwenye mkutano huo.
Mbunge Kingu akicheza sanjari na wasanii wa Kikundi cha Mshikamano.
Mkutano ukiendelea.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Ihanja, Juma Ntandu akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mbunge Kingu akimkabidhi kadi ya CCM Mzee, Abrahaman Moja aliyehamia chama hicho kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Ihanja, Obedi Madai akitoa taarifa ya miradi ya maendeleo iliyofanyika katika kata hiyo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
SERIKALI imetenga sh.milioni 360 kwa ajili ya kupeleka maji Kata ya Ihanja iliyopo Wilayani Ikungi mkoani Singida.
Hayo yalibainishwa jana na Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu wakati akiwahutubia wananchi wa kata hiyo katika mkutano wa hadhara ambao ulikuwa na lengo la kuelezea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanyika katika eneo hilo pamoja na kujua changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.
"Serikali imetupa sh.milioni 360 kwa ajili ya kutuwekea maji katika kata hii ambapo pia tutayafikisha vijiji vya jirani" alisema Kingu.
Kingu alisema hivi sasa kazi inayofanyika ni usanifu wa mradi huo na wakati wowote itaanza kujengwa miundombinu kwa ajili ya kusambaza maji hayo kwenda kwa wananchi.
Alisema katika kata hiyo Serikali imeweza kujenga madaraja saba yaliyopo barabara ya kwenda Kata ya Ndulu, Kituo cha Afya cha kisasa na sasa wanataka kuongeza kujenga madarasa mengine na hosteli katika Shule ya Sekondari ya Masinda ili iwe na kidato cha tano na sita kama itakavyo kuwa katika Tarafa ya Sepuka.
Kingu alisema miradi yote hiyo inafanyika kwa msaada mkubwa wa Rais Dkt. John Magufuli baada ya kuziba mianya ya fedha za serikali ambazo zilizokuwa zikitumika vibaya na mafisadi na kuwa katika jimbo hilo kuna miradi mikubwa ya maji 24.
Aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Rais Dkt.John Magufuli miradi mingi ya maendeleo imefanyika na mingine inaendelea kujengwa.
Kingu aliwahimiza wananchi kutunza miundombinu ya miradi hiyo baada ya kukamilika na kueleza kuwa itakuwa haina maana miradi iliyogharamiwa na serikali kwa fedha nyingi ikaachwa iharibike.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Ihanja, Obedy Madai, alipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali pamoja na mbunge huyo za kuwaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo na kusema miradi yote iliyofanyika katika kata hiyo thamani yake inaweza kufika sh.bilioni moja.
0 comments:
Post a Comment