Sunday, 30 December 2018

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally Atoa Maagizo MAZITO Kwa Naibu Waziri wa Kilimo

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amemwagiza Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa kutafuta fedha za kuwalipa wakulima wa zao la kahawa mkoani Kagera kwa bei inayoridhisha kulingana na gharama watumiazo katika uzalishaji.
 
Dk Bashiru alitoa agizo hilo juzi mbele ya wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa huo wanaotoka wilaya za Ngara Kyerwa na Karagwe alipokutana nao mjini hapa.
 
Katibu mkuu huyo wa CCM alitoa agizo kwa Bashungwa ambaye ni Mbunge wa Karagwe (CCM) aliyekuwapo kwenye
kikao hicho kwenda kuhakikisha bei inaboreshwa ili kuwavutia wakulima wa zao hilo.
 
Alisema licha ya Serikali kuzuia magendo ya kahawa kutoka Kagera kuingia Uganda lakini inanunuliwa kwa kificho kisha inasafirishwa na kuwekwa katika kasha au kopo la robo kilo hadi nje ya nchi ikiwa na thamani kubwa hasa China.
 
“Waganda wananunua kahawa kwa magendo wanaikaanga na kuifunga kwa kuweka picha ya mwanamke mrembo wa Kiganda, wanaisafirisha hadi China kupitia bandari yetu inauzwa kakopo Sh40,000 iweje mkulima apatiwe Sh1,000?” alihoji Dk Bashiru.
 
Pia alimuagiza Mkurugenzi Halmashauri ya Ngara, Aidan Bahama kutowanyang’anya wananchi ardhi kwa madai ya kuwagawia wawekezaji kutoka Korea Kusini.
 
“Nilikupigia simu kukuzuia sasa nakupa ‘live’ sitaki kusikia wawekezaji wa nje wanapewa ardhi bila kufuata utaratibu wa kuridhiwa kwanza na mkutano mkuu wa vijiji,” alisema.
 
Mkuu Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali, Marco Gaguti alisema katika kupambana na biashara ya magendo ya kahawa wilaya ya Misenyi imekamata magari 12 yenye tani zaidi ya 60 na pikipiki zilizokuwa zikisafirisha Uganda.


from MPEKUZI http://bit.ly/2Qc1023
Share:

Lugola Atoa ONYO Kwa Wanaotumia Misikiti na Makanisa Kuvuruga Amani ya Nchi

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema Serikali haitawavumilia wanaotumia taasisi za dini ikiwamo misikiti na makanisa kuvuruga amani.
 
Alisema hayo juzi kwa niaba ya Rais John Magufuli wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Kamati ya Amani ikiwa ni kusheherekea Sikukuu ya Krismasi.
 
Waziri huyo alisema bado kuna viashiria vya mtu mmoja mmoja na vikundi vya watu wanaotaka kuvuruga amani, vitendo ambavyo Serikali haitavivumilia.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum alisema ni mara ya kwanza kwa Waislamu kualikwa na kukaa pamoja katika kusheherekea Sikukuu ya Krismasi.
 
“Pamoja na kuwapo kwa mahusiano mazuri kati ya Wakristo na Waislamu nchini bado kumekuwa na shida kwa baadhi ya watu pale tunapokaa pamoja katika sikukuu hizi na kushindwa kutofautisha kusherehekea na kutambua,” alisema.
 
Naye Askofu wa Kanisa la Ufufuo, Paul Bendera alisema siku zote amani inatoka kwenye moyo wa mtu. 

“Haiwezekani tunakakaa pamoja akatokea mtu akatugawa, ili kuendeleza amani iliyopo tunapaswa kuthamini viongozi wetu na kutii mamlaka zao.”


from MPEKUZI http://bit.ly/2SxGtat
Share:

Saturday, 29 December 2018

KIJANA INITIATIVE KUWAINUA WAJASIRIAMALI NA WASIOJIWEZA MOROGORO

Taasisi ya Kijana Initiative Foundation imeungana na familia mia moja (100) zinazoishi katika mazingira magumu wakiwemo wajane pamoja na wanawake wajasiriamali wadogo,ili kubadilishana mawazo na kula chakula cha pamoja katika ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Jordan mkoani Morogoro. Hafla hiyo imefanyika Leo 29 Desemba 2018 na kujumuisha Viongozi mbalimbali akiwemo Ndg Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro ambaye alikuwa mgeni rasmi, pamoja na Ndg Said Said Nguya mdau wa maendeleo na wanawake wajasiriamali pamoja na familia zinazoishi katika mazingira magumu ambazo zimeonesha furaha ya wazi kwa msaada…

Source

Share:

TAMASHA KUBWA LA MKESHA WA MWAKA MPYA KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA,KIINGILIO BURE


Tamasha kubwa la mkesha wa kufunga 2018 na kufungua mwaka 2019 linatarajiwa kufanyika Desema 31 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mkesha huo utakaokuwa wa aina yake unatarajia kumdondosha Mwanamuziki wa nyimbo za injili kutoka nchini Nigeria anaejulikana kwa jina la Chris Shalom, anayetamba na wimbo wake maarufu uitwao 'my beautifier' na nyingine nyingi.

Pamoja Na Chris Shalom pia waimbaji wengine mbalimbali mahiri kutoka hapa nchini akiwemo Jesica Honore, Goodluck Gosbert, Joel Lwaga Na John Lisu wanatarajiwa kutumbuiza katika mkesha huo.

Mkesha wa mwaka 2019 umeandaliwa na Nabii (prophet) Clear Malisa wa Passion Java ministry, kutoka ubungo kibangu jijini Dar es Salaam.Waigizaji/wachekeshaji na watu maarufu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa pia kuwepo akiwemo Pastor Kuria kutoka show ya churchchill nchini Kenya.

Katika tamasha hilo hakuna kiingilio na usafiri utatolewa kwa watu wote katika vituo vyote vikubwa vya usafiri Dar es Salaam.Mkesha wa mwaka 2019, umedhaminiwa Na Clouds media group, Elishadai shopping center Na Fair Travel adventures.


Share:

SIMBA WAILAZA SINGIDA UNITED 3 -0 , KICHUYA BALAA MTUPU

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya ameamua kumtumia salamu kocha Mkuu, Patrick Ausems baada ya kuonyesha ufundi wa kucheka na nyavu leo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliochezwa uwanja wa Taifa kutokana na kuanzia benchi mara nyingi.

Kichuya aliwanyanyua mashabiki kwa kutoa pasi ya bao la kwanza dakika ya 17 lililofungwa na John Bocco ambaye kwa sasa anafikisha bao la tatu kwenye Ligi.

Dakika ya 49 Kichuya alifunga bao la pili akiwa ndani ya 18 kwa mguu wa kulia lililomshinda mlinda mlango wa Singida United kabla ya kulazimisha kuingia ndani ya 18 na kufunga bao la tatu dakika ya 54 kwa mguu wake wa kulia akimalizia pasi za Clytous Chama.

Licha ya kufungwa mabao hayo bado Singida United walijitahidi kufanya mashambulizi kwa kushtukiza lango la Simba hali iloyomfanya mlinda mlango Aishi Manula kuwa katika kazi nzito kuokoa jahazi la Simba na kufanikiwa.
Share:

AFISA UHAMIAJI AFARIKI BAADA KUNYWA POMBE KUPITA KIASI


Na John Walter-Babati
Afisa uhamiaji Mkoani Manyara aliyefahamika kwa jina la Peter Kambanga (35- 40) amepoteza maisha usiku wa alhamisi Disemba 27 kwa kile kinachoelezwa kunywa pombe kupita kiasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Agustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi hilo lilifika katika chumba alichopanga marehemu, mjini Babati na kukuta kimefungwa kwa ndani na kuwalazimu kuvunja ndipo walipoukuta mwili huo.

Kamanda Senga amesema kuwa chanzo cha kifo hicho ni unywaji wa pombe kupindukia na kukosa hewa na kuongeza kuwa alikuwa akiishi mwenyewe katika chumba alichokuwa amepanga.

Aidha Senga amesema mwili wa Marehemu umesafirishwa leo Jumamosi Disemba 29,2018 kwenda wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma kwa ajili ya taratibu za Mazishi.

Kamanda Senga ametoa wito kwa wakazi wa Manyara kuishi pamoja na ndugu au familia zao pindi wanapokuwa mbali kikazi.

Sambamba na hilo jeshi la polisi mkoani Manyara limewasishi wananchi kunywa pombe kistaarabu na kuendesha magari kwa uangalifu huku likizidi kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu katika kipindi hiki cha siku kuu za mwisho wa mwaka.

Share:

Utabiri Uliotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Kuanzia Usiku Huu




from MPEKUZI http://bit.ly/2rYaGnn
Share:

SHILINGI BILIONI 8.5 ZAELEKEZWA MACHINJIO YA VINGUNGUTI

Na Heri Shaban Serikali imetenga shilingi bilioni 8.5 kwa ajili ya Machinjio ya Kisasa eneo la Vingunguti Wilayani Ilala. Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam Paul Makonda katika hafla ya kutoa zawadi ya Mwaka Mpya wakati akigawa ng’ombe kwa Jeshi la Polisi na Hospitali za Mkoa wa Dar es Salam. “Serikali hivi karibuni inatarajia kuzindua ujenzi wa machinjio ya Kimataifa Rais John Magufuli ataweka jiwe la Msingi katika machinjio haya ya VINGUNGUTI yatakayo gharimu bilioni 8.5 “alisema Makonda. Makonda alisema katika Afrika Mashariki machinjio hayo ya…

Source

Share:

Mawaziri wakutana Mbeya kumpongeza Rais Magufuli

Mawaziri wameungana kumpongeza Rais John Magufuli kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini kwa kasi kubwa.

Pongezi hizo zimetolewa leo Jumamosi Desemba 29, 2018 jijini Mbeya katika kongamano la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) lililofanyika kitaifa jijini humo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema Rais Magufuli amefanya kazi kubwa kuhakikisha elimu inapatikana kwa wote bila kujali hali zao kiuchumi.

"Mheshimiwa Rais ameweza kusaidia kutolewa kwa elimu bure jambo lililopelekea ongezeko la watoto wanaoandikishwa katika shule zetu," amesema Profesa Ndalichako.

Naye Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angellina Mabula amesema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli imesaidia kwa kiasi kikubwa kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi.

"Serikali inaandaa mfumo ambao utasaidia kuondokana na tatizo la ardhi kumilikiwa na mtu zaidi ya mmoja," amesema Mabula.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso amesema miradi iliyotakiwa kutekelezwa katika awamu hii ni 1,810 lakini mpaka sasa miradi 1,659 imekwisha kutekelezwa.


from MPEKUZI http://bit.ly/2BLPi9b
Share:

Mbowe Atuma Ujumbe Toka Gerezani

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Seif Sharif Hamad, ameweka wazi mipango ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe baada ya kutoka gerezani ni kuungana na vyama vingine vya upinzani.

Katibu Mkuu huyo ameyasema  hayo baada ya kutumia siku ya Jumamosi ya leo kuwatembelea viongozi Mwenyekiti Mbowe pamoja na Mbunge Esther Matiko katika gereza la Segerea baada ya kufutiwa dhamana.

"Nimeitumia fursa ya kuonana na Mhe. Freeman Mbowe na Mhe. Esther Matiko kuwaeleza kuhusu  Azimio la Zanzibar na mikakati ya vyama sita vya siasa kurudisha demokrasia Tanzania. Mhe. Mbowe amenambia yuko pamoja na sisi na akitoka tu gerezani ataungana nasi kuendeleza atakapopakutia" Amesema Maalim Seif

Aidha kiongozi huyo amebainisha kwamba viongozi hao wawili bado wapo imara na wana imani kwamba haki itatendeka juu yao.


from MPEKUZI http://bit.ly/2GIspcw
Share:

UJENZI WA BARA BARA YA NJOMBE KUELEKEA RUVUMA WANUKIA

Na Amiri kilagalila Naibu waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Elias kwandikwa amewahakikishia wananchi wa Njombe kuanza kwa ujenzi wa bara bara kuu ya Njombe, Ruvuma ili kuondokana na uchakavu wa bara bara hiyo kwa baadhi ya maeneo kutokana na kudumu tangu ilipo jengwa. Naibu waziri ameyasema hayo mkoani Njombe wakati akizindua ukumbi mkubwa na wakisasa wenye ukubwa wa sikwea mita 1000 ukiwa na kumbi tatu ndani uliopo Hagafilo halmashauri ya mji wa Njombe unaomilikiwa na mbunge wa jimbo la Njombe mjini Edward france Mwalongo. “watu wa Njombe mmekuwa na…

Source

Share:

YANGA WAICHAPA MBEYA CITY 2 - 1 ....MAKAMBO NOMAA


Kikosi cha Yanga kilichocheza dhidi ya Mbeya City.

Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania klabu ya Yanga leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Kwa matokeo ya leo Yanga sasa inaendelea kuongoza ligi ikiwa na alama 50 ikifuatiwa na Azam FC wenye alama 40 baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 leo kutoka kwa Mtibwa Sugar.

Mshambuliaji wa Yanga mkongomani Heritier Makambo ndio alikuwa shujaa wa Yanga akifunga mabao yote mawili katika dakika za 11 na 41 kipindi cha kwanza wakati bao la Mbeya City likifungwa na Iddy Selemani.

Makambo sasa amefikisha mabao 11 kwenye ligi na kuongoza orodha ya wafungaji.

Yanga sasa imebaki kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo kwenye ligi kuu msimu huu baada ya wenzao Azam FC kutibuliwa rekodi na Mtibwa Sugar huko Turiani Morogoro.

Wekundu wa msimbazi ambao wapo katika nafasi ya 3 wanashuka dimbani saa 1:00 kukipiga na Singida United kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam.
Via >>Eatv
Share:

Ben Paul, Depay, uso kwa uso Dubai

Kupitia ukurasa wa star wa Bongo Fleva @iambenpol nimeona picha akiwa na star wa zamani wa Manchester United @memphisdepay kwa sasa anacheza Lyon ya Ufaransa.

Nikatamani kujua Ben Paul amekutanaje na Depay na kama walipiga story hadi kufikia kupiga picha. Ndugu yetu akanisimulia mwanzo mwisho mambo yalivyokuwa.

“Nimekutana nae hapa Dubai kwenye hotel ambayo nimefikia, nimeingia hapa juzi yeye sijui yupo hapa tangu lini.”

Jana wakati naenda kupata lunch ndio nikakutana nae, yeye pia alikuwa anaenda lunch…akaniangalia halafu akasema: “Wewe kuna rafikiyangu umefanananae.”

“Nilikuwa sijamjua nikawa najiuliza huyu jamaa ni nani lakini sura yake ilikuwa inaniijia baada ya kumkaribia nikamuuliza wewe ni Memphis akasema ndiyo yeye na pale yupo holiday.

“Tukaongea kidogo masuala ya muziki akasema ametoa wimbo, nikaangalia instagram yake nikaona, baada ya hapo tukapiga story kidogo na picha tukaenda kula chakula tukaachana.”

“Story nyingi zilikuwa kuhusu muziki, anauliza Afrika vipi tunafanyaje, tukabadilishana mawasiliano tutakuwa tunawasiliana labda baadaye chochote kinaweza kutokea.”



from ShaffihDauda http://bit.ly/2EVDOnx
Share:

CCM Arusha wakutana kumpongeza Rais Magufuli kwa Kufuta Kikokotoo

Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa Arusha kimempongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake mzuri katika kipindi cha miaka mitatu ikiwemo kurejesha kikokotoo cha zamani cha mafao ya wafanyakazi.

Wakitoa tamko lao leo Jumamosi Desemba 29, 2018 katika mkutano uliofanyika ukumbi wa CCM mkoa wa Arusha na kuwashirikisha wanaccm kutoka wilaya zote tano za mkoa wa Arusha, wamesema Rais John Magufuli ndiye mzalendo wa kweli.

Akitoa salamu kwa niaba ya wabunge wa mkoa Arusha, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ambaye pia ni mbunge wa Ngorongoro amesema katika kipindi cha miaka mitatu Rais Magufuli amefanya kazi ya mfano.

Ole Nasha amesema ndani ya miaka mitatu, Rais Magufuli amenunua ndege, amejenga madarasa na vivuko, ameanza ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es salaam hadi Dodoma.

"Sio haya tu Rais wetu ameanza mradi mkubwa wa umeme wa Stiglers Gorge na jana amefanya kubwa kutetea wafanyakazi kurejesha kikokotoo cha zamani," alisema.

Mkuu wa wilaya ya Arusha, Gabriel Daqaro amesema, kazi alizofanya Rais ni kubwa na inawahakikishia CCM ushindi mwaka 2020.

Katika mkutano huo uliokuwa unaongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Loota Sanare pia ulihudhuriwa na mkuu wa mkoa Arusha Mrisho Gambo, wabunge na madiwani.


from MPEKUZI http://bit.ly/2Al01ra
Share:

PICHA: Watumishi Jijini Mwanza Waandamana Kuunga Mkono Agizo La Rais Magufuli Kuhusu Kikokotoo

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali wakipita katika barabara ya Kenyatta wakielekea kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ili kufikisha ujumbe wao wa kumpongeza Rais John Magufuli baada ya kuiagiza mifuko ya hifadhi kuendelea kulipa malipo ya waastafu kwa kutumia utaratibu wa zamani wakati wadau wakiendelea na majadiliano hadi 2023.

Watumishi mbalimbali wa umma wakiimba wimbo wa mshikamano baada ya kuhitimisha maanandamano yao ya kuunga mkono agizo la Rais John Magufuli la kuiataka mifuko ya hifadhi ya jamii kuendelea na utaratibu wa zamani kulipa mafao ya wastaafu badala ya kutumia kikokotoo kipya. Picha zote na Daud Magesa
Waandamani hao wakiingia kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza jana kuunga mkono agizo la Rais John Magufuli kwa mifuko ya hifadhi ya jamii kuendelea kuwalipa watumishi waliostaafu mafao yao kwa kutumia utaratibu wa zamani.


from MPEKUZI http://bit.ly/2SmraRH
Share:

Waziri Mkuu Majaliwa Atembelea Mradi Wa Uendelezaji Miji Ya Kimkakati Katika Jiji La Dodoma

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea Mradi wa Uendelezaji  wa Miji ya Kimkakati katika jiji la Dodoma na kukagua ujenzi wa maegesho ya malori makubwa  katika eneo la Nala na uboreshwaji wa mandhari ya eneo la kupumzikia la Chinangal ijijini Dodoma.

Pia amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi andelee kutenga maeneo ya mapumziko ili wananchi wapate sehemu za kukutana na kubadilishana mawazo baada ya kumaliza kufanya kazi.

Waziri Mkuu amekagua maeneo hayo leo (Jumamosi, Desemba 29, 2018) ambapo ameupongeza uongozi wa jiji la Dodoma kwa kubuni wazo hilo na kusema kwamba ni muhimu kwa miji mikubwa kutenga maeneo ya kwa ajili ya mapumziko.

Amesema lazima jiji la Dodoma lipangwe kisasa  na amewataka wahandisi wahakikishe maeneo ya mapumziko yatengwa na yanatumika kama ilivyokusudiwa. Pia amemtaka Mkurugenzi wa Jiji, Kunambi aendelee kusimamia ujenzi wa kimkakati ndani ya jiji hilo.

”Hatuwezi kuwa tumejaza nyumba kila eneo, watu hawana mahali pa kupumzika na kukutana na marafiki zao plan ya Chinangali Park ni nzuri, Jiji la Dar es Salaam plan ya awali kulikuwa na maeneo ya mapumziko lakini watu wa Idara ya Ardhi waliyauza.”

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amekagua utekelezaji wa agizo alilolitoa Oktoba 21, 2018  kwa uongozi wa jiji la Dodoma la kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa  kwa ajili ya kuchezea watoto na kuziba barabara ya tisa  katika Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Madukani jijijini Dodoma. 

 Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na utekelezwaji wa agizo lake baada ya kutembelea eneo hilo na kukuta uzio umebomolewa na sasa kuna bustani iliyojengwa kwa ajili ya mapumziko na pia barabara imefunguliwa na wananchi wanaendelea kuitumia kama ilivyokuwa awali.

 Uzio huo ambao mbali na kujengwa katika eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto kwenye mtaa wa Mji Mpya kata ya Madukani pia uliziba barabara ya tisa, hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Waziri Mkuu ameendelea kusisistiza uongozi wa jiji kutenga ardhi na kupima viwanja kwa ajili ya matumizi mbalimbali yakiwemo ya biashara, makazi, taasisi, huduma za jamii, viwanda pamoja na maeneo ya wazi kwa ajili ya mapumziko.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma amesema jiji la Dodoma ni miongoni mwa majiji manane nchini yanayotekeleza mradi wa uboreshaji wa miji ya kimkakati unaofadhiliwa na Serikali kupitia mkopo wa Benki ya Dunia.

Amesema katika jiji la Dodoma mradi huo unahusisha ujenzi wa miundombinu ya barabara katika maeneo ya Kikuyu, Chidachi, Kinyambwa, Itega, Njedengwa, Mapinduzi, Ilazo, Ipagala, Chamwino, Kilimani, Majengo, Mlezi pamoja na maingilio na stendi kuu ya mabasi na soko kuu zenye jumla ya urefu wa kilomita 26.6.

Mkurugenzi huyo amesema barabara hizo zinajengwa kwa kiwango cha lami, pia zitawekwa taa za barabarani takriban 925 zinazotumia mfumo wa umeme wa jua. Hata hivyo mradi huo utahusisha ujenzi wa kituo cha maegezo ya malori makubwa takribani 300 katika eneo la Nala.

Ameongeza kuwa mradi huo unahusisha ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi na soko kuu katika eneo la Nzuguni, ujenzi wa vituo sita vya watembea kwa miguu, ujenzi wa vizimba saba vya kukusanyia taka ngumu, uboreshaji wa mandhali ya eneo la kupumzikia katika eneo la Chinangali na ujenzi wa mtaro wa maji ya mvua wenye urefu wakilomita 6.5 katika eneo la Ipagala.


from MPEKUZI http://bit.ly/2QVeQLn
Share:

CCM Watuma Rambirambi Kifo Cha Mzee Ndejembi

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Mzee Pancras Mtemi Ndejembi  ambaye amekuwa sehemu ya mzee maarufu na wanaoheshimika katika Chama kada wa Chama na Kiongozi Mstaafu wa  Chama na Serikali.

Ndejembi amefariki katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alikopelekwa jana Ijumaa baada ya hali yake kubadilika ghafla.


from MPEKUZI http://bit.ly/2SrF7xJ
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger