Thursday, 27 December 2018

RAISI TRUMP ALISHTUKIZA JESHI LA MAREKANI NCHINI IRAQ

Share:

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI DEC 27 2018

Real Madrid wanataka kumpa ofa mchezaji wa Chelsea raia wa Uhispania Isco, 26, na kiungo wa kati wa Croatia Mateo Kovacic ambaye tayari yuko kwa mkopo huko Stamford Bridge - kama sehemu ya makubaliano kumsaini mshambuliaji wa Chelsea raia wa Ubelgiji Eden Hazard, 27. (Onda Cero, via Metro)

Juventus hawawezi kumuuza kiungo wa kati wa Brazil mwenye miaka 28 Douglas Costa, ambaye amehusishwa na Manchester City na Manchester United, mwezi Januari. (Calciomercato)
West Ham wametoa ofa ya pauani milioni 6.5 kwa kiungo wa kati wa Chile Gary Medel, 31, aliyekatalikwa na klabu ya Uturuki ya Besiktas. (Talksport)

Kiungo wa kati wa Tottenham mbelgiji mwenye miaka 31 Mousa Dembele, ambaye mkataba wake unaisha anatafutwa na meneja wa Monaco Thierry Henry. (Le Sport 10 - in French)

Watford wana hofu wanaweza kumpoteza kiungo wa kati Mfaransa Abdoulaye Doucoure, 25, kwenda Paris St-Germain mwezi ujao na wanaweza kumwendea aliyekuwa mchezaji wa Nice Mfaransa Adrien Tameze, 24, achukue nafasi yake. (Mail)
Mkurugenzi mkuu wa CSKA Moscow Roman Babaev anaaminia mchezaji wa mkopo wa Everton Nikola Vlasic, 21, anataka kubaki kwenye kalabu lakinia anasema klabu haitakuw na uwezo wa kumsaini kabisa mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia. (Liverpool Echo)

Meneja wa Newcastle United Rafael Benitez hafikirii kuwa klabu hiyo itakuwa tayari kumsaini mchezaji mapema mwezi Januari. (Chronicle)

Mmiliki wa Nottingham Forest Evangelos Marinakis anafikiria kumfuta meneja Aitor Karanka baada ya mechi bila ushindi ripoti za mzozo wa wachezaji kwenye klabu. (Mail)Ernesto Valverde

Kocha wa Barcelona Ernesto Valverde bado haijakijulisha klabu hiyo ya Uhispania ikiwa ataendelea na mkataba kwa mwaka wa tatu huko Nou Camp. (Marca)

Atletico Madrid wanajaribu kuuuzuia Bayern Munich kufufua kipenge cha kukata mkataba wa mlinzi mwenye miaka 22 mfaransa Lucas Hernandez cha euro milioni 80 mwezi Januari. (Marca)

Meneja wa West Brom Darren Moore anasema hana wasi wasi kuhusu uwezekano wa kuwindwa na vilabu vya Ligi ya Premia mchezaji straika Jay Rodriguez, 29. (Times - subscription required)
Share:

MKANDARASI MUNGAI ASAIDIA YATIMA WA KITUO CHA DBL IRINGA.

  NA FRANCIS GODWIN, IRINGA Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi ya GNSM Geofrey Mungai ametoa msaada wa chakula na nguo wa zaidi ya shilingi milioni 1 kwa watoto yatima wa kituo cha Daily Bread Life Tanzania (DBL) mkimbizi mjini Iringa kwa ajili ya kusherekea siku kuu ya Krismass na mwaka mpya. Mungai amekabidhi msaada huo jana na kuwa amelazimika kutoa msaada huo kwa watoto hao kama njia ya kuwajali na kuwafanya yatima hao kufurahia sikukuu kama watoto wenye wazazi na sehemu ya kuhamasisha jamii kuendelea kuwakumbuka yatima wakati wa sikukuu…

Source

Share:

LISSU: NITAGOMBEA URAIS UCHAGUZI UJAO 2020.

  Wakati vuguvugu la Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 likianza chini kwa chini, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema yupo tayari kugombea urais ikiwa vyama vya upinzani vitampa ridhaa hiyo. Lissu ambaye yupo nchini Ubelgiji akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30, Septemba 7 mwaka jana akiwa Dodoma na watu wasiojulikana, amesema hayo jana wakati akizungumza na gazeti la Mwananchi kuhusu maendeleo ya afya yake. Mwanasiasa huyo amesema yeye ni mwanachama wa Chadema na hawezi kufanya jambo pasi na kuridhiwa na chama chake au vyama…

Source

Share:

INASIKITISHA! …WANAWAKE WANAVYOIGEUZA MITANDIO KITANZI CHA KUJINYONGEA.

  Na Bakari Chijumba, Mtwara. Matukio ya watu kuripotiwa kujinyonga yameonekana kushika kasi huku matumizi ya mtandio kama kifaa cha kujinyongea yakishika kasi. Katika matukio mawili yaliyoripotiwa mfululizo yanathibitisha hilo ambapo la kwanza, mkazi mmoja wa Kijiji cha Nakayaya, wilayani Tunduru mkoani Ruvuma Awetu Makunula (44), amejinyonga hadi kufa kwa madai ya kuchoka kusumbua wanafamilia kutokana na hali ya afya yake. Taarifa za tukio hilo zinaeleza kuwa Makunula alikutwa akining`inia juu ya mti wa mkorosho jirani na nyumba ya wazazi wake. Mume wa marehemu Makunula, Salum Namtikwe, amesema usiku walilala…

Source

Share:

DC MPWAPWA ATAKA MIFUGO ITUMIKE KUKUZA UCHUMI WA NCHI.

  Na Stephen Noel Mpwapwa -Dodoma Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Mhe Jabir Shekimweri, amewataka wafugaji kuzingatia kanuni bora za ufugaji ili kuweza kuwa na mifugo bora inayo weza kukidhi kwenye soko la kimataifa. Shekimweri ametoa kauli hiyo wilaya hapa alipo kuwa na akizindua zoezi la Uogeshaji Mifugo wa mifugo iliofanyika katika Kata ya Mazae kijiji/kata cha kisokwe. Amesema lengo zoezi hilo ni kuweza kuboresha mifugo kwa kuwakinga na magonjwa ambayo husababishwa na kupe. Katika ufunguzi huo Mhe Shekimweri amesisitiza umuhimu wa kuwa na mifugo yenye afya bora.…

Source

Share:

KATIBU MKUU CCM TAIFA ASHIRIKI KUZINDUA KAMPENI YA KUTOKOMEZA UDUMAVU WA WATOTO KAGERA.

  Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally jana akiwa mkoani Kigoma ameanzisha kampeni ya kutokomeza udumavu wa watoto Mkoani Kagera. Amezungumza hayo akiwa katika ukaguzi wa kiwanda cha kuchakata Nyanya ili kupata “(tomato sauce”) Kiitwacho VICTOLIA EDIBLES LTD kilichopo eneo la Kafunjo kata Butelankuzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera. Akiwa katika ukaguzi huo Dr.Bashiru Ally amewataka viongozi wote wa Chama na serikali kuendeleza kampeni hii ili kupunguza na kukomesha udumavu wa watoto Mkoa wa Kagera na nchini kwa ujumla. Amesisitiza kuwa Kagera ni Mkoa wenye vyakula…

Source

Share:

RAISI MAGUFULI APOKEA MAJINA YA VIGOGO WA KUWAKATA MISHAHARA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania ATCL Ladislaus Matindi, ameeleza tayari ameshamkabidhi Rais Magufuli orodha ya majina ya viongozi ambao walikatisha safari zao za ndege katika shirika hilo licha ya kukatiwa tiketi za serikali.

Akizungumza Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi, amedai wameshatekeleza agizo hilo la Rais Magufuli ambalo alilitoa kwenye hafla ya upokeaji wa ndege mpya ya Tanzania A220-300 aina ya Airbus.

Matindi amesema “majina ya vigogo husika tumeshayakabidhi kwa Rais, tangu tumeelekezwa tulifanyia kazi maelekezo hayo na kisha tukayakabidhi sehemu husika,”

“Siwezi kutaja ni vigogo wa kada gani, wasiliana na Ofisi ya Rais wataweza kuwa na majina pamoja na Idara au Taasisi wanazotoka, sisi tumepeleka orodha,” ameongeza Luhindi.

Akizungumza Desemba 23, 2018 Rais Magufuli alisema “nimeambiwa pia baadhi ya tiketi huwa zinakatwa na watendaji wa serikali halafu wakati wa mwisho hawasafiri, anatakiwa kusafiri kwenye ndege na amekatiwa tiketi na serikali, lakini hasafiri, hivyo kwa nafasi ile ndege inaenda tupu,” Viongozi wanaokatwa mishahara wafika kwa Magufuli.
Chanzo:Eatv

Share:

ALIYETEKWA ZAIDI YA MIAKA 30 APATIKANA

Mwanamke aliyeokolewa na polisi baada ya kushikiliwa mateka kwa miaka 30 (wapili kushoto) na mwanae wa miaka tisa wameungana na familia yao.

Operesheni ya kumnasua mwanamke huyo ilifanyika kwa ushirikiano wa polisi wa nchi za Argentina na Bolivia.

Mahala ambapo alikuwa akishikiliwa mwanamke huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 45 lilikuwa halifahamiki toka miaka ya 80.

Hata hivyo, mapema mwaka huu, polisi walipata taarifa kuwa alikuwa akishikiliwa katika eneo la Bermejo, kusini mwa Bolivia baada ya uchunguzi, polisi walifanikiwa kuitambua nyumba aliyokuwemo na kufanikiwa kumuokoa akiwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka tisa.

 Katika taarifa iliyotolewa na polisi nchini Argentina wanasema mwanamke huyo amefanikiwa kurejeshwa na kuungana na familia yake katika mji wa Mar del Plata.

Taarifa hiyo hata hivyo haikusema ni nani aliyetekeleza tukio la utekaji miaka 32 iliyopita, huku pia jina la mwanamama huyo pamoja mtoto wake hayatajwa.

Chanzo: Bbc
Share:

Video: YOUNG KILLER FT DELA -WAKIPEKEE

Msanii wa muziki wa hip hop, Young Killer Msodoki ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao, Wakipekee akiwa amemshirikisha muimbaji Dela kutoka nchini Kenya.

Share:

TUNDU LISSU KUGOMBEA URAIS 2020?

Wakati vuguvugu la Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 likianza chini kwa chini, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema yupo tayari kugombea urais ikiwa vyama vya upinzani vitampa ridhaa hiyo.

Lissu ambaye yupo nchini Ubelgiji akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30, Septemba 7 mwaka jana akiwa Dodoma na watu wasiojulikana, amesema hayo jana wakati akizungumza na Mwananchi kuhusu maendeleo ya afya yake.

Mwanasiasa huyo alisema yeye ni mwanachama wa Chadema na hawezi kufanya jambo pasi na kuridhiwa na chama chake au vyama washirika wa Chadema kwani kufanya hivyo ni kinyume cha taratibu na maadili.

Kauli ya Lissu kuhusu kugombea urais mwaka 2020 imetokana na swali aliloulizwa kutokana na kuwa miongoni mwa wanasiasa wa upinzani wanaotajwatajwa, “Wakikaa katika vikao na kunipa bendera, nitakubali kubeba msalaba huo mzito kwa mikono miwili.”

Pia aliulizwa, ikiwa hataombwa na chama atajitosa mwenyewe kuwania nafasi hiyo? Rais huyo wa zamani wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) alisema, “Maadili yangu, unaambiwa ukiwa katika chama lazima upewe fursa kwa hiyo nitasubiri fursa hiyo.”

Katika Uchaguzi Mkuu uliopita wa 2015, vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF vilimsimamisha Edward Lowassa kuwania nafasi ya urais na licha ya kushindwa Dk John Magufuli wa CCM, alipata kura nyingi ambazo hazijawahi kufikiwa na mgombea yeyote wa upinzani.

Katika uchaguzi huo, ilishuhudiwa kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi wa vyama vingi ulipoanza mwaka 1995, upinzani ukipata kura zaidi ya milioni sita ikiwa ni tofauti ya kura milioni mbili dhidi ya mshindi wa nafasi hiyo.

Lowassa alipata kura milioni 6.01 sawa na asilimia 39.97 huku Dk Magufuli akiibuka mshindi kwa kupata kura milioni 8.9 sawa na asilimia 58.46.

Kuhitimisha matibabu Desemba 31

Share:

KOCHA MKUU WA YANGA AREJEA DAR


Mwinyi Zahera

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Mwinyi Zahera amerejea nchini usiku wa kuamkia leo Desemba 27,2018, ambapo mara tu baada ya kufika amesema programu zote za maandalizi ya mechi dhidi ya Mbeya City anaziacha kwa kocha msaidizi Noel Mwandila.

Akiongea mara baada ya kutua uwanja wa ndege wa Julius Nyerere akitokea Ufaransa, Zahera amesema kuelekea mechi hiyo hataingilia chochote kwenye maandalizi kwani kocha msaidizi ameshamalizana na wachezaji.

''Kwasababu wachezaji wamefanya program zote za mechi timu nitaiacha kwa Noel aendelee na mchezo huu ambao najua wachezaji wanajua umuhimu wake kwetu'', amesema Zahera.

Zahera ambaye alikwenda nchini Ufaransa kushughulikia masuala yake binafsi ya kibiashara ameongeza kuwa lengo lake ni kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa wanaongoza ligi na wachezaji wanalijua hilo.

Yanga ambayo inaongoza ligi, itakuwa ugenini Desemba 29, 2018 kukipiga na Mbeya City katika mchezo wa raundi ya 18 kabla ya kurejea Dar es salaam kucheza na Azam FC na kukamilisha michezo 19 ya mzunguko wa kwanza.
Share:

MWANAMKE AJIUA KWA MADAI YA KUCHOKA KUSUMBUA FAMILIA

Mkazi wa Kijiji cha Nakayaya, wilayani Tunduru mkoani Ruvuma Awetu Makunula (44), amejinyonga hadi kufa kwa madai ya kuchoka kusumbua wanafamilia kutokana na hali ya afya yake.

Taarifa za tukio hilo zinaeleza kuwa Makunula alikutwa akining`inia juu ya mti wa mkorosho jirani na nyumba ya wazazi wake, mjini hapa.

Mume wa marehemu Makunula, Salum Namtikwe, alisema kuwa usiku walilala wote na kabla ya tukio hilo aliamka majira ya saa 11 alfajiri na kumuaga kuwa anatoka nje kwa ajili ya kufagia nje ya nyumba yao ili amalize shughuli hiyo mapema na kwenda shambani.

Alisema baada ya kupewa maelezo hayo yeye aliendelea kulala, lakini baadaye alishangaa kupata taarifa za mkewe kukutwa akiwa amejinyonga hadi kufa baada ya kujining`iniza katika mti uliopo jirani na nyumbani kwa wazazi wake.

Alisema baada ya kupatiwa taarifa hizo aliamka na kwenda eneo la tukio na kumtambua marehemu na baadaye walitoa taarifa kwa viongozi wa serikali kwa ajili ya taratibu za kuuondoa mwili huo katika eneo hilo.

Aidha, akisimulia maisha ya mkewe, alisema kabla ya tukio hilo alikuwa akisumbulia na maradhi mbalimbali mara kwa mara jambo ambalo lilikuwa likimnyima amani wakati wote.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, ASCP Gemin Mushy, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kusema polisi inaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo hicho.

Kamanda Mushy, alisema katika tukio hilo mwanamke huyo alijinyonga kwa kutumia mtandio alio jifunga shingoni na upande mwingine kuufunga juu ya mti wa mkorosho.
Share:

KIGWANGALLA AMVAA MASHA KUHUSU FASTJET...WAMESHINDWA KUFANYA BIASHARA WAO WENYEWE


Pichani, Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla, Kulia ni Lawrence Masha

Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla ameitetea Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukanusha kwamba haijazuia vibali vya kuingiza ndege mpya kwenye Kampuni ya Fastjet Tanzania inayomilikiwa na aliyekuwa Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Waziri Kigwangalla amesema kwamba kwa taarifa alizonazo ni kuwa Kampuni ya Fastjet imeshindwa kufanya biashara nchini na sio inavyosemekana kuwa imezuiwa kuingiza ndege mpya na serikali.

Masha akizungumza na chombo kimoja cha habari nchini, siku ya jana alisema “TCAA inasema ili niweze kuingiza ndege hiyo nimalize kwanza madeni yote, baadhi ya madeni tayari yamelipwa na Fastjet Plc mengine Fastjet Tanzania. Tayari tumemaliza, lakini fedha imeisha, kwa kuwa tayari fedha nyingine tulizitumia kutimiza matakwa yao, wangeniruhusu nifanye kazi ili nipate fedha ya kulipa yaliyobaki''.
Pichani, Ndege ya Fastjet.

Akijibu kuhusu malalamiko hayo Kigwangalla amesema "Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba wameshindwa kufanya biashara wao wenyewe! Na hakuna sababu ya kuwazuia kuingiza ndege yao mpya. Ni kwamba wazungu wamejiondoa wamebaki wazawa na hawajazuiliwa kuingiza ndege zao" Kigwangalla

Hivi karibuni Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga nchini (TCAA) ilisema Shirika la Ndege la fast jet kwa sasa halina hali nzuri na limepoteza sifa ya kuendelea na huduma hiyo, hivyo ilitoa notisi ya siku 28 ya nia ya kulifuta kabisa shirika hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Hamza Johari, amesema 'Notice' hiyo inaanza Disemba 17 hadi Januari huku akitoa tahadhari kwa wananchi kutotumia usafiri wa shirika hilo ili kuepuka usumbufu.

Aidha amesema kuwa pamoja na kuzuiwa kufanya huduma nchini, lakini hawatakiwi kuondoka kwakuwa wanadeni, "Mamlaka imezuia ndege hiyo (Fastjet) isiondoke hapa nchini kwa sababu Shirika linadaiwa madeni mengi, TCAA pekee inadai zaidi ya bilioni 1.4".
Share:

WANANCHI WAKIMBIA KIJIJI KUKWEPA MSAKO WA VYOO

Wananchi wa vitongoji vilivyopo kijiji cha Muungano, wilayani Momba, wameyakimbia makazi yao wakihofia kukamatwa baada ya kuwapo kwa msako wa kuwakamata wasiokuwa na vyoo.

Kata ya Kamsamba ni miongoni mwa kata wilayani Momba ambayo imekumbwa na ugonjwa wa Kipindupindu na watu zaidi ya 100 kuugua na kusababisha serikali kuweka mikakati ya kudhibiti ugonjwa huo.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kamsamba, Gerad Makwasa, alisema viongozi ngazi ya wilaya wakiwa na askari mgambo, walifika katika bonde la Kamsamba kuendesha doria kuwasaka wasiokuwa na vyoo, hali iliyowalazimu wakazi wa kijiji hicho kukimbilia kusikojulikana. 

Ofisa Tarafa ya Kamsamba, Zakayo Mwasomola, alisema juzi walikaa kikao na Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Kamsamba kujadili hali hiyo ambapo alisema kata zilizokumbwa zaidi ni ugonjwa huo ni Ivuna wagonjwa 35, Samang’ombe 35 na Kamsamba 34 na aliyefariki dunia ni mmoja.

Alisema ugonjwa huo uliibuka Novemba 11 mwaka huu na jitihada zinafanyika kudhibiti hali hiyo.

Alisema wamekuwa wakihamasisha watu kuweka hali ya usafi wa mazingira,kujenga vyoo bora,kuchemsha maji ya kunywa na kunawa kwa sabuni pindi watokapo chooni.

“Ni kweli wananchi karibu wote wa kijiji cha Muungano wameyakimbia makazi yao wakihofia kukamatwa, lakini tumeandika majina yao, tunafahamu kuwa watarejea tu kwani wameacha familia zao wengine wake zao ni wajawazito,’’alisema Mwasomola.

Mwenyekiti wa kamati ya Maafa,Juma Irando, alisema hiyo ni
operesheni endelevu ya kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo bora ambacho kitakuwa kinatumika.

Irando ambaye pia ni Mkuu wa wilaya hiyo, alisema kata hiyo imekumbwa na Kipindupindu kutokana na watu wengi kutokuwa na vyoo na walitoa muda wa kujenga kwa hiyari kuanzia Novemba 30 mwaka huu hadi Desemba 30 mwaka huu.

Alisema huo ulikuwa ni mkakati wa kimkoa ambapo tayari
siku zimekwisha na sasa wapo katika utekelezaji.

Alisema kwamba kitendo cha wanakijiji hao kukimbia sio dawa ya kumaliza tatizo, kwani operesheni hiyo ni endelevu.
Share:

Wednesday, 26 December 2018

DIWANI AJIUA KWA KUTUMIA MTANDIO


Diwani wa zamani wa kata ya Nyerere, Unguja Asha Ali Abei amejinyonga hadi kufa usiku wa kuamkia leo Jumatano Desemba 26, 2018.

Akizungumza leo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja, Kheri Musa amesema marehemu ambaye kwa miaka ya nyuma alikuwa diwani, alikutwa amekufa kwa kujinyonga akitumia mtandio alioufunga katika dirisha, tukio lililotokea katika shehia ya Magomeni.

Baadhi ya majirani wa marehemu walisema kwamba walipata taarifa za kifo hicho asubuhi baada ya mtoto wa marehemu kupiga kelele.

Sheha wa shehia ya Magomeni, Rajab Ali Ngauchwa amesema si vyema wananchi kuchukua hatua za haraka katika mambo yanayowachanganya.

Amesena ni vyema familia kukutana na kujadili ili kupata ufumbuzi wa tatizo kuliko watu kuchukua uamuzi kama huo wa kujitoa uhai.
Share:

Makubwa Haya : KIJANA AFARIKI KWENYE SHINDANO LA KUFANYA MAPENZI..ROUND 7 TU KWISHA HABARI YAKE



Makubwa Haya!! ndivyo unaweza kusema... Ama kweli hili ni tukio la kufungia mwaka 2018. Katika hali isiyokuwa ya kawaida Kijana aliyejulikana kwa jina la Davy amefariki dunia baada ya kufanya mapenzi na kwenda round saba mfululizo na mwanamke aliyejulikana kwa jina la Loveth nchini Nigeria.

Watu hawa walibeti juu ya nani anatisha zaidi kwa kufanya mapenzi muda mrefu zaidi ,basi Davy akaweka dau la Naira 50,000 ambazo ni shilingi elfu 14 za Kenya ama laki 3 za Tanzania kwa atakayeshinda.

Isome zaidi hapa chini

A middle-aged man, simply known as Davy, has died in a popular hotel in Ikotun area of Lagos State during a sex competition with a lady identified as Loveth.

It was gathered that the late Davy had argued with Loveth on who can last longer in a sex bout.

Both claimed they were stronger and refused to admit defeat.

During the argument, Davy staked N50,000 on the condition that if Loveth defeats him during the romp, she will take the money.

Loveth agreed, moved into the hotel and booked for a chalet.

It was gathered that while the marathon sex lasted, Davy pulled through to the sixth round but Loveth was unshaken till the seventh round when he collapsed and died on top of her.

She then raised the alarm and contacted the hotel management, who handed her over to the Ikotun Police Division while the body of the deceased was deposited at an undisclosed hospital for autopsy.

Loveth was later transferred to the SCIID Panti, Yaba, where she told investigators what transpired between her and the late Davy. The fate of Loveth will depend on the outcome of the autopsy.

Source - Guardian.ng
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger