Tuesday, 25 December 2018
MPACHIKA MABAO TAMBWE AWEKA REKODI HII YA HATARI
NA KAROLI VINSENT MFUMANIA nyavu wa kuogopwa zaidi wa timu ya Yanga, Mrundi, Amis Tambwe, ameweka historia ya kipee jana kwenye michuano ya Kombe la FA kwa kufunga mabao matatu ‘hat-trick’. Mrundi huyo ambaye ni hatari kwa kufunga mipira ya kichwa ameweka Rekodi hiyo ambayo ni ya kwanza katika mashindano ya Kombe la FA tangu yaanze msimu huu kwani hakuna mchezaji mwingine aliyefunga mabao hayo kwenye mchezo mmoja. Tambwe ambaye hivi karibuni alikuwa hapewi nafasi kubwa ya kuanza kwenye kikosi cha Yanga jana alikuwa lulu kwa kuing’arisha Yanga dhidi ya…
SAKATA LA MBOWE NA MATIKO KUSOTA GEREZANI,CHADEMA YAPIGA ODI KWA WANASHERIA WA NCHI ZA NJE
NA KAROLI VINSENT CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinajipanga kuongeza wanasheria ikiwemo kuwatoa nje ya nchi ili kuhakikisha wanamtoa Gerezani Mwenyekiti Taifa wa chama hicho ,Freeman Mbowe pamoja na Mbunge wa Tarime mjini,Ester Matiko katika kesi ya “kisiasa” wanayokabiliwa nao. Mbowe na Matiko wapo Gerezani yapata mwezi sasa baada ya kufutiwa dhamana Novemba mwaka huu baada ya kudaiwa kukiuka masharti ya dhamana . Taarifa ambazo Mtandao wa DarMpya.com imezipata kutoka ndani ya Chadema inasema viongozi wa chama hicho wanajipanga kuongeza wanasheria wa ndani kwenye kesi hiyo pamoja na kutoa…
WHOZU AFUNGA MWAKA NA NDINGA JIPYA,ASEMA MATUNDA YA TIGO FIESTA
Mchekeshaji na mburudishaji chipukizi hapa Tanzania, Whozu amefanikiwa kutimiza ndoto yake ya kumiliki gari, hii ni baada ya kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye mikoa 13 kwenye tamasha la Togo Fiesta.
Whozu ameshea na mashabiki wake picha ya gari hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kuandika “Wengi walikuwa wananitizama kama mchekeshaji lakini clouds wakanitizama kama entertainer…wakanifungulia dunia nakunipa Nafasi ya mimi kujifungulia maisha…. Kuperfom Fiesta 13 kati ya Fiesta 15 Mungu ni mwema #mynewride mpiraaa mpyaaaa napiga round nazunguka dar nzima nikimaliza naunganisha kwenda moshi..MUSIC PAYS #MatundaYaTigofiesta“
Kwa upande mwingine, Whozu amewashukuru pia mashabiki wake, vyombo vya habari na Maproducer waliomsaidia kwa kuandika “Niwashukuru pia Mshabiki zangu Asanteni sana kwa support Mwenyezi Mungu Awabariki sana.Shukrani pia Kwa Media Zote Nawashukuru kwa Nafasi yangu Kwenu🙏 Shukrani pia kwa Producers @osam_lucifer Hakika najua unafuraha Uliniamini Nami nikakuaminisha. Pia Zombie Langu @s2kizzy haha Nilikwambia Lakini! Asante pia Directors @lucca_swahili & @joowzeytz May God bless you all Fam & Fans“.
Whozu mwaka huu (2018) amefanya vizuri kwenye muziki na ngoma yake ya Huendi kwa Mbinguni, na ndio wimbo uliomfanya atumbuize karibia mikoa yote iliyopitiwa na Fiesta.
IDADI YA VIFO KUTOKANA NA KIMBUNGA CHA TSUNAMI YAONGEZEKA INDONESIA
Idadi ya vifo iliyotokana na janga la kimbunga cha Tsunami kilichoikumba Indonesia inaendelea kuongezeka. Watu 373 wamethibitishwa kupoteza maisha na wengine 1,400 wamepata majeraha.
Kwa mujibu wa DW Swahili, Idadi hiyo ya vifo inategemewa kuongezeka zaidi, huku watu 128 wakiwa hawajulikani walipo hadi sasa hasa katika maeneo yaliyoathirika vibaya ya pwani ya kisiwa cha magharibi cha Java na kisiwa cha kusini cha Sumatra.
Juhudi za kutafuta miili ya mamia ya watu pamoja na kuwanusuru waliopata majeraha zimeongezeka leo hii kufuatia kimbuga cha Tsunami cha hivi karibuni kilichopiga nchini Indonesia. Wataalamu wamekusanya ushahidi unaothibitisha kwamba kimbunga hicho kilichochewa na mlipuko wa volkano.
Ni kwa mara ya pili kimbunga cha Tsunami kinapiga Indonesia ndani ya mwaka huu. Matetemeko makubwa ya ardhi yalichochea kimbunga hicho cha Tsunami na kupiga kisiwa cha Sulawesi mwezi Septemba.
WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUHUJUMU SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA ATCL
Mawakala 10 wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi ikiwamo kulisababishia Shirika hasara, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha Sh. milioni 10.8.
Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ally Salum.
Wakili wa Serikali, Wankyo Simon, aliwataja washtakiwa hao kuwa ni, Fabian Ishengoma (34), Adam Kamara (27), Marlon Masubo (29), Neema Kisunda (24), Alexander Malongo (29) na Tunu Kiluvia (32).
Wengine ni Jobu Mkumbwa (30), Mohammed Issah (38), Godfrey Mgomela, Absalom Ambilikile na Janeth Lubega.
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa kati ya Machi 10 na Oktoba 9, mwaka huu, mahali tofauti jijini Dar es Salaam na Mwanza washtakiwa kwa pamoja wakiwa mawakala wa ATCL, walilisababishia Shirika hilo hasara ya Sh.10,874,280.
Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa tarehe na mahali pa shtaka la kwanza, washtakiwa wote kwa pamoja walijipatia fedha hizo.
Shtaka la tatu, ilidaiwa kuwa tarehe na mahali pa tukio la kwanza na la pili, washtakiwa wote walijipatia fedha hizo wakati wakijua ni mazalia ya udanganyifu yaliyotokana na utakatishaji fedha.
Hakimu alisema mahakama yake haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi na kwamba washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote hadi pale Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), atakapotoa kibali au upelelezi utakapokamilika itahamishiwa Mahakama Kuu Divisheni ya uhujumu uchumi na rushwa.
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Hakimu Salum alisema kesi hiyo itatajwa Januari 7, 2019, washtakiwa wamepelekwa mahabusu.
KOCHA AGEUKA KUWA MDHAMINI AIPIGA JEKI YANGA , KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA MBEYA CITY
Klabu ya soka ya Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wake wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Mbeya City Jumapili hii hivyo kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amewaomba wanachama kuichangia timu ili iweze kufafiri kwa ndege na kiasi kitakachopelea yeye ataongezea.
Zahera ambaye hayupo nchini amedai kitendo cha timu kusafiri tarehe 27 na kwenda kucheza tarehe 29 sio rahisi kwenda kwa basi hivyo ni lazima iende kwa ndege ili iweze kupata matokeo.
''Mimi kocha Mwinyi Zahera naomba wanachama waichangie klabu iweze kusafiri kwa ndege kwenda Mbeya ili tukacheze na tupate matokeo na mimi binafsi nitaongezea kiasi kitakachopelea'', amesema Zahera.
Aidha Zahera ambaye ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DR Congo amesema matokeo ya Yanga ni muhimu kwa wanachama na timu nzima ili kuendelea kuongoza ligi kwahiyo kila mmoja anayo sababu ya kuhakikisha timu inasafiri vyema.
Yanga kwasasa inaongoza ligi ikiwa na alama 47 kwenye mechi 17 ikifuatiwa na Azam FC yenye alama 40 kwenye mechi 16 huku Simba ikiwa nafasi ya 3 na alama 30 kwenye mechi 13.
Chanzo: Eatv
MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU MATATANI KWA KULAWITI WATOTO WENZAKE
Mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi ya Wilunze mwenye umri wa miaka 14 anatuhumiwa kuwalawiti wanafunzi wenzake ambapo katika tukio la hivi karibuni alimlawiti mtoto wa miaka mitatu.
Hayo yalibainishwa na Mtendaji wa Kijiji Cha Wilunze Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Georgina Richard wakati akizungumza juzi katika mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa vijiji na kata kupitia mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia, mimba na ndoa za utotoni unaotekelezwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Woman Wake Up (WOWAP).
Alieleza kuwa tukio la kulawitiwa mtoto wa kiume wa miaka mitatu lilitokea Novemba 26, mwaka huu kijijini hapo. Alisema mtuhumiwa huyo ni mtoro wa kudumu na mara ya mwisho alikuwa akisoma darasa la tatu Shule ya Msingi Wilunze.
Alisema siku ya tukio mtuhumiwa huyo alimuingiza mtoto huyo kwenye nyumba ambayo haijamalizika na kumfanyia kitendo hicho.
“Aliyeshuhudia kitendo hicho ndio alikwenda kutoa taarifa kwa mama wa mtoto ambapo mtoto huyo mdogo alipekekwa hospitali kupimwa na kukutwa na manii mapajani ambazo zimekauka, na alikuwa ameingiliwa kinyume na maumbile,” alisema.
Alisema ndipo mama huyo alipewa barua na kwenda kuripoti tukio katika kituo cha Polisi Chamwino. Mtendaji huyo wa Kijiji alisema mtuhumiwa huyo bado hajulikani alipo na kesi hiyo iko kwenye upelelezi.
“Hali ya mtoto inaendelea vizuri, tukapata taarifa kuwa mama mtuhumiwa alimfuata mama wa mtoto aliyelawitiwa ili waweze kuelewana nikawaambia sitaki kusikia kitu kama hicho wasubiri sheria ifuate mkondo wake,” alisema.
Alisema kutokana na uchunguzi aliofanya baada ya tukio hilo ikabainika kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akiwalawiti baadhi ya watoto wa darasa la kwanza na la pili.
“Tulikwenda hadi shuleni tukawabaini watoto waliofanyiwa kitendo hicho wako wa kike na wengine wa kiume, tukagundua watoto walikuwa wakifanyiwa vitendo hivyo lakini walikuwa hawasemi,” alisema.
Alisema mtuhumiwa huyo mara kadhaa amekuwa akifikishwa ofisi ya Kijiji kutokana na utoro na mpaka sasa anaendelea kutafutwa ili sheria ichukue mkondo wake.
Chanzo : Habarileo
Monday, 24 December 2018
UVCCM YAMKINGIA KIFUA RAIS MAGUFULI, YAAHIDI KUMLINDA KATIKA VITA YA UJENZI WA UCHUMI
Na Augustine Richard Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM leo Desemba 24, 2018 umejitokeza hadharani na kuweka bayana mambo makuu nane yaliyofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli ndani ya miaka mitatu ya uongozi wake ambayo ni viashilia vikubwa vya ujenzi wa uchumi wa kati katika Taifa la Tanzania. Akizungumza na wandishi wa habari katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM zilizopo Upanga Jijini Dar Es Salaam Katibu Mkuu Mwalimu Raymond Mwangwala ameainisha mambo makuu nane ikiwemo,…
MBUNGE WA SIMANJIRO AIMWAGIA SIFA UJAMAA COMMUNITY RESOURCE TEAM - UCRT
Mkuu wa wilaya ya Simanjiro,Mhandisi Zephania Chaula(katikati) akifuatilia mazungumzo ya mbunge wa jimbo hilo,James Ole Millya(kushoto) na Katibu Tawala wa wilaya ya Simanjiro,Zuwena Omary.
Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoa wa Manyara,James Ole
Millya akizungumza kwenye mkutano wa kukabidhi Hati za Kimila kwa ajili ya malisho ya mifugo katika kijiji cha Lerumo Kata ya Ruvuremit.
Mkuu wa wilaya ya Simanjiro,Mhandisi Zephania Chaula(kushoto) akipokea zawadi ya Ndama kutoka kwa wananchi wa Kijiji cha Lerumo.
Mbunge wa jimbo la Simanjiro,James Ole Millya (katikati) akipokea zawadi ya Ndama kutoka kwa wananchi wa Kijiji cha Lerumo.
Mkuu wa wilaya ya Simanjiro,Mhandisi Zephania Chaula(kushoto) akifurahia zawadi ya fimbo aliyokabidhiwa na wananchi wa Kijiji cha Lerumo Kata ya Ruvuremit baada ya kukabidhi Hati za Kimila kwa vijiji Sita.
Kwaya ya Lerumo ikitumbuiza wakati wa mkutano huo.
Wananchi wakifurahia baada ya Hati za kimila kukabidhiwa kwa viongozi wao.
Mratibu wa taasisi ya Ujamaa Community Resouce Team wilaya ya Simanjiro.Edward Loure (wa pili kushoto) akipokea zawadi ya Ndama kutoka kwa wananchi wa Kijiji cha Lerumo.
Mkuu wa wilaya ya Simanjiro,Mhandisi Zephania
Chaula(wa pili kushoto) akikabidhi Hati ya Kimila za nyanda za malisho zilizoandaliwa na taasisi ya Ujamaa Community Resource Team(UCRT) katika mkutano uliofanyika Kijiji cha Lerumo Kata ya Ruvuremit,Hati za Kimila zilikabidhiwa kwa vijiji Sita.
Furaha ya kukabidhiwa Hati ya Kimila .
Kwaya ya Lerumo ikitumbuiza wakati wa mkutano huo.
Picha zote na Filbert Rweyemamu
WADAU WA ELIMU WACHANGIA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 250 UJENZI WA MADARASA BUSEGA SIMIYU
Na Stella Kalinga, Simiyu Wadau mbalimbali wa elimu wamechangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega mkoani Simiyu katika Harambee iliyofanyika Mjini Nyashimo, ambapo zimepatikana jumla ya shilingi 254, 969,000/= fedha taslimu zikiwa ni shilingi 15,360,000/= ahadi shilingi 241,809,000/= na mifuko ya saruji 127. Akiongea na wadau hao Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo ambaye alialikwa kama Mgeni rasmi wa Harambee hiyo, Luteni Kanali Josephat Mshashi, Mkuu wa Kikosi cha 27 Makoko Musoma amesema upo umuhimu wa kuhakikisha watoto wanapata elimu kwa kuwa elimu…
CHADEMA WAJA NA MKAKATI HUU WA KUHAKIKISHA WANAMCHOMOA MBOWE GEREZANI
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeanza kuchangishana fedha kuongeza nguvu ya wanasheria katika kesi zinazowakabili wanachama na viongozi wake wakiwamo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko. Mbowe na Matiko ambao wanakabiliwa na kesi ya uchochezi inayowakabili pamoja na viongozi wengine saba wa chama hicho, walifutiwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 24 katika ofisi za Chadema Kanda ya Pwani zilizopo Magomeni Makuti, Mwenyekiti wa kanda hiyo, Frederick Sumaye, amesema wanataka haki itendeke haraka ili viongozi…
WAAGIZAJI MIZIGO YA NJE WATAKIWA KUKATA BIMA KWA KAMPUNI ZA NDANI.
NA KAROLI VINSENT Mamlaka ya usimamizi wa shughuli za bima Tanzania (TIRA) kwa kushirikiana na Chama Cha mawakala wa forodha na uondoshaji mizigo Tanzania ,(TAFFA) wamewataka wafanyabiashara na waagizaji mizigo kutoka nje kuhakikisha kuwa wanakatia bidhaa zao bima kupitia kampuni za ndani zenye usajili. Agizo hilo limetolewa Jijini Dar es Salaam na Rais wa (TAFFA) Stephen Ngatunga,wakati wa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuwahamasisha waagizaji hao kutumia bima za kampuni za ndani. Amesema kwa kipindi kirefu waagizaji wa bidhaa nje ya nchi walikuwa wakikata bima kupitia makampuni ya nje…
YEYOTE ATAKAYEKATIZA MDOMONI MWA YANGA AJIHESABU AMEKWISHA,YAENDELEZA DOZI YAKE ,HUYO TAMBWE ACHA–
NA KAROLI VINSENT YEYOTE atakayekatiza mbele ya Yanga basi ajue amekwisha ndivyo unaweza kusema baada ya Mabingwa hao wa kihistoria kuendeleza kutoa kichapo kwa yeyote yule wanayekutana naye ambapo leo wameifumua bila huruma timu ya Tukuyu Stars kwa mabao 4-0 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho nchini. Yanga ambayo mpaka sasa haijafungwa hata mechi moja kwenye michezo yote ya Ligu kuu Tanzania Bara ambapo katika mchezo huo na Vijana hao kutokea Mkoani Mbeya imepata mabao yake kupitia kwa Amis Tambwe aliyefunga matatu huko moja likiwekwa kimiani na Mfumania Nyavu hatari…