Friday, 21 December 2018

MSOMI WA UDSM AJIUA KWA KUJIRUSHA GHOROFA LA ROCKY CITY MALL MWANZA...AKUTWA NA UGORO


Musa Ally (25), mkazi wa Kiloleli wilayani Ilemela jijini Mwanza anayedaiwa kuwa na elimu ya chuo kikuu/shahada sayansi ya kompyuta aliyoipata Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) amejirusha katika jengo la la Rocky City Mall na kufariki dunia.


Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Desemba 21, 2018 kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Advera Bulimba amesema tukio hilo limetokea leo saa saba mchana.


Imeelezwa kuwa Musa alichukua uamuzi huo kutokana na kuwa na msongo wa mawazo, kukosa kazi.

Bulimba amesema kijana huyo alionekana akiwa amelewa kupita kiasi na tangu Desemba 16, 2018 na alikamatwa na kuwekwa kituo cha polisi Kirumba, kilevi kilipopungua aliachiwa.

Amesema katika uchunguzi wa awali marehemu alibainisha kuwa alikuwa na msongo wa mawazo kwa sababu ya kukosa kazi licha ya kuwa na elimu ya juu.

Bulimba amesema baada ya polisi kumuachia alikwenda kunywa tena pombe na baadaye kujirusha kutoka ghorofa ya tatu na kukutwa na pombe kali na ugoro.

“Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa kijana huyo amesema amejiingiza kwenye ulevi na asilaumiwe mtu yeyote. Amesema amechukua uamuzi huo yeye binafsi, pia akidai yeye ni masikini hana baba wala mama,” amesema Bulimba.


Amesema mwili umehifadhiwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi licha ya kutotaja jina la hospitali hiyo.


Bulimba amesema, maandishi aliyokutwa nayo marehemu yalisomeka kwamba “yeye ana shahada sayansi ya kompyuta aliyoipata Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).”

Na  Jonathan Musa na Jesse Mikofu, Mwananchi



Share:

Picha:WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA RAFIKI SDO WAFANYA ZIARA KATIKA MAKUMBUSHO YA MWALIMU J.K NYERERE

shirika lisilo la kiserikali la Rafiki Social Development Organization -SDO linalojihusisha na miradi mbalimbali ya kijamii ikiwa ni pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia limefanya ziara mkoani Mara kwa kutembelea makumbusho ya mwatogo wilayani Butiama alipozikwa muasisi wa taifa la Tanzania hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere

Katika ziara hiyo Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Rafiki SDO Gelard Ng’ong’a ameiomba jamii kujenga utaratibu wa kutembelea makumbusho hayo ili waweze kujifunza historia ya Baba wa taifa kwa kuangalia mifano halisi inayopatikana katika makumbusho hayo . 

‘tujifunze historia ya mwalimu na kuna mambo mazuri aliyafanya mwalimu na sisi pia tutumie nafasi hiyo kuishi kama mwalimu ili tuwe wazalendo katika nchi yetu na tufanye kazi tupate maendeleo’ alisema Ng’ong’a 

Kwa upande wao baadhi ya wafanyakazi wa shirika la Rafiki  SDO wamesema katika makumbusho hayo wamejifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na namna Baba wa Taifa alivyoipenda nchi, huku wakisema kuwa wapo tayari kufuata nyayo za baba wataifa hasa katika utendaji kazi ili kupata maendeleo zaidi. 

Ziara ya Rafiki SDO mkoani mara ni sehemu ya kusheherekea siku ya rafiki na familia Rafiki Family Day

baadhi ya wafanyakazi wa shirika la Rafiki SDO wakiwa katika kaburi la  baba wa taifa  hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere

Kaburi la Baba wa Taifa hayati Mwalimu Nyerere
Mwongozaji wa wageni wanaofika katika makumbusho ya makazi ya baba wa Taifa bi. Gaudencia Waziri akitoa ufafanuzi juu makumbusho hayo kwa wafanyakazi wa Rafiki SDO
Bi gaudencia Waziri akitoa ufafanuzi katika makaburi ya wazazi wa hayati Mwalimu J.K Nyerere
Makaburi ya wazazi wake Hayati Baba wa Taifa  Mwalimu Nyerere
baadhi ya wafanyakazi wa Rafiki SDO wakicheza mchezo wa bao alilokuwa akicheza Hayati  Baba wa taifa na wageni wake waliokuwa wakimtembelea enzi za uhai wake nyumbani kwake Mwitongo Butiama .


Moja ya picha kubwa inayopatikana katika makumbusho ya Mwalimu J.K Nyerere , picha hii inaonesha baadhi ya picha za Baraza la mawaziri la mwisho la raisi wa kwanza Mwl. J.K Nyerere wakati akielekea kung'atuka madarakani mwaka 1985

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Rafiki SDO Gelard Ng'ong'a akimsalimia  mtoto wa sita Hayati Baba wa taifa   Mwalimu  Nyerere, Madaraka Nyerere mara baada ya kudhuru makumbusho ya makazi ya baba taifa katika kijiji cha Mwitongo, Butiama mkoani Mara


baadhi ya staff wa Rafiki SDO wakiwa pamoja mmoja ya watoto wa baba wa taifa , Madaraka Nyerere
utalii wa ndani unaendelea na hapa mkurugenzi mtendaji wa Rafiki SDO, Gelard Ng'ong'a akitazama baadhi ya kumbukumbu zinazopatikana katika makumbusho hayo


Hii ni radio ambayo alikuwa akiitumia Hayati Mwalimu Nyerere kwa ajili ya kusikiliza habari mbalimbali ,hayati Mwalimu pia alipenda kutumia radio hii katika baadhi ya ziara  zake za ndani na nje ya nchi ,Redio hii alipewa nchini ujerumani mwaka 1996


Share:

SAKATA LA KULAZWA MAKABURINI : RC HAPI AAGIZA KATIBU WA BAVICHA AKAMATWE NA POLISI POPOTE ALIPO


 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi ameliagiza Jeshi la polisi mkoani humo kufanya uchunguzi juu ya tuhuma zilizosambaa mtandaoni zikimuusisha na imani za kishirikina.

Hapi amesema hadi leo Ijumaa Desemba 21, 2018 jeshi la polisi limegundua aliyetunga uzushi huo ni Katibu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) wilaya ya Temeke, Hilda Newton.

“Nimeagiza popote alipo huyo katibu wa Bavicha akamatwe atoe maelezo ya alichokizusha mtandaoni na athibitishe alichokiandika," amesema Hapi.

Hapi amesema amepitia akaunti ya Hilda Newton na kugundua ni tabia yake kuzusha vitu vya uongo mtandaoni.

Amesema kumtaja kwa kimo chake hajaona kama ni udhalilishaji bali alitofautisha watu waliokuwa katika picha hiyo.

"Nimemtaja kuwa ni mfupi na kweli ni mfupi ukilinganisha na mtu aliyekuwa amesimama naye katika picha niliyoiposti kumtaka akajisalimishe."

Awali baada ya kutakiwa kujisalimisha, Hilda alinukuliwa akisema kwamba hatokwenda polisi kujisalimisha kama alivyotakiwa na Hapi.


Na Berdina Majinge, Mwananchi 
Share:

MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUPIGWA SHOTI YA UMEME JUU YA NGUZO


Fundi wa umeme

Mwanafunzi mmoja wa chuo cha mafunzo Wilaya ya Wete, Pemba aliyejulikana kwa jina la, Hemed Suleima Seif (40) amefariki baada ya kupigwa na shoti ya umeme wakati akijaribu kufanya matengenezo.

Inaelezwa kuwa kabla ya kukutwa na umauti, mwanafunzi huyo alikuwa akifundishwa ujuzi wa matengenezo ya Umeme kwa vitendo na mwalimu wake.

Akithibisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa polisi mkoa wa Kaskazini Pemba, Sheikhan Mohammed Sheikhan amesema tukio hilo limetokea saa 1:45 za asubuhi, wakati marehemu akiwa chini ya mwalimu wa fani hiyo wakijaribu kurekebisha kasoro katika moja ya nguzo ya jengo.

“Ni kweli tumepokea taarifa kutoka kwa wenzetu wa chuo cha mafunzo kuwa kuna mwanafunzi anaetambuliwa kwa jina la Hemed Suleiman, amefariki baada ya kupigwa na shoti ya umeme,” amesema.

“Tayari maiti imekabidhiwa jamaa zake kwa mazishi na jeshi la polisi inatoa pole kwa wafiwa,” ameongeza.

Kamanda Sheikhan pia amesema uchunguzi wa awali uliofanywa na madaktari wa hospitali ya Wete umebainisha kuwa marehemu aliathirika mwili mzima. Amewaomba wananchi kuwa waangalifu wakati wanapokua katika harakati zao hasa za kushughlikia masuala ya umeme.
Chanzo- EATV
Share:

TAASISI YA GOVERNANCE LINKS YAKABIDHI MIRADI YA MFANO JIJINI MWANZA


Mkurugenzi wa taasisi ya Maendeleo na Utafiti ya Governance Links Tanzania, Donald Kasongi (wa pili kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu Mradi wa Ustahimilivu katika Jijini la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience) wakati wa zoezi la kukabidhi matenki ya kuvuna maji ya mvua yaliyojengwa kupitia mradi huo katika Shule za Msingi Mabatini A na B zote za Jijini Mwanza, hii leo Disemba 21, 2018.

Mradi wa Ustahimilifu katika Jiji la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience) ulibuniwa na taasisi ya Governance Links Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Mwanza ukilenga kuwajengea uwezo wananchi pamoja na wadau/ taasisi mbalimbali kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi pamoja na hatari ya Majanga ikiwemo mafuriko.
Mkurugenzi wa taasisi ya Maendeleo na Utafiti ya Governance Links Tanzania, Donald Kasongi amesema ujenzi wa matenki ya mfano ya kuvuna maji ya mvua katika Shule za Msingi Mabatini A na B Jijini Mwanza, umegharibu shilingi Milioni tano hivyo wananchi na Shule nyingine zinaweza kutumia mradi huo kujifunza namna bora ya kuvuna maji ya mvua badala ya kupoteza kiasi kikubwa wakati wa mvua.
Utekelezaji wa Mradi wa majaribio wa Ustahimilifu katika Jiji la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience) ulianza mwezi Otoba 2017 na unafikia tamati mwezi huu Disemba 2018 huku kukiwa na matarajio makubwa ya mradi huo kuwa endelevu.
Taasisi ya Maendeleo na Utafiti ya Governance Links Tanzania imekabidhi manteki mawili ya kuvuna maji ya mvua katika Shule za Msingi Mabatini A na B, yaliyojengwa kupitia mradi wa Ustahimilivu katika Jijini la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience). 

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Donald Kasongi amesema ujenzi wa matenki hayo ya mfano umegharimu shilingi Milioni tano hivyo wananchi na Shule nyingine Jijini Mwanza zinaweza kutumia mradi huo kujifunza namna bora ya kuvuna maji ya mvua badala ya kupoteza kiasi kikubwa cha maji wakati wa mvua. 

Kasongi amesema hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Ustahimilifu katika Jiji la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience) unaolenga kuwajengea uwezo wananchi pamoja na wadau/ taasisi mbalimbali kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi pamoja na hatari ya Majanga ikiwemo mafuriko. 

Wakizungumza kwa niaba ya wenzao, wanafunzi Mariam Thomas (Mabatini B), Rayton Mandalu (Mabatini A) pamoja na Rhoda Madaraka (Mabatini B) wamesema uvunaji wa maji ya mvua umewasaidia kupata maji ya kutosha kwa ajili ya usafi wa madarasa, vyoo, kumwagilia miche ya miti na hivyo kuwaondolea adha iliyokuwepo awali.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG 
Share:

PAPA FRANCIS ATANGAZA JIMBO LA MBEYA KUWA JIMBO KUU...AMTEUA NYAISONGA KUWA ASKOFU MKUU


Kabla ya kuundwa kwa Jimbo kuu la Mbeya, Jimbo Katoliki la Iringa lilikuwa ni sehemu ya Jimbo kuu la Songea likiwa na Parokia 38, zinazohudumiwa na Mapadre wa Jimbo 72, Mapadre watawa 38, watawa wa kiume ni 332 na watawa wa kike ni 667. 

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameunda Jimbo kuu Jipya ya Mbeya nchini Tanzania linaloundwa na Jimbo Katoliki la Mbeya, Jimbo Katoliki la Iringa na Jimbo Katoliki la Sumbawanga. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu ametemua Askofu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga kuwa Askofu mkuu wa kwanza wa Jimbo kuu la Mbeya nchini Tanzania.

 Kabla ya uteuzi huu, Askofu Nyaisonga ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC, alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda. Jimbo kuu la Mbeya kwa sasa linaundwa na Parokia 48 zinazohudumiwa na Mapadre wa Jimbo 73, Mapadre watawa 15; lina watawa wa kiume 15 na watawa wa kike ni 299 kadiri ya takwimu za Kanisa kwa Mwaka 2018.

Kabla ya kuundwa kwa Jimbo kuu la Mbeya, Jimbo Katoliki la Iringa lilikuwa ni sehemu ya Jimbo kuu la Songea likiwa na Parokia 38, zinazohudumiwa na Mapadre wa Jimbo 72, Mapadre watawa 38, watawa wa kiume ni 332 na watawa wa kike ni 667. Jimbo Katoliki la Sumbawanga lilikuwa chini ya Jimbo kuu la Tabora likiwa na Parokia 21 zinazohudumiwa na Mapadre wa jimbo 53, Mapadre watawa ni 7; watawa wa kiume ni71 na watawa wa kike ni 348.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga, alizaliwa kunako tarehe 3 Novemba, 1966, Wilayani Bunda, Mkoani Mara. Baada ya masomo yake ya msingi na sekondari, huko Mbeya na Sumbawanga, kunako Mwaka 1989 alijiunga na Seminari kuu ya Kibosho, Moshi, kwa ajili ya masomo ya Falsafa na baadaye akaendelea na masomo ya Kitaalimungu huko Segerea, Jimbo kuu la Dar es Salaam na hatimaye, kuwekewa mikono kama Shemasi, kunako mwaka 1995 baada ya kumaliza mwaka wa kichungaji, alioufanya katika Parokia ya Itaka, Jimbo Katoliki la Mbeya.

Tarehe 11 Julai, 1996 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre, Jimbo Katoliki la Mbeya na Hayati Askofu Yakobo Dominic Sangu. Historia inaonesha kwamba, huyu ndiye aliyekuwa Padre wa mwisho kuwekewa mikono na Hayati Askofu Sangu. Baada ya Upadrisho alifanya utume katika sehemu mbalimbali za Jimbo Katoliki Mbeya, kama Paroko usu huko Itumba na Mwalimu wa Seminari Ndogo ya Mbalizi. Kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2001 alijiendeleza kwa masomo ya juu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, ambako alijipatia shahada ya kwanza. Baada ya masomo yake, alirudi kuendelea na kazi yake kama Mkuu wa shule ya Sekondari ya Pandahill, kuanzia mwaka 2001 hadi mwaka 2006.

Kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2009 alijiendeleza kwa masomo ya juu zaidi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alikojipatia Shahada ya uzamili katika masomo ya Sayansi Jamii. Kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2011 alikuwa ni Mhadhiri Msaidizi katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino cha Tanzania, SAUT, kilichoko Jijini Mwanza. Akiwa SAUT. Kunako Mwezi Agosti, 2010, alitumwa nchini Ujerumani kwa masomo ya juu zaidi, kama sehemu ya maandalizi ya kuwa ni Jaalimu wa Elimu hasa katika somo la Jiografia. Kabla ya kuhitimu masomo yake huko Ujerumani, tarehe 9 Januari 2011 akapokea simu kutoka kwa Balozi wa Vatican nchini Tanzania, ikimtaarifu kwamba, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI amemteua kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Dodoma na hatimaye, kuwekwa wakfu kama Askofu, tarehe 19 Machi 2011. Tarehe 17 Februari 2014, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda na kusimikwa rasmi tarehe 4 Mei 2014.

Askofu mkuu mteule Gervas Nyaisonga wa Jimbo kuu la Mbeya katika mahojiano maalum na Vatican News anasimulia kwamba, wito wake kama Mkatoliki na baadaye kama Padre na sasa kama Askofu na Askofu mkuu ni mchango mkubwa alioupokea kutoka kwa wazazi wake na kwa namna ya pekee Mama yake Mzazi aliyekuwa na nafasi ya pekee katika malezi. Huyu alikuwa kwa hakika ni Mwalimu na katekista wa kwanza katika majiundo yake ya maisha ya kiroho. Hii inatokana na ukweli kwamba, Baba yake Mzazi hakuweza kuwa nyumbani wakati wote kutokana na dhamana na utumishi wake kwa umma. Tangu akiwa mtoto mdogo alitamani na akapenda kutumikia Altareni pamoja na kusoma masomo Kanisani wakati wa Liturujia ya Neno la Mungu. Alipofikia umri wa kujiunga na Seminari ndogo, yeye alikuwa ni kati ya vijana kumi waliochaguliwa kutoka Parokiani mwake, lakini kati yao wawili tu, ndio waliobahatika kufikia Daraja Takatifu la Upadre, yaani Yeye Askofu mkuu mteule na Padre Januari Mwilwa wa Jimbo Katoliki la Mbeya.

Akiwa Seminari ndogo wito na ari ya kujitoa kwa ajili ya kumtumikia Mungu na jirani viliendelea kukua na kukomaa taratibu, akijikita zaidi katika maisha ya: Sala, Masomo, Kazi na Michezo, kama sehemu ya vipaumbele wakati wa malezi Seminarini. Ni mahali alipokuza vipaji vyake kwa ajili yake mwenyewe na Kanisa kwa ujumla. Akaendelea kukua katika kimo na busara sanjari na kukomaa kwa wito wake, akitamani daima kuwa Padre. Alipohitimu masomo ya kidato cha sita, alishawishiwa na walimu wake kwenda Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria, ili baadaye, aweze kujiunga na Chuo Kikuu kwa masomo ya juu zaidi. Mkurugenzi wa miito hakucheza mbali na vijana wake, akamshauri kujiunga na Seminari kuu kwa ajili ya kuendelea na masomo ya kipadre, ushauri huu ukajikita katika moyo wake, akapiga moyo konde na kwenda Seminarini.

Kwa sasa anamwimbia Mungu utenzi wa shukrani kwa matendo makuu aliyomtendea katika hija ya maisha yake kwa kumteuwa kuwa Askofu mkuu wa kwanza wa Jimbo kuu la Mbeya, muda wa mwezi mmoja tu tangu alipofariki dunia Askofu Evaristo Marcus Chengula, hapo tarehe 21 Novemba 2018. Hili ndilo Kanisa Katoliki la Tanzania: maajabu yaliyofanyika hata baada ya kufariki dunia kwa Kardinali Laurian Rugambwa, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, tarehe 8 Desemba 1997; Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa Askofu mkuu mwandamizi Polycarp Pengo kuwa Kardinali na kumsimika rasmi tarehe 22 Februari 1998.

Chanzo - Vatican News
Share:

MAGUFULI ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUSIMAMIA NIDHAMU KWENYE UCHAGUZI 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameliagiza Jeshi la Polisi kuimarisha nidhamu kwenye uchaguzi ujao wa serikali za Mitaa wa mwaka 2019.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Desemba 21, 2018 katika mahafali ya kuhitimisha mafunzo ya Maofisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Polisi, ambapo amesema kuna baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakilituhumu jeshi hilo kwa vitu ambavyo, amedai si vya kweli.

"Mwaka 2019 tunaingia katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, nawaomba Jeshi la Polisi mkasimamie nidhamu," amesema Rais Magufuli.

Ameongeza kuwa, "Watu wasioukuwa na shukrani ndio watawasema vibaya, lakini sisi tunaotambua na kuthamini mchango wenu katika ulinzi wa taifa hili, tunatembea kifua mbele huu ni ukweli usiofichika kuwa Jeshi la Polisi mnafanya kazi nzuri".

Kwa upande wake, Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro amesema Jeshi hilo limejipanga vya kutosha kusimamia usalama katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020, na kusema kuwa hawatatoa nafasi kwa mtu yeyote atakayehatarisha amani ya nchi.


“Tumejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi unakwenda vizuri. Siku zote huwa nasema kama unaamua kuchukua silaha ya AK 47 ambayo haipatikani duka lolote na kuingia nayo barabarani ili uwatishe wananchi, hatuwapi nafasi,” amesema.

Katika mahafali hayo wahitimu 513 wamemaliza kozi ya maofisa polisi na wakaguzi wasaidizi.

IGP Sirro amewataka askari hao kuhakikisha wanazingatia uadilifu katika utendaji wao kwani bila kufanya hivyo taaluma hiyo haitaleta tija kwa Taifa.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema polisi hawatayumbishwa katika kusimamia amani ya nchi huku akionya maandamano yanayolenga uchochezi.

“Hatutayumbishwa, tutaendelea kusimamia amani ya nchi hii kwa mujibu wa sheria. Wale wote wanaotaka kucheza na amani ya nchi hii wakiwamo wale wanaotaka kuandamana, nasema ole wao, narudia tena ole wao,” amesema Masauni.
Share:

VIONGOZI WAMVAA MKUU WA MKOA ANAYEDAIWA KULAZWA MAKABURINI NA WACHAWI WA IRINGA


Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi

Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi kumtaka Katibu wa BAVICHA Kinondoni, Hilda Newton kujisalimishakatika kituo cha polisi Iringa siku ya leo, kwa kusambaza taarifa zenye ujumbe wa kwamba huko Iringa 'Ali Happi amelazwa makaburini, viongozi wamekimkingia kifua kuwa hatajisalimsha.

Hapi amekutana na vikwazo kutoka kwa viongozi mbalimbali baada ya sakata hilo kusambaa kwenye mitandao likimuhusisha, Hilda kuchapisha habari iliyosema,"Watu Iringa nimewanyoshea mikono . Naambiwa mwezi 1 uliopita, Ally Happi alikuwa amelala nyumbani kwake ilipofika alfajiri alijikuta amelala makaburini akiwa amevaa boksa pekee ikabidi akimbilie Dar alafu tangu siku hiyo mpaka leo hajarudi Iringa na kaomba abadlishiwe kituo cha kazi".

Baada ya habari hiyo kusambaa katika mitandao Disemba 17, Hapi alimtaka kiongozi huyo wa Baraza la Vijana Chadema kuripoti kituo cha polisi Iringa Desemba 21.

"Mlio karibu na huyu binti mfupi wa BAVICHA mkumbusheni kesho tarehe 21 saa 2 asb ndio mwisho wa kujisalimisha kwa hiyari kwa RPC Bwire Central Police Iringa" Ally Hapi.

Baada ya kauli hiyo ya Hapi katika ukurasa wake wa Twitter, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche ameandiaka, "Mtume Bwire amtafute hatajisalimisha 'unless' useme sheria gani inakupa mamlaka wewe 'kumsummon'!!!. Tumia madaraka vizuri, bado wewe ni kijana, lakini kwasababu yamekulevya hautaelewa".


Naye Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amemjibu Kiongozi huyo kwamba, "Kwanini unakosa busara?. Unamwita mtu mfupi? Halafu wewe ni Kiongozi?, huna mamlaka ya kumwita Mtu yeyote kuripoti Polisi. Hatakuja na hutafanya kitu. Jifunze hekima za uongozi Ally. Usiwe na kibri kwani kibri si maungwana. Sasa Hilda hatatii amri yako batili. Tuone utafanya nini".

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA, Patrick Ole Sosopi amemjibu Hapi kwamba, "Nafikiri this time utaelewa Job Description (majukumu ya kazi) yako vizuri kwa sababu tunafahamu hujui, semina elekezi za majukumu yenu mlio wengi hajapewa. Wewe utakuwa Mwalimu wa wenzako kupitia hili, Jeuri ya Madaraka uliyonayo na kutumia vyombo vya dola vibaya, Hilda Newton hatokuja tuone".

Kwa upande wa Mbunge wa Iringa, Peter Msigwa amesema, "Hayo ni matumizi mabaya ya madaraka! Uongozi wa kutisha tisha watu umepitwa na wakati, kama umekosewa fuata tatatibu za kisheria , huna madaraka ya kukamata kamata watu ovyo!".

Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA), Zubeda Sakuru naye amemjulisha kiongozi huyo kwamba, "Hatokuja na hutofanya kitu. Mweupe wewe".

Share:

TANZANIA NA UGANDA ZAKUBALIANA KUIMARISHA BIASHARA NA UCHUMI

Mkutano kati ya Tanzania na Uganda kujadili namna ya kuimairisha mahusiano ya kibiashara na kiuchumi ulifanyika Mutukula, Uganda kuanzia tarehe 17 hadi 19 Desemba 2018. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda na Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia Kyabambadde waliongoza ujumbe wa nchi zao katika mkutano huo.

Mkutano huo ulihitimishwa kwa Mawaziri kusaini taarifa ya makubaliano ambayo pamoja na mambo mengine, waliafikiana kuvitafutia ufumbuzi vikwazo vya kibishara na vile visivyo vya kiforodha vinavyozorotesha biashara baina ya nchi hizo mbili.

Mkutano huo ulianza kwa ngazi ya Wataalamu na Makatibu Wakuu ambapo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph R. Buchwaishaija.

Aidha, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt Aziz Ponary Mlima na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Kabonero walishiriki mkutano huo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mutukula, Uganda
Share:

MBOWE,MATIKO SASA RASMI KULA KRISMASI NA MWAKA MPYA 2019 GEREZANI

Kesi Na. 112/2018 ya uchochezi inayowakabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Mbunge wa Tarime mjini, Ester Matiko na viongozi wengine saba wa chama hicho imeahirishwa leo Desemba 21, 2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hadi January 3, 2019.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Simon Wankyo akisaidia na wakili Salim Msemo amedai leo Ijumaa Desemba 21, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Wilbard Mashauri kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Simon amedai kuwa hawana taarifa ya kinachoendelea mahakama ya juu hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo, wakili Faraja Mangula amedai kuwa wakili wa washitakiwa hao Peter Kibatala na Sheck Mfinanga wamepata dharura hivyo wanaomba mahakama ipange Januari 4, 2019.

Akijibu hoja hiyo, wakili Simon amedai wanaiachia mahakama ipange tarehe itakayoona inafaa na hakimu Mashauri kuahirisha kesi hiyo hadi Januari 3, 2019.

Mbowe na Matiko wako gereza la Segerea baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana Novemba 23, 2018 kwa kukiuka masharti ya dhamana ikiwemo kutoka nje ya nchi bila kibali.
Share:

Breaking : Pakua Upya App ya Malunde 1 blog ...Imeboreshwa Kukupa Raha zaidi ...Bonyeza HAPA SASA

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog

NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Kama bado una app yetu ya zamani kuanzia sasa haitakuletea habari tena...Hii ni taarifa ya mwisho kuonekana kwenye Simu yako... Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Share:

NDEGE MPYA AIRBUS A220-300 KUTUA TANZANIA JUMAPILI HII

Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas amesema Serikali itapokea ndege yake nyingine mpya toleo la Airbus A220-300 Jumapili Desemba 23, 2018.

Abbas ameeleza hayo leo Ijumaa Desemba 21, 2018 katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.

“Ungana nasi kuipokea ndege ya kwanza kununuliwa na Serikali kwa toleo la Airbus A220-300. Ni Tanzania pekee.’Ngorongoro-Hapa kazi Tu’, itawasili nchini Jumapili hii na siku chache baadaye ndege nyingine kama hiyo itawasili Dodoma-Hapa Kazi Tu,” ameandika Dk Abbas.


Share:

RAIS MAGUFULI ATOA MILIONI 700 KUBORESHA CHUO CHA TAALUMA YA POLISI

Rais John Magufuli ameahidi kutoa Sh700milioni kwa ajili ya kuboresha chuo cha taaluma ya Polisi kilichopo jijini Dar es Salaam kutokana na kukabiliwa na changamoto ya miundombinu ikiwamo uhaba wa majengo.

Akizungumza leo Ijumaa Desemba 21, 2018 katika sherehe za kufunga mafunzo ya maofisa wa polisi na wakaguzi wasaidizi wa jeshi hilo zilizofanyika viwanja vya chuo hicho, Rais Magufuli amesema atatoa fedha hizo ili kulinda heshima ya chuo hicho.

Amesema fedha hizo zitatolewa kabla ya Ijumaa wiki ijayo huku akisisitiza matumizi sahihi ya fedha hizo.

Awali Mkuu wa Chuo hicho, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Anthony Rutta akitoa taarifa ya mafunzo hayo alitaja changamoto ya uhaba wa miundombinu ikiwamo madarasa na mabweni na kuomba kiasi cha Sh700milioni.

“Nimekusikia umeomba Sh700milioni nitakuletea ili parekebishwe na kupendeza. Pamoja na kuwa sisi (Serikali) tunahamia Dodoma lakini hapa ni lazima papendeze,” amesema Magufuli.

Rais Magufuli ameagiza kuhakikisha fedha hizo zinatumika kama zilivyopangwa na kusisitiza kuwa atafuatilia.

“Pale Jeshi la Magereza nilitoa fedha kwaajili ya kujenga nyumba za askari halafu hazikujengwa, sasa wakati mwingine unapata shida unatoa nyumba kwa ajili ya maaskari halafu hakuna nyumba, nimemuagiza kamishna wa magereza afuatilie hizo hela zimepotelea wapi,” amesema.
Share:

AHUKUMIWA JELA MIAKA 20 KWA KUHUJUMU UCHUMI WA NCHI

Na,Naomi Milton Serengeti Machaba Nyantito(30) mkazi wa kijiji cha Robanda wilayani hapa amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia katika mahakama ya wilaya ya Serengeti Mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile mwendesha mashtaka wa Jamhuri Emmanuel Zumba kabla ya kutolewa kwa hukumu alimkumbusha mshtakiwa makosa yake katika kesi ya uhujumu uchumi namba 94/2017 Zumba alisema mshtakiwa huyo anashtakiwa kwa makosa matatu kosa la kwanza ni kuingia ndani ya Hifadhi bila kuwa na kibali kinyume na kifungu namba 21(1)(a)(2) na kifungu namba 29(1) cha…

Source

Share:

Breaking : Pakua Upya App ya Malunde 1 blog ...Imeboreshwa Kukupa Raha zaidi ...Bonyeza HAPA SASA

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownloap App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog

Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog 

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog


NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Kama bado una app yetu ya zamani kuanzia sasa haitakuletea habari tena...Hii ni taarifa ya mwisho kuonekana kwenye Simu yako... Tafadhali fuata maelekezo hapo juu...Pakua app yetu Mpya

Share:

VIJANA ILALA WATAKIWA KUJITAMBUA,WATENGEWA MAMILIONI YA FEDHA

Vijana katika halmashauri ya manispaa ya Ilala watakiwa kujitambua na kuchangamkia fursa zilizopo kwenye manispaa hiyo na kukopa pesa za kujiendeleza ili kuweza kujikwamua kiuchumi kuelekea Tanzania ya viwanda. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko (katikati kulia aliyevaa miwani) akikagua baadhi ya bidhaa za zinazotengenezwa na vijana wakati wa uzinduzi wa kongamano la Jukwaa la Vijana Ilala. Hayo yamesemwa wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Vijana Manispaa ya Ilala na mstahiki meya wa manispaa hiyo Charles Kuyeko ambapo amewataka vijana kujitambua na kuweza kutumia fursa adimu zitolewazo na…

Source

Share:

MSANII AFANDE SELE AWASHUKIA BASATA

NA KAROLI VINSENT WAKATI Wasanii Diamond Platnumz na Msanii Rayvanny wakiomba msamaha kwa serikali kwa hatua ya kwa makosa waliofanya na kupelekea kufungiwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) . Hatimaye Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop hapa nchini, Afande Sele,ameibuka na kulishukia Baraza la Basata kwa hatua yake ya kuwafungiwa wasanii hao kutotumbuiza ndani na nje ya nchi. Mkali huyo wa miondoka ya Kufoka Fuko ameanza kwa kushangazwa kwa nini BASATA wawafungie wasanii hao kutofanya show nje ya nchi ile hali wamefanya kosa hilo ndani ya nchi? “Haijawahi kutokea….unacheza…

Source

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger