Thursday, 20 December 2018

HABARI KWENYE MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DESEMBER 20/2018

Katibu leo December 20, 2018,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania.  

Source

Share:

Wednesday, 19 December 2018

WANAOBEZA MIMI KUWASAIDIA WALEMAVU KUPATA VIUNGO BANDIA NI MTAZAMO WAO -MBUNGE MHE RITTA KABATI.

  Na Francis Godwin,Iringa MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) amesema kuwa mkakati wa ni kuhakikisha anawasaidia watu wenye ulemavu wa viungo katika mkoa huo kupata msaada wa bure wa viungo vya bandia na wanaosema anafanya siasa kupitia walemavu hao ni mtazamo wake na si makusudi yake kuwabangua wenye ulemavu. Akizungumza Jana wakati wa zoezi la kuwasafirisha zaidi ya walemavu 25 kwenda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwawekea miguu bandia ,Kabati alisema kuna mwanasiasa amekuwa aitumia majukwaa ya siasa kubeza kazi hiyo anayoifanya kwa…

Source

Share:

WAFANYABIASHARA WADOGO 25,000 MKOANI MWANZA KUPATIWA VITAMBULISHO.

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndugu John Mongella, hivi Leo amekabidhi Vitambulisho 25,000 vya wafanyabiashara wadogo maarufu wamachinga kwa wilaya saba za mkoa wa Mwanza. Ndg. Mongellea, akikabidhi vitambulisho hivyo, amesema zoezi hili ni endelevu litakalowafikia wafanyabiashara wadogo wote mkoani Mwanza. Kwa kuanzia wilaya ya Nyamagana na Ilemela watafikiwa wafanyabiashara 10,000 kutokana na wingi ya idadi na kadi 15,000 zitagawanywa katika wilaya tano zilizobakia za mkoa wa Mwanza. Ndg. Mongella amekemea dhamira mbaya ya wafanyabiashara wakubwa wasiowaaminifu wanaotaka kuhujumu zoezi hili kwa kufadhiri wachuuzi wadogo wadogo ili wapate vitambulisho…

Source

Share:

RC AAGIZA WANAFUNZI WOTE WALIOFAULI KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA JANUARY MWAKANI.

  Na Allawi Kaboyo Bukoba. Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti awaongoza Wadau wa Elimu Mkoani Kagera kuweka mikakati ya muda mfupi na mda mrefu ili kuhakikisha wanafunzi 14,046 kati ya wanafunzi 39,545 waliofaulu Mtihani wa Darasa la Saba mwaka 2018 na kukosa Vyumba vya Madarasa wanaanza masomo yao kama wenzao 25,499 ifikapo Januari 7, 2019. Mikakati hiyo iliwekwa katika kikao cha Wadau wa Elimu wa Mkoa wa Kagera kilichofanyika Mkoani hapa Desemba 18, 2018 katika ukumbi wa Halmashauri Wilaya ya Bukoba na kuongozwa na Mhe.…

Source

Share:

MAKOMBORA YA MBUNGE MNYIKA MBELE YA JPM YAMVURUGA MAKONDA

NA KAROLI VINSENT NI wazi kuwa Kauli aliyoitoa  mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika kuhusu demokrasia, bomoabomoa na vyuma kukaza imemvuruga  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ndivyo unaweza ukasema Baada ya Mnyika ndipo ikamfanya Makonda  kuanza kueleza masuala mbalimbali yaliyofanywa na Rais John Magufuli tangu aingie madarakani. Wa Kwanza kuanza kuibua majadala huo ni Mbunge Mnyika ambapo alipopewa nafasi ya kusalimia wananchi,alitumia nafasi hiyo kulalamikia kukosekana kwa Demokrasia ,Kukosekana kwa Utu kwenye Bomoa Bomoa pamoja na Hali mbaya ya Uchumi waliokuwa nayo watanzania kwa sasa (Vyuma…

Source

Share:

POLISI WATOA AMRI YA KUKAMATWA KWA MKE WA RAISI MSTAAFU NI BAADA YA KUMPIGA MWANAMITINDO


Polisi nchini Afrika Kusini imetoa amri ya kukamatwa kwa Grace Mugabe, mke wa aliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye anatuhumiwa kumshambulia na kumjeruhi mwanamitindo wa Afrika Kusini, Gabriella Engels, mwaka 2017.

Mwanasheria anayefanya kazi na shirika la kutetea haki za binadamu la AfriForum la huko Afrika Kusini, Garrie Nel amesema amethibitishiwa na Polisi kuhusu kutolewa kwa amri hiyo, na kuongeza kuwa ikiwa Bi. Mugabe atakanyaga kwenye ardhi ya Afrika Kusini atakamatwa.

Mwanasheria huyo vile vile ametaka mchakato wa kumtia mbaroni Grace Mugabe na kumsafirisha hadi Afrika Kusini uanze sasa.

Grace Mugabe anatuhumiwa kumpiga na kumjeruhi mwanamitindo Gabriella Engels kwenye hotel moja mjini Johannesburg Agosti mwaka 2017, lakini hakushtakiwa kwa sababu alikuwa na kinga ya kidiplomasia.
chanzo:Eatv
Share:

TAASISI YA MOYO YA JAKAYA YAFANYA UPASUAJI KWA ZAIDI YA WATOTO 1000

TAASISI ya moyo ya Jakaya Kikwete imefanikisha kufanya upasuaji kwa zaidi ya watoto 1000 ikiwa ni upasuaji mkubwa kwa watoto 600 na upasuaji mdogo kwa zaidi ya watoto 400. Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mbio za Heart Marathon kwa mwaka 2019 Rais wa Tanzania Health Summit (THL) Dkt. Omary Chillo amesema kuwa mbio hizo zitafika kilele Aprili 28, 2019 katika viwanja vya Coco Beach ikiwa ni mara ya nne tangu kuanzishwa kwake na kusema kuwa malengo ya kuendesha mbio hizo ni kusaidia juhudi za serikali za kupunguza magonjwa…

Source

Share:

YANGA KUWAKOSA VIUNGO WAKE MACHACHARI KESHO, MCHEZO KATI YAO NA AFRICAN LYON

Klabu ya soka ya Yanga inatarajia kuwakosa viungo wake muhimu, Papy Tshishimbi na Feisal Salum 'Fei toto' katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya African Lyon utakaopigwa kesho.

Fei toto ataukosa mchezo wa kesho katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kutokana na kupewa kadi tatu za njano ambapo hivi sasa atasubiri mchezo unaofuata.

Ukiachana na Fei toto, pia inaelezwa kuwa kiungo fundi kutoka nchini Congo, papy Kabamba Tshishimbi amerejea kwao baada ya kupatwa na msiba wa baba mkwe wake hivi karibuni.

Kukosekana kwa viungo hao wawili kunafanya idadi ya wachezaji watakaokosekana katika mchezo huo kufikia wanne baada ya Andrew Vicent na Raphael Daudi kuwa majeruhi.

Yanga itavaana na African Lyon ambayo imeamua kutumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid kama uwanja wake wa nyumbani mpaka mwisho wa msimu huu. Mpaka sasa ina pointi 44 baada ya kucheza michezo 16 huku ikiwa inaongoza ligi.
Share:

Ripoti:ITACHUKUA MIAKA 200 KWA WANAWAKE KUPATA MALIPO SAWA NA WANAUME


Jarida la uchumi duniani limetoa taarifa kuwa itachukua miaka 200 kufikia usawa wa malipo kati ya mwanamke na mwanaume

Ripoti ya mwaka 2018 toleo la uwiano wa kijinsia ulimwenguni, lililoandaliwa na Jukwaa la uchumi duniani (WRF) na kutolewa tarehe 17 mwezi Desemba limeweka picha halisi ya hali ya haki za wanawake katika siasa, uchumi na elimu.

Wakati ripoti hiyo imeandika kuwa nchi 88 kati ya 149 zilizo fanyiwa utafiti zimeonyesha kuongeza juhudi katika kushughulikia maswala ya usawa wa malipo na uwakilishi wa kisiasa lakini picha halisi ya matokeo kwa ujumla bado ni changamoto. Ina kadiriwa kuwa kufikia usawa wa kijinsia ulimwenguni itachukua miaka 100.

Hata hivyo hiyo ni taarifa njema ukifananisha na na hali ilivyo katika baadhi ya maeneo kama inavyo onekana hapa chini.

1. Miongo miwili mpaka kufikia usawa wa malipo

Kukosekana kwa usawa katika ushirikiano wa kiuchumi na fursa duniani kote inaweza kuwa jambo la wazi kabisa, lakini kutokuwa na usawa wa kijinsia katika maswala ya kisiasa ni tatizo kubwa zaidi.

Japokuwa pengo la kisiasa linaondoka haraka zaidi.

Ripoti ya hivi karibuni ya shirika la kazi la kimataifa (ILO) inasema utofauti wa kipato ulimwenguni kati ya mwanamke na mwanaume unakaribia asilimia 20.


Shririka la WEF pia lilifafanua kuwa wanawake wataendelea kufanya shughuli zisizo na malipo.

"Kati ya nchi 29 ambazo takwimu zake zipo, wanawake wanatumia mara mbili zaidi ya muda wao katika kazi za nyumbani na shughuli nyingine zisizo na malipo tofauti na wanaume," ripoti hiyo imeelezaa.

Pia watafiti wamegundua asilimia 60 ya nchi zilizofanyiwa tafiti wanawake wana fursa sawa ya kupata huduma za kifedha kama wanaume, huku umiliki wa ardhi ukiwa asilimia 42.Zaidi ya asilimia 60 ya wabunge Rwanda ni wanawake lakini kiujumla wanawake wabunge duniani ni asilimia 24 tu.

2. Fursa katika ofisi za umma.

Kwa sasa wanawake ambao ni wakuu wa nchi wapo katika nchi 17 kati ya 149 zilizo fanyiwa uchambuzi katika ripoti ya kijinsia ulimwenguni, ni zaidi ya asilimia 11.

"Kwa miaka 50 iliyopita, wastani wa wanawake ambao ni wakuu wa nchi au mawaziri wakuu katika nchi hizo 149 walikaa madarakani kwa wastani wa miaka miwili," taarifa imefafanua.

Hali ni ya ahueni katika nafasi za uwaziri, kukiwa na asilimia 18 ya mawaziri wanawake duniani.

Katika bunge kuna asilimia 24 tu ya wanawake.

Moja ya nchi ambazo zimefanya vizuri ni Rwanda ambapo ulimwengu mzima ndio nchi yenye usawa mkubwa kabisa wa wanawake bungeni kwa asilimia 61.3Pengo la usawa wa kijinsia katika elimu litazibwa katika kipindi cha miaka 14 kwa mujibu wa WEF

3. Vikwazo vya elimu bado vikubwa katika baadhi ya nchi

Kwa mujibu wa WEF, nchi 44 zimeonyesha kuwa na wanawake wasiojua kusoma na kuandika ni asilimia 20.

Nchi ambayo imefanya vibaya zaidi ni Chad, ambapo kuna asilimia 13 pekee ya wanawake wanaojua kusoma na kuandika.

Japo kuwa ukosefu wa usawa wa kijinia katika elimu ulimwenguni unaweza kuondolewa ndani ya miaka 14, haraka zaidi ya ilivyo tazamiwa awali.

Lakini bado kuna wasiwasi katika takwimu za jumla za wanafunzi wanao jiunga shule: Wasichana asilimia 65 na wavulana asilimia 66 wamejiunga elimu ya sekondari ulimwenguni.a

4. Usawa wa kiafya

Ripoti hiyo inaeleza kuwa usawa wa kijinsia katika afya ulimwenguni unakaribia kutimia.

Kipengele hicho kimeangazia muda wa kuishi na upatikanaji wa huduma za afya.

Katika nchi zote zilizo chunguzwa, ninchi tatu pekee Kuwait, Bhutan na Bahran wanawake wanaishi muda mrefu zaidi kama wanaume.Iceland kwa mara nyingine ndio nchi yenye usawa wa kijinsia zaidi ya nchi zote duniani

5. Pesa pekee haimalizi utofauti wa kijinsia

Wakati nchi nne zilizo endelea - Iceland, Norway, Sweden and Finland - zikiongoza kipengele cha utofauti katika jinsia, listi hiyo haija ongozwa na nchi tajiri kama unavyofikiria.

Nicaragua (5), Rwanda (6), Philippines (8), na Namibia (10) ndio nchi zinazo endelea katika 10 bora na nchi hizi zinazo endelea ndio zimefikisha karibu nusu ya 30 bora.

Nchi yenye uchumi mkubwa zaidi duniani - Amerika - ipo nafasi ya 51, wakati Italia ipo nafasi ya 70.

Nchi nyingine ambazo hazikutegemewa kushika nafasi ya chini ni Russia (75th), Brazil (95), China (103) na Japan (110)

Chanzo:Bbc
Share:

MBUNGE MNYIKA NA RAIS MAGUFULI WATOFAUTIANA MCHANA KWEUPE KUHUSU BOMOABOMOA

Na Bakari Chijumba, Mtwara. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John  Magufuli amesema waliobomolewa nyumba kupisha upanuzi wa barabara, eneo la Kimara hadi Mbezi jijini Dar es Salaam hawatalipwa fidia kwa kuwa walijenga katika eneo la hifadhi ya barabara. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo Jumatano Desemba 19, 2018 katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la upanuzi wa barabara hiyo kuifanya iwe njia nane, eneo la Kimara Stop Over, ambapo amesisitiza hakuna fidia na hata wanaodai wakienda mahakamani hakuna fidia.. “Niwambie tu wananchi kuwa ukisogelea barabara madhara…

Source

Share:

FORBES YATOA LIST YA MASTAA MATAJIRI DUNIANI ,KYLIE JENNER AFIKIA UTAJIRI WA JAY Z


Fahamu kuwa jarida la Forbes 2018 limetaja list ya watu maarufu wenye utajiri mkubwa nchini Marekani huku list hiyo ikiongozwa na mwongozaji wa Filamu George Lucasmwenye utajiri wa Dola Billions 5.4 za Kimarekani sawa na zaidi ya Trillion 12 za Kitanzania.

Huku mwanadada Kylie Jenner’21 akitajwa kufikia utajiri wa rapper Jay Z wakifungana kwa kuwa na utajiri wa kiasi cha dola Milioni 900 sawa na zaidi ya shillingi Trillion 2 za Kitanzania wote wakiwa wameshikilia nafasi ya 5.

Unaambiwa kuwa utajiri wa Kylie Jenner umetokana na malipo ya kipindi cha Televisheni (Keeping Up With The Kardashians) pamoja na bidhaa zake za urembo (Kylie Cosmetics Line).

Hii ndio list kamili ya watu maarufu wenye utajiri mwaka 2018.

1. George Lucas

Net worth: $5.4 billion

2. Steven Spielberg

$3.7 billion

3. Oprah Winfrey

$2.8 billion

4. Michael Jordan

$1.7 billion

5. (tie) Kylie Jenner

$900 million

5. (tie) Jay-Z

$900 million

7. David Copperfield

$875 million

8. Diddy

$825 million

9. (tie) Tiger Woods

$800 million

9. (tie) James Patterson

$800 million
Share:

KIUMBE WA AJABU APEWA JINA LA DONALD TRUMP... TABIA ZAO ZINAFANANA

EnviroBuild, kampuni iliyopata haki ya kumpa kiumbe huyo jina, iliongeza nywele bandia kwenye kiumbe huyo jambo lililomfanya kuwa na muonekano unaokaribiana na wa Trump.

Kiumbe anayeweza kuishi baharini na katika nchi kavu amepewa jina la Rais wa Marekani Donald Trump, ingawa huenda kiongozi huyo asitake kuhusishwa na kiumbe huyo kutokana na sifa zake.

Amfibia huyo huwa anafukia na kuficha kichwa chake mchangani anapokabiliwa na hatari, jambo ambalo pengine limewashawishi wahusika kumpa kiumbe huyo jina la Trump kutokana na kiongozi huyo kukana kwamba shughuli za viwanda na za kibinadamu zinachangia mabadiliko ya tabia nchi.

Kiumbe huyo pia ni kipofu, hawezi kuona.

Mnyama huyo ambaye amepewa jina Dermophis donaldtrumpi, aligunduliwa katika eneo la Panama, na alipewa jina hilo na mkuu wa kampuni ya EnviroBuild ambaye alikuwa amelipa $25,000 (£19,800) kwenye mnada kupata fursa ya kumpa jina kiumbe huyo.

Kampuni hiyo imesema inataka kuhamasisha watu kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.

"[Dermophis donaldtrumpi] huathiriwa sana na mabadiliko ya tabia nchi na kwa hivyo ni kiumbe aliye katika hatari ya moja kwa moja ya kuangamia kutokana na sera ya somo wake kuhusu mazingira," mwanzilishi mwenza wa EnviroBuild, Aidan Bell, amesema kupitia taarifa.
Kiumbe huyo mdogo ni wa aina ya caecilian, ambao ni viumbe watelezi wanaofanana na minyoo au nyoka, na huishi sana chini ya ardhi.

Bw Bell amesema tabia za kiumbe huyo zinashabihiana sana na za Trump.

"Kupuuza mambo (sawa na kuficha kichwa mchangani) humsaidia Donald Trump kukwepa maafikiano kuhusu madhara ya mabadiliko ya tabia nchi," amesema.Pesa zilizopatikana kutokana na kupiga mnada nafasi ya kumpa kiumbe huyo jina zitakabidhiwa shirika la Rainforest Trust

Wanasayansi duniani wanakubaliana kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanasababishwa na shughuli za kibinadamu.

Lakini Bw Trump, ambaye utawala wake umekuwa ukiendeleza matumizi ya mafuta yanayotokana na kaboni, amewatuhumu wanasayansi hao kwa kuwa na "ajenda ya kisiasa" na kutilia shaka kwamba binadamu wanahusika katika ongezeko la joto duniani.

Chanzo - BBC
Share:

MNYIKA AMPONGEZA RAIS MAGUFULI, AMUOMBA AFANYE UBINADAMU... MWENYEWE AGOMA

Mbunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), John Mnyika amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa kuweza kuamua kujenga barabara ya njia nane.

Amesema kuwa Watanzania wamemuombea asiwe na kiburi, huku akisema Wananchi wana malalamiko juu ya Bomoabomoa ambapo amemuomba kutanguliza utu, wa Mwl. Nyerere mbele.

Aidha, Mnyika ameongeza kuwa maendeleo ni ya vitu lakini maendeleo zaidi ni ya watu huku akimtaka atafakari kuwalipia fidia Wananchi waliopisha ujenzi huu.

“Kuna hili suala la bomoabomoa tunaomba ubinadamu utumike kwa kuwalipa fidia wananchi ili kuondoa malalamiko yaliyopo,” amesema.

Mbali na suala hilo la bomoabomoa, Mnyika pia amemuomba Rais Magufuli kuondoa vikwazo vinavyoikabili demokrasia nchini.

”Demokrasia na Maendeleo ni mapacha, tunakuomba Rais unapofanya kazi za Miradi ya Maendeleo vilevile ukatumia fursa hii kuzungumzia kuondoa vikwazo vinavyoikabili Demokrasia ya Nchi ambayo tunaamini vitasaidia Nchi kusonga mbele,”amesema Mnyika.

Pia ameongeza kuwa kuna mambo matano yanatoka kwa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambayo anawaomba Watanzania na Rais kwa ujumla kuweza kuyatafakari kwa muda huu tunapoelekea mwaka 2019.

Mnyika amesema kuwa akisikia Wafanyakazi wa Umma wanalilia kikokotoo, wengine wamepandishwa madaraja hawajapandishwa mishahara, Wafanyabiashara wanalia Mtaani, na kumuomba akipata nafasi ya kuzungumza pamoja na uzinduzi utatoa matumaini ya Taifa kwa 2019 na 2020″.


Hata hivyo,Rais John Magufuli amemgomea John Mnyika, Mbunge wa Kibamba na Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo kuhusu ombi lao la kuitaka serikali kuwalipa fidia wakazi wa Kimara na Mbezi waliobomolewa nyumba ili kupisha mradi wa barabara ya njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha. 

 Rais Magufuli amesisitiza kwamba serikali haitalipa fidia kwa watu waliobomolewa nyumba zao kupisha upanuzi wa barabara hiyo, kwa kuwa walijenga ndani ya hifadhi ya barabara.
Share:

MKUU WA MKOA WA IRINGA ADAIWA KULAZWA MAKABURINI NA WACHAWI... MWENYEWE ATAKA ALIYEZUSHA AJISALIMISHE POLISI

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Salum Hapi ameonesha kushangazwa na madai ya kujikuta amelala kwenye makaburi mkoani Iringa, kitendo ambacho kinahusishwa na imani za kishirikina.

Kupitia mtandao wake wa Twitter Hapi ameandika ujumbe ulioashiria kuwa analichukulia tukio hilo ni la mzaha ambapo aliambatananisha na picha yenye maneno yanayodai kufanyiwa kitendo hicho.

Aidha katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameamuru mtumiaji huyo wa mitandao ya Kijamii, Hilda Newton kwenda kujisalimisha kwa Mkuu wa Polisi Iringa kwa ajili ya kutoa maelezo kabla ya disemba 21 mwaka huu,

”Aliyetunga na kusambaza uzushi huu akajisalimishe yeye Mwenyewe kwa RPC Bwire Iringa kabla ya tar 21.12.2018 saa 2:00 asb. Nasikia ni Katibu wa BAVICHA,”ameandika RC Hapi katika ukurasa wake wa Twitter

Kupitia ukurasa wa twitter wa mtu ambaye alisomeka kwa jina la Hilda Newton, aliandika,”Naambiwa mwezi mmoja uliopita, alikuwa amelala nyumbani kwake ilipofika alfajiri alijikuta amelala makaburini,”

Share:

WAKAZI WA MANISPAA NA MIJI KUNUFAIKA NA UMEME WA REA

  Na Mwandishi wetu Ruvuma. Shirika la umeme nchini Tanesco mkoani Ruvuma kupitia wakala wa kusambaza umeme vijijini Rea limeendelea kusambaza umeme katika vijiji mbalimbali vilivyopo kwenye mpango ndani ya mkoa wa Ruvuma na kuwafanya wananchi mkoani humo kunufaika na matunda ya serikali ya awamu ya tano. Akitoa salamu za shukrani kwa uongozi wa Tanesco mkoa wa Ruvuma kutokana na kasi waliyonayo ya kuhakikisha wananchi mkoani humo wanapata nishati hiyo, Mhe Subira Mgalu, Naibu Waziri Nishati amemtaka mkandarasi wa kampuni ya Namis kufanya kazi kwa kasi na umakini ili kuondoa…

Source

Share:

SALUM MWALIMU : NIMEKAMATWA,NIMEPIGWA NA KUDHALILISHWA


Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Zanzibar), Salum Mwalimu.

Baada ya Polisi mjini Mafinga mkoani Iringa Jumapili ya Disemba 16, kumkamata na baadaye kumwachia, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Zanzibar), Salum Mwalimu, mwenyewe amefunguka kuwa kilichofanyika ni uonevu dhidi ya demokrasia.

Akizungumza na www.eatv.tv, Mwalimu amesema kuwa kinachodaiwa na aliyetoa agizo la kukamatwa kwake kuhusiana na kutokuwa na kibali cha kufanya mkutano wa ndani hakikuwa sahihi kwa mujibu wa sheria.

Mwalimu amesema kitendo alichofanyiwa kilikuwa cha udhalilishaji na uonevu kwani, hakuwa na kosa lolote ambalo alitenda na kuongeza kuwa hata mikutano ya hadhara ya kisiasa huwa hakuna kibali bali taarifa.

"Sisi sio wajinga kuwa tunavunja sheria makusudi, kama sheria hiyo ipo tungeifuata kama tunavyofanya kwingine, nimekamatwa, nimepigwa na kudhalilishwa bila sababu za msingi", amesema Mwalimu.

Salum Mwalimu alikamatwa wakati akijiandaa kushiriki kikao cha ndani cha chama hicho, na baadaye kuachiwa bila masharti yoyote kutoka kwa Jeshi la Polisi.

Chanzo- EATV
Share:

RAISI ASEMA WALIOBOMOLEWA NYUMBA ZAO HAKUNA FIDIA

Rais John Magufuli amesema waliobomolewa nyumba kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro eneo la Kimara hadi Mbezi jijini Dar es Salaam hawatalipwa fidia kwa kuwa walijenga katika eneo la hifadhi ya barabara.

Rais Magufuli ametoa ufafanuzi huo leo Jumatano Desemba 19, 2018 katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la upanuzi wa barabara hiyo inayofanyika eneo la Kimara Stop Over.

Huku akirejea mara tatu kusema "hakuna fidia", Magufuli amesema hata wakienda mahakamani hakuna fidia.

“Niwambie tu wananchi kuwa ukisogelea barabara madhara yake ni umasikini, hata mimi sijafurahishwa na hii bomoabomoa kwa kuwa wapo ndugu zangu nyumba zao zimebomolewa,” amesema.

"Ni vyema kuwaambia ukweli kesi hii hata wakienda wapi hawawezi kushinda."
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger