Sunday, 20 November 2016

BARABARA YA NJOMBE-MAKETE-MBEYA KUWEKWA LAMI


1
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akifafanua jambo kwa wananchi wa kijiji cha Mang’oto Wilayani Makete ambapo aliwataka walioko kwenye hifadhi ya barabara wabomoe nyumba zao na kutafuta nyumba mbadala ili kuwezesha zoezi la ujenzi wa barabara kuanza na zoezi la fidia lifuate baadaye.
2
Mbunge wa Makete Profesa, Norman Sigala akifafanua jambo kwa wananchi wa Jimbo hilo kuhusu umuhimu wa kutafuta nyumba mbadala ili kupisha ujenzi wa barabara ya Njombe –Makete KM 109 utakaoanza hivi karibuni.
3
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi (kulia), akimshukuru Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani kufuatia hatua ya ujenzi wa daraja la Ruhuhu linalounganisha mkoa wa Njombe na Ruvuma.
4
Wanananchi wa kijiji cha Mang’oto Wilayani Makete wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Hayupo pichani).
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amewataka wananchi waliowekewa alama za kubomoa nyumba zao zilizopo pembezoni mwa barabara ya Njombe-Makete hadi Mbeya KM 205 waanze kuhama kwenye nyumba hizo ili  kupisha zoezi la ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Akizungumza mara baada ya kukagua barabara hiyo Eng. Ngonyani amesema awamu ya kwanza ya ujenzi wake itaanza wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya kupatikana mkandarasi na mkandarasi mshauri ambayo itahusisha sehemu ya Njombe hadi Makete KM 109.4.
“Kuweni waadilifu waliowekewa alama za kijani kwenye nyumba zao watalipwa fidia lakini wenye alama nyekundu hawatalipwa hivyo ni vizuri wote kutafuta maeneo mengine ya makazi ili kuepuka usumbufu mara zoezi la ujenzi litakapoanza”. Amesema Eng. Ngonyani.
Eng. Ngonyani amesema kwa kuwa kazi ya ujenzi na ulipaji fidia zinagharamiwa na Serikali ni vema zoezi la ujenzi wa barabara likaanza wakati Serikali ikitafuta fedha kwa ajili ya fidia.
“Ili tuweze kufanikiwa katika mambo yote tumeona tuanze na zoezi lenye gharama kubwa ambalo ni ujenzi wa barabara kisha zoezi la fidia litaendelea wakati ujenzi wa barabara unaendelea”. amesisitiza Eng. Ngonyani.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi ameishukuru Serikali kwa jitihada za ujenzi wa daraja la Ruhuhu linalounganisha Mkoa wa Njombe na Ruvuma na ameiomba Serikali kuangalia namna ya kuweka lami barabara inayokwenda kwenye hospitali ya Mkoa wa Njombe na ile inayoenda hospitali ya misheni ya Ikonda wilayani Makete ili kuwezesha barabara hizo kupitika kwa urahisi wakati wote wa mwaka.
Katika hatua nyingine Mbunge wa Makete Profesa, Norman Sigara amemuomba  Naibu Waziri Eng. Ngonyani  kuhakikisha Mkandarasi anayejenga barabara ya Njombe –Makete na Makete –Mbeya kupitia Kitulo anaanza kazi iyo kwa wakati ili kuongeza kasi ya wananchi kubomoa nyumba zao katika maeneo ya hifadhi ya barabara na hivyo kuunganisha kirahisi mkoa wa Njombe na Mbeya kwa barabara ya lami.
Naibu Waziri Ngonyani yupo katika ziara ya kukagua Miundombinu ya Barabara, Bandari na Mawasiliano katika mikoa ya Nyanda za juu Kusini ambapo tayari amekamilisha ziara yake katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Ruvuma.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Share:

MAJALIWA :SERIKALI IMEONDOA URASIMU WAWEKEZAJI WATOE HOFU


reli
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini TRL, Masanja Kadogosa (kulia) kuhusu ujenzi  wa reli  inayounganisha  reli ya kati na  kiwanda cha Kiluwa Still Group cha Mlandizi Pwani Novemba 19, 2016  . Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.(Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali imefanikiwa kuondoa urasimu katika baadhi ya halmashauri nchini na idara husika katika kutoa hati miliki kwenye maeneo ya uwekezaji ili kukuza sekta ya uwekezaji.
Aidha Majaliwa amefarijika kukuta njia ya reli yenye urefu wa km 4.3 kutoka reli ya kati kuelekea kiwanda cha kutengeneza nondo cha kilua kilichopo Kibaha Vijijini mkoani Pwani imekamilika kwa asilimia 100.
Sambamba na hayo amezisihi halmashauri nchini kutoa Ushirikiano kwa wawekezaji ili kuongeza ari ya kushawishika kuongeza viwanda.
Majaliwa aliyasema hayo katika ziara yake ya kutembelea maendeleo ya kiwanda cha Kilua cha Mlandizi na kiwanda cha kuunganisha magari na zimamoto cha Equator suma jkt Ruvu.
Alisema ameridhishwa na hatua zinazoendelea katika kukamilisha ujenzi wa viwanda hivyo.
Majaliwa alitoa wiki mbili kwa mkandarasi wa umeme katika kiwanda cha kilua kuhakikisha anakamilisha kufikisha umeme wa uhakika kiwandani humo.
Alieleza kuwa viwanda hivyo vimefikia kwenye hatua nzuri kwani vimekamilika kwa asilimia 80 na vyote vinatarajiwa kuanza kazi mapema mwaka 2017.
Hata hivyo alisema licha ya serikali kuondoa urasimu ulipokuwa ukilalamikiwa sasa halmashauri ziendelee kutenga maeneo, kupima maeneo ili kufungua milango ya uwekezaji.
Majaliwa alisema serikali imedhamiria kujenga viwanda na kufufua ambavyo vilikufa .
Aliiupongeza uongozi wa mkoa wa Pwani kwa kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya rais John Magufuli kujenga viwanda na kuvuta wawekezaji.
“Kiwanda hicho ni mradi mkubwa wenye thamani ya zaidi ya bil 200 mara utakapo kamilika utazalisha tani 2,000 na kuajili ya watu 300-800’
“Awamu ya kwanza ya kiwanda hiki kimegharimu dola za kimarekani mil. 45 sawa na sh. bil. 90 za kitanzania, na awamu ya pili kitagharimu zaidi ya dola milioni 100 sawa na zaidi ya bil 200, mitambo imefungwa na kipo vizuri,hivyo alimpongeza mwekezaji mzawa Mohammed Kilua”alielezea.
Waziri mkuu alisema mradi huo utakapoanza kazi utaliingizia mapato taifa kwa kiasi kikubwa ,kuwezesha ajira kwa wazawa na kuwaingizia kipato wajasiliamali.
Alisema mkoa wa Pwani unaangaliwa kupeleka viwanda na anashukuru uongozi wa mkoa na kupokea wawekezaji.
Kuhusu kiwanda cha kuunganisha magari na zimamoto Majaliwa alisema ni kiwanda mkombozi nchini.
Majaliwa alisema kwa kuunganisha matrekta na zimamoto kutarahisisha kupata kwa gharama nafuu vyombo hivyo vya moto nchini.
Nae waziri wa uchukuzi, pro. Makame Mbalawa aliomba reli hiyo itumike kwa matumizi lengwa.
Pro. Mbalawa alielezea viwanda vinavyohitajika njia za reli zinaboreshwa na kujengwa lakini pia ni jukumu la wawekezaji hao kuzitunza na kuzitumia vyema.
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,alisema serikali mkoani hapo imedhamiria kuongeza wawekezaji na ongezeko la viwanda ili kuongeza ajira hususan kwa kundi la vijana.
Alisema wapo baadhi ya wananchi waliotakiwa kupisha reli hiyo ambao wanadai fidia ya sh. mil 95.726 na halmashauri inadai sh. mil 307.206.
Mhandisi Ndikilo alisema mkoa wanayotaarifa na wanaendelea na mazungumzo ili haki yao walipwe kwa wakati.
Alisema wananafasi kubwa ya kufanikisha nchi kuwa ya viwanda kwa kushirikiana na wamiliki wa viwanda.
Mhandisi Ndikilo alisema kuwa kwa sasa mkoa wa Pwani ajenda yake ni kuhakikisha unakuwa mkoa wa viwanda na hilo linawezekana kwa kuwa na viwanda vingi vya kuzalisha bidhaa mbalimbali.
Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la reli nchini, Masanja Kadogosa, alisema waziri mkuu alitoa agizo wakamilishe reli hiyo na sasa wamemalizia.
Alisema ujenzi huo umetumia sh. Mil 863 kwa kutumia mafundi wa ndani gharama ambayo ni ndogo.
Kadogosa alielezea kwamba wangetumia mafundi wa nje gharama ingekuwa kubwa.
Alisema licha ya kumaliza reli hiyo lakini kiwanda hicho cha kilua kimeomba tena kuongezewa reli nne za ziada.
Mkurugenzi wa kiwanda hicho Mohamed Kilua alisema wanatarajia kujenga kwenye eneo hilo viwanda vingine vinne.
Alitaja viwanda vinavyotarajiwa kujengwa kuwa ni kiwanda cha kutengeneza pikipiki, gemsum, tissues na nguzo za umeme.
Kilua alisema kukamilika kwa kiwanda hicho kinaliingizia pato taifa bil.25 kwa mwaka na  kuzalisha nondo tani 2,000 kwa siku
Share:

HIZI HAPA KURASA ZA NDANI MAGAZETI YA LEO JUMAPILI TAREHE 20.11.2016

TANO BORA  KWENYE HABARI ZA MICHEZO LEO


TANO BORA  KWENYE KATUNI ZA LEO

KUMI BORA KURASA ZA NDANI MAGAZETINI LEO


1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
Share:

Saturday, 19 November 2016

Batch 7 Allocations for the 2016-2017 SUA continuing students receiving loan from HESLB

Share:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA


polisi
  • MTU MMOJA AMEUAWA NA  WATU WANAOZANIWA KUWA NI MAJAMBAZI KATIKA TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA WILAYANI NYAMAGANA.
  • MWANAMKE MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMFANYIA VITENDO VYA UKATILI MJUKUU WAKE WILAYANI NYAMAGANA.
  • MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLSI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MTOTO WA DARASA LA TATU WILAYANI NYAMAGANA.
KWAMBA TAREHE 17.11.2016 MAJIRA YA SAA 20:30HRS KATIKA MTAA WA NKURUMA KATA NA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA MWANAMKE MWENYE ASILI YA KIASIA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA VASANTBEN RAMANBHAI, MIAKA 48, MUHINDI, MAMA WA NYUMBANI NA MKAZI WA MTAA WA RUFIJI, ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI MOJA SEHEMU YA MGONGONI NA WATU WANAOZANIWA KUWA NI MAJAMBAZI WALIVAMIA DUKA LA MIAMALA YA FEDHA YA  M –PESA, TIGO PESA NA AIRTEL MONEY NA BIDHAA NYINGINE MBALIMBALI MALI YA LAURENT PETER NA KUFANIKIWA KUPORA FEDHA NA SIMU TANO.
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKWENDA DUKANI HAPO KUPATIWA HUDUMA, NDIPO GHAFLA WALITOKEA MAJAMBAZI WATATU WAKIWA NA PIKIPIKI MMOJA KATI YAO AKIWA SILAHA  NA KUFYATUA RISASI KADHAA HEWANI, NDIPO RISASI MOJA  ILIMPATA MAREHEMU SEHEMU YA MGONGONI NA KUFARIKI DUNIA . AIDHA KATIKA TUKIO HILO MAJAMBAZI HAO WALIFANIKIWA KUPORA  FEDHA AMBAZO HAIJAFAHAMIKA NI KIASI GANI HADI SASA NA SIMU TAN0, SIMU TATU KATI YA HIZO ZILIKUWA ZIKITUMIKA KUFANYA KAZI YA KUTUMA MIAMALA YA FEDHA  NA NYINGINE MBILI ZIKITUMIKA KATIKA MAWASILIANO YA KAWAIDA, ZOTE MALI ZA MWENYE DUKA.
JESHI LA POLISI LIPO KATIKA  UPELELZI NA MSAKO WA KUHAKIKISHA  WATU HAO WANAKAMTWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO SENGA ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUTULIA NA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KATIKA KUFANIKISHA KUWAKAMATA WATU HAWA WENYE NIA OVU DHIDI YA USALAMA WA WANANCHI NA MALI ZAO. TUNAENDELEA KUWASIHI WANANCHI WATULIE WASIWE NA MASHAKA JESHI LAO LA POLISI LIPO VIZURI KUHAKIKISHA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO UNAIMARISHWA.
KATIKA TUKIO LA PILI
MNAMO TAREHE 11.11.2016 MAJIRA YA 20:00HRS KATIKA MTAA WA MAHINA KATA YA BUTIMBA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA AMINA HAMISI MIAKA 56 MKAZI WA MAHINA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI BAADA YA KUMLAZIMISHA KULA KINYESI MJUKUU WAKE AITWAYE REHEMA SADIKI MIAKA 07, KITENDO AMBACHO NI UKATILI DHIDI YA MTOTO NA NI KOSA KISHERIA.
INADAIWA KUWA SIKU TAJWA HAPO JUU MTOTO HUYO ALIKWENDA CHOONI KUJISADIA NA KUSHINDWA KUMWAGIA MAJI ILI KUONDOA KINYESI CHAKE , NDIPO BIBI YAKE ILI KUMUADHIBU ALIMUAMURU  KULA KINYESI  HICHO, KITENDO AMBACHO MTOTO HUYO ALIKITEKELEZA.
AIDHA BAADA MTUHUMIWA KUFANYA UKATILI HUO KWA MTOTO. RAIA WEMA  WALITOA TAARIFA  POLISI AMBAO WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA HUYO. UPELELEZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA MOJA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO SENGA ANATO WITO KWA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA AKIWATAKA KUSHIRIKIANA KWA PAMOJA NA JESHI LA POLISI KATIKA KUDHIBITI VITENDO VYA UKATILI HASA KWA WATOTO KATIKA MKOA WETU. ALIONGEZA KUWA UKATILI NI KOSA KISHERIA  HIVYO WANANCHI WAACHE KUFANYA VITENDO HIVYO NA WATAKAO BAINIKA SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE.
KATIKA TUKIO LA TATU.
KWAMBA TAREHE 16.11.2016 MAJIRA YA SAA 19:00HRS KATIKA MTAA WA NYABUROGOYA KATA YA NYEGEZI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTOTO JINA TUNALIHIFADHI MWENYE UMRI WA MIAKA 11, MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU SHULE YA MSINGI NYABUROGOYA ALIBAKWA NA MTU ALIYEJULIKANA KWA JINA LA JAMES CHIRAGWIRE MIAKA 42, AFISA MTENDAJI KATA YA MKUYUNI NA KUMSABABISHIA MAUMIVU MAKALI KATIKA SEHEMU ZAKE ZA SIRI, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ANAISHI JIRANI NA NYUMBANI KWA MTOTO HUYO ANAYEISHI NA MAMA YAKE MZAZI, AIDHA INASEMEKANA KUWA MTUHUMIWA ALIKUWA NA MAZOEA YA KUMCHUKUA MTOTO HUYO NA KUINGIA NAE NDANI KWAKE NA KUMPATIA FEDHA NA ZAWADI NDOGONDOGO NDIPO SIKU HIYO ALIPOFIKA NYUMBANI KWAO, MTOTO ALIMKUTA PEKE YAKE NDIPO ALIMCHUKUA MTOTO HUYO NA KUMFUNGA KITAMBAA USONI KISHA AKAINGIA NAE NDANI KWAKE NA KUMFANYIA UKATILI HUO.
AIDHA MTOTO AMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUBAINIKA KWAMBA  KWELI AMEINGILIWA KIMWILI, MTOTO YUPO HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE  AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU, MTUHUMIWA WA UHALIFU HUO AMEKAMATWA, AIDHA JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO SENGA ANATOA WITO KWA WANANCHI WA MKOA WA MWANZA, AKIWATAKA KUWA MAKINI WAKATI WOTE NA WATOTO WADOGO WASIACHWE PEKE YAO ILI KUEPUSHA VITENDO KAMA HIVI, LAKINI PIA ANAWASIHI  WANANCHI KUTOA TAARIFA POLISI ZA WATU WENYE TABIA KAMA HIZI ILI HATUA STAHIKI ZIWEZE KUCHUKULIWA.

IMETOLEWA NA:
ACP: AUGUSTINO SENGA
KAIMU KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
Share:

Canada: Mtuhumiwa mwingine wa mauaji ya kimbari arejeshwa Rwanda


media
Mtuhumiwa wa mauaji ya Rwanda, Jean Claude Seyoboka, wakati alipowasili KIgali.
Afisa wa zamani kwenye jeshi la Rwanda, amewasili jijini Kigali baada ya kusafirishwa kutokea nchini Canada, akituhumiwa kuwa alihusika kwenye mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, ambayo watu laki 8 waliuawa.
 Mwendesha mashtaka wa Rwanda, Jean-Bosco Mutangana, amethibitishwa kurejeshwa nchini humo kwa mtuhumiwa Jean Claude Seyoboka, usiku wa kuamkia leo, ambapo sasa atajibu tuhuma za mashataka ya mauaji yanayomkabili.
Seyoboka, ambaye alikuwa ni Luteni wa pili kwenye jeshi la Rwanda, anatuhumiwa kuhusika na mauajiya watusi zaidi ya 72 jijini Kigali na pia anadaiwa kuwa alihudhuria vikao vilivyoidhinisha mauaji hao.Machafuko hayo yaliyodumu kwa miezi minne, ambapo watu zaidi ya laki 8 waliuawa wengi wakiwa watusi, yalichangiwa baada ya kudunguliwa kwa ndege iliyokuwa imembeba rais wa nchi hiyo Juvenal Habyarimana ambaye alikuwa Muhutu, mwezi April mwaka 94.
Seyoboka aliwasili nchini Canada mwaka 1995, ambako alipatiwa hifadhi ya kudumu nchini humo mwaka mmoja baadae.Hata hivyo kibali cha hifadhi yake kilitenguliwa miaka kumi baadae, baada ya kutolewa ushahudi kwenye mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari ya Rwanda iliyokuwa jijini Arusha, Tanzania na kumuhusisha na mauaji hayo.
Mamlaka nchini Rwanda zilitoa waranti ya kukamatwa kwa Seyoboka mwaka huu, lakini alipigana kupinga kurejeshwa nchini mwake kwa kile alichosema anahofia usalama wake na mateso.
Seyoboka anakuwa mtuhumiwa wa pili wa mauaji ya kimbari kusafirishwa kutoka nchini Canada, baada ya mwanasiasa wa zamani wa nchi hiyo Leon Mugesera kurudishwa nchini Rwanda mwaka 2012.
Mugesera alihukumiwa kifungo cha maisha jela, mwezi April mwaka 1994 kwa madai ya kuhusika kwenye mauaji ya maelfu ya raia.Juma lililopita pia, mwendesha mashtaka wa Uholanzi, alithibitisha kuwa raia wawili wa Rwanda ambao ni watuhumiwa wa mauaji hayo, nao watarejeshwa nchini mwao.
Nchi ya Rwanda iliomba kurejeshwa nchini humo kwa raia wake Jean-Claude Lyamuremye na Jean-Baptiste Mugimba, mwaka 2012 na 2013, ili warudi kukabiliana na tuhuma za kesi za mauaji na uhalifu dhidi ya binadamu
Share:

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA UTEUZI VIONGOZI MBALIMBALI


diaw
Share:

Obama akutana na viongozi wa Ulaya


Deutschland Sechser-Treffen mit Merkel und Obama im Kanzleramt (picture-alliance/dpa/K. Nietfeld)
Viongozi wa Ulaya wako Berlin kutaka kuhakikishiwa na Rais Barack Obama wa Marekani juu ya mkondo ambao yumkini ukafuatwa na rais mteule wa Marekani Donald Trump kutokana na ahadi zake kuweza kutibua mfumo wa dunia,
Rais Obama amekaririwa akisema "Kujitolea kwetu kwa Ulaya ni kwa kudumu na misingi yake iko katika maadili tunayoshirikiana maadili ambayo Angela ameyataja,kujitolea kwetu kwa demokrasia,kujitolea kwetu kwa utawala wa sheria,kujitolea kwa utu wa watu katika nchi zetu na katika dunia. Muungano wetu wa washirika wetu wa NATO umekuwa msingi wa sera ya kigeni ya Marekani kwa takriban miaka sabini katika nyakati mbaya na nzuri na kwa kupitia marais wa vyama vyote viwili na kwa sababu Marekani ina utashi wa msingi kwa utulivu na usalama wa Ulaya."
Rais Barack Obama wa Marekani alitowa kauli hiyo katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Berlin hapo Alhamisi (17.11.2016) ambao pia ilihudhuriwa na mwenyeji wake Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.
Fadhaa ya kuchaguliwa kwa Trump imewatia wasi wasi viongozi wa Ulaya kutokana na kiongozi huyo kuhoji mkataba wa usalama uliodumu kwa takriban miaka sabini wa washirika wa Marekani chini ya kivuli cha Jumuiya ya Kujihami ya NATO pamoja na kuahidi kujitowa katika mikataba iliopatikana kwa  tabu ya mabadiliko ya tabia ya nchi na kudhibiti mpango wa nyuklia wa Iran.
Kujipendekeza kwa Putin
Kujipendekeza kwake kwa Rais Vladimir Putin wa Russia pia kumezusha masuali juu ya msimamo wake juu ya hatua ya Russia kumuunga mkono Rais Bashar al Assad katika vita vya Syria na halikadhalika dhima ya Russia katika mzozo mashariki mwa Ukraine.
Kabla ya kufanyika kwa mazungumzo hayo Obama alikuwa na matumaini ya hadhari kwamba Trump anaweza kubadili msimamo wake mara ataposhika wadhifa huo wa urais.Amesema mtu inabidi awe makini akiwa katika wadhifa huo venginevyo hutoweza kudumu kwa muda mrefu kwani matatizo yatakuja kukuumbuwa.
Obama amesema anatumai kwamba rais mteule atakuwa na mtizamo ule ule wa tija kutafuta nyanja ambapo wanaweza kushirikiana na Russia pale maadili yao, utashi wao vinakwenda sambamba lakini rais mteule atakuwa tayari kusimamama dhidi ya Russia pale inapokiuka maadili yao na kanuni za kimataifa.
Kubadilishana mawazo
Mkutano wa leo kati ya Obama na viongozi wa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani,Italia na Uhispania ni wa kwanza kufanyika tokea kuchaguliwa kwa Trump.
Mkutano huo utatowa nafasi ya kubadilishana mawazo hadharani kwa njia isio rasmi juu ya masuala muhimu ya kimataifa mathlan mada nzito ya mapambano yanayongozwa na Marekani dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu nchini Syria na Iraq halikadhalika suala la mzozo wa wahamiaji barani Ulaya.
Obama amesema Umoja wa Ulaya unaendelea kuwa mojawapo ya mafanikio makubwa ya kisiasa na kiuchumi duniani mafanikio ambayo hayapaswi kuchukuliwa kijujuu
Share:

HIZI HAPA KUREASA ZA NDANI MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBER TAREHE 19.11.2016

TANO BORA KWENYE HABARI ZA MICHEZO LEO


TANO BORA  KWENYE KATUNI ZA LEO


KUMI BORA  KURASA ZA NDANI MAGAZETINI LEO


1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger