Sunday, 5 June 2016
Saturday, 4 June 2016
VIDEO: Askari wa Usalama Barabarani akichukua Rushwa - Juni 01, 2016
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Huyu ni askari anayesadikiwa kutoka katika kituo cha Urafiki, kilichoko Ubungo Dar es Salaam.
Alikuwa na wenzake wapatao wanne au watano, mmoja akiwa katika sare za jeshi pia, na wengine wakiwa katika mavazi ya kiraia. Walitega mingo katika makutano ya barabara ya Ubungo Maziwa na Barabara ya Morogoro. Walikuwa wakichukua rushwa kwa dereva wa bodaboda na magari. Mengine, jionee zaidi.
Huyu ni askari anayesadikiwa kutoka katika kituo cha Urafiki, kilichoko Ubungo Dar es Salaam.
Alikuwa na wenzake wapatao wanne au watano, mmoja akiwa katika sare za jeshi pia, na wengine wakiwa katika mavazi ya kiraia. Walitega mingo katika makutano ya barabara ya Ubungo Maziwa na Barabara ya Morogoro. Walikuwa wakichukua rushwa kwa dereva wa bodaboda na magari. Mengine, jionee zaidi.
Bibi kizee akutwa nyumbani kwa Waziri Nchemba akichawia
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Bibi kizee alivyonaswa usiku akirandaranda na tunguri nyumbani kwa Waziri Mwigulu Nchemba.
Stori: Francis Godwin, Risasi Jumamosi
DODOMA: Katika hali
isiyo ya kawaida bibi kikongwe mmoja ambaye hakuweza kujulikana jina
lake, amezua sintofahamu baada ya kukutwa nyumbani kwa Waziri wa Kilimo,
Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akizunguka nyumba yake usiku huku
akiwa na tunguri na wembe wenye damu.
Tukio
hilo lilitokea Mei 31, mwaka huu majira ya saa 6 usiku katika eneo la
Kilimani mjini Dodoma kwenye nyumba ya waziri huyo ambako ni makazi ya
mawaziri na viongozi mbalimbali wa umma.
Akizungumza na mwandishi wetu, eneo la
tukio, shuhuda wa tukio hilo, Sumai Juma alisema kuwa alimwona mwanamke
huyo akiwa amekumbatia vitu vyake akizunguka nyumba ya waziri.
Baada
ya kumwona mtu huyo, alilazimika kuita mlinzi na kujaribu kumhoji bila
mafanikio kutokana na mwanamke huyo kutojua lugha yoyote na kila
anachoulizwa alikuwa hajibu zaidi ya kurudia maneno yaleyale ambayo
alikuwa akimuulizwa.
“Huyu
kikongwe alikuwa kama na zaidi ya miaka 70 hivi, nilimwona akiwa
amesimama katika dirisha la mheshimiwa waziri na baada ya kumfuata
alianza kuzunguka nyumba hiyo asijue mlango wa kutokea…nyumbani hapa
kuna uzio mrefu sana ambao bibi kama huyu hana uwezo wa kupanda na
getini muda wote kuna walinzi wa Kampuni ya Moku Security ambao
hawakumwona akiingia getini hapo,” alisema Juma.
Hata hivyo, alisema baada ya kumkamata
walichunguza mzigo aliokuwa amebeba ambao ulifungwa katika kanga,
kulikuwa na kuni kama 17 hivi, kikopo chenye vitu kama ungaunga mweusi
mfano wa vumbi, mkaa na wembe aina ya Topaz uliokuwa haujafunguliwa ila
ulikuwa umelowa damu.
Juma
aliongeza kuwa, baada ya kumkagua na kutokana na mtu huyo kutojitambua,
walilazimika kumpeleka Kituo cha Polisi Dodoma ambako walimweka
mahabusu baada ya kushindwa kujieleza na asubuhi Waziri Nchemba
alilazimika kwenda kuruhusu kuachiwa huru baada ya kumsamehe.
Kwa
upande wake Waziri Nchemba alisema ameshindwa kujua lengo la mwanamke
huyo katika nyumba yake lakini yeye hana hofu yoyote kwani yupo kwa
ajili kuwatumikia wananchi kwa nafasi yake ya uwaziri na hivyo kazi yake
anayoifanya anaiweza kwa kuwa anamtanguliza Mungu mbele.
Hata hivyo, alitoa wito kwa Watanzania
kuendelea kuliombea taifa kwani kazi kubwa ambayo serikali ya Rais Dk.
John Pombe Magufuli inayofanya ni tunu kubwa ya nchi yetu.
Wasanii wafanya uchafu!
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Zainabu Ally na Naomy Mmbaga wakifanya yao.
Stori: Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Katika
hali ya kushangaza, wasanii wa kike wanaochipukia kwenye anga la filamu
Bongo, Zainabu Ally na Naomy Mmbaga, wamenaswa wakifanya vitendo vichafu
wakiwa lokesheni.
Tukio hilo lililopigwa chabo na kachero
wetu, lilijiri juzikati katika Hoteli ya KD iliyopo maeneo ya Akachube,
Kijitonyama jijini Dar wakati wasanii hao walipokuwa wakiigiza muvi yao
ndipo walipofanya uchafu huo baada ya kukolea na ‘ulabu’.
“Awali kabla ya kuanza kurekodi walianza
kupiga mambo yao, baada ya kurekodi ndipo wakaongezea tena mitungi na
hapo ndipo walipokolea na kuanza kufanya mambo ya ajabu,” alizungumza
kachero wa kujitegemea aliyeshuhudia tukio hilo.
Kachero wetu alifanikiwa kuwafotoa picha
kadhaa lakini alipojaribu kuwauliza kulikoni wafanye vitendo hivyo
ambavyo ni kinyume na maadili ya Kitanzania, wasanii hao hawakutoa
majibu ya moja kwa moja kutokana na kukolea ulabu.
Hata hivyo, kesho yake Naomy alipatikana
na alipoulizwa kwa nini walifanya vitendo hivyo aliomba stori hiyo
isitoke kwa madai itamharibia.
“Please iache hiyo bwana, itaniharibia.
Si unajua yale ni mambo ya lokesheni tena, mzee akijua itakuwa noma,”
alisema Naomy ambaye ameshauza nyago kwenye Sinema ya Laghai, Penzi la
Giza, F.B.I, Part of Job Samira na nyingine kibao.
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUAHIRISHWA KWA USAILI WA 08-09 JUNI 2016
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya
Tanzania Metrological Agency (TMA), Tanzania Meat Board (TMB), The Local
Government Training Institute (LGTI) na Registration, Insolvency And
Trusteeship Agency (RITA) alitoa tangazo katika tovuti ya Sekretarieti
ya Ajira la kuita kwenye usaili tarehe 1 Juni, 2016 waombaji wa kazi
waliowasilisha maombi na kukidhi vigezo kwa taasisi zilizoanishwa hapo
juu. Kupitia tangazo hili Waombaji kazi wote waliotangaziwa kuitwa
kwenye usaili kwa tangazo hilo wanafahamishwa kuwa usaili huo
umeahirishwa mpaka hapo watakapotangaziwa tena hapo baadaye. Kwa
Matangazo ya nafasi za kazi yaliyotolewa mnamo tarehe 6 Mei, 2016, 11
Mei, 2016, 18 Mei, 2016 na tarehe 26 Mei, 2016 nayo waombaji kazi
watakaokidhi vigezo watataarifiwa hapo baadae kuhusu mchakato wake
unavyoendelea. Aidha, Kupitia tangazo hili, Sekretarieti ya Ajira kwa
niaba ya Serikali inaomba radhi waombaji kazi wote waliowasilisha maombi
na wale waliokuwa wamejiandaa kuhudhuria usaili huo kwa usumbufu wowote
utakaojitokeza.
Tanzania imetolewa na Misri michuano ya AFCON 2017 leo June 4
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
June 4 2016 ilikuwa ni siku ambayo timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars itacheza mchezo wake wa tatu wa Kundi G wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika 2017 AFCON, kwa kucheza na timu ya taifa ya Misri The Pharaos uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Huu ni mchezo ambao Taifa Stars alikuwa anahitaji ushindi wa aina yoyote ile.
Huu ulikuwa ni mchezo wa tatu kwa Taifa Stars, lakini ulikuwa ni mchezo wa marudiano na timu ya taifa ya Misri baada ya mchezo wa kwanza kuchezwa Misri June 14 2015 katika mji wa Alexandria na kumalizika kwa Taifa Stars kufungwa jumla ya magoli 3-0, hivyo huu ulikuwa ni mchezo wa kulipa kisasi kwa Taifa Stars, lakini pia ulikuwa ni mchezo wa kutengeneza mazingira ya kufuzu AFCON 2017.
Hata hivyo timu ya Taifa ya Tanzania licha ya kuwa nyumbani imekubali kipigo cha goli 2-0, , magoli ya Misri yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea anayeichezea klabu ya AS Roma ya Italia Mohamed Salah dakika ya 43 na 58, kwa upande wa Tanzania Mbwana Samatta alikosa penati iliyopatikana baada ya Himid Mao kufanyiwa faulo ndani ya 18.
Kwa matokeo hayo Taifa Stars wanakuwa wametolewa rasmi katika michuano ya kuwania kufuzu AFCON 2017, lakini imebakiza mchezo mmoja wa kukamilisha ratiba itakayocheza September dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles, Misri imefikisha jumla ya point 10, Taifa Stars point moja na Nigeria ina point 2.
Watumishi 11 wasimamishwa kazi kwa kuwa na vyeti feki vya form 4
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Watumishi 11 mkoani wa idara ya afya mkoani Mbeya wamesimamishwa kazi baada ya kukutwa na kosa la kughushi vyeti vya kidato cha nne hilo limefanyika baada ya zoezi la kuhakikisha vyeti kwa kushirikiana na baraza la mitihani NECTA ikiwa ni mwitikio wa agizo alilotoa rais John Magufuli
Amesema waliwakilisha vyeti vingi NECTA na hivyo 11 ndio vikabainika vilikuwa vya kughushi ambao karibia wote ni wanawake
Watumishi 11 mkoani wa idara ya afya mkoani Mbeya wamesimamishwa kazi baada ya kukutwa na kosa la kughushi vyeti vya kidato cha nne hilo limefanyika baada ya zoezi la kuhakikisha vyeti kwa kushirikiana na baraza la mitihani NECTA ikiwa ni mwitikio wa agizo alilotoa rais John Magufuli
Amesema waliwakilisha vyeti vingi NECTA na hivyo 11 ndio vikabainika vilikuwa vya kughushi ambao karibia wote ni wanawake
KUAHIRISHWA KWA USAILI UTUMISHI - 6/3/2016
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Katibu
wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Tanzania
Metrological Agency (TMA), Tanzania Meat Board (TMB), The Local
Government Training Institute (LGTI) na Registration, Insolvency And
Trusteeship Agency (RITA) alitoa tangazo katika tovuti ya Sekretarieti
ya Ajira la kuita kwenye usaili tarehe 1 Juni, 2016 waombaji wa kazi
waliowasilisha maombi na kukidhi vigezo kwa taasisi zilizoanishwa hapo
juu.
Kupitia
tangazo hili Waombaji kazi wote waliotangaziwa kuitwa kwenye usaili kwa
tangazo hilo wanafahamishwa kuwa usaili huo umeahirishwa mpaka
watakapotangaziwa tena hapo baadaye.
Kwa
Matangazo ya nafasi za kazi yaliyotolewa mnamo tarehe 6 Mei, 2016, 11
Mei, 2016, 18 Mei, 2016 na tarehe 26 Mei, 2016 nayo waombaji kazi
watakaokidhi vigezo watataarifiwa hapo baadae kuhusu mchakato wake
unavyoendelea.
Aidha,
Kupitia tangazo hili, Sekretarieti ya Ajira kwa niaba ya Serikali
inaomba radhi waombaji kazi wote waliowasilisha maombi na wale waliokuwa
wamejiandaa kuhudhuria usaili huo kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na
X.M. DAUDI
KATIBU
Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma.
Mambo Mawili Yanayoibana Serikali Katika Mgogoro wa Wanafunzi 7000 Waliotimuliwa UDOM
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Kitilla Mkumbo amesema
kuna mambo mawili yanayoibana Serikali katika mgogoro wa wanafunzi
waliotimuliwa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).
Akizungumza
jana kwenye kipindi cha ‘Kipima Joto’ kinachorushwa na kituo cha
luninga cha ITV, Profesa Mkumbo alisema Serikali haiwezi kukwepa lawama,
kwa sababu ndiyo iliyoanzisha utaratibu wa kudahili wanafunzi wa kidato
cha nne kupitia mfumo maalumu kabla ya kuanza kusoma shahada ya chuo
kikuu.
Pia,
alisema Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), haiwezi kuhusika moja kwa
moja kwenye udhaifu uliojitokeza katika udahili wa wanafunzi hao, bali
Seneti ya Udom inapaswa kuwajibika katika hilo.
Alisema
kuna udhaifu wa kiutendaji kwa seneti hiyo yenye mamlaka ya kudahili
wanafunzi wenye sifa ambayo iliiacha kazi hiyo mikononi mwa TCU.
Mkumbo alisema kazi ya TCU ni kuidhinisha majina ya wanafunzi waliokwisha dahiliwa na chuo husika na si kuchagua.
“Chuo
chochote ndicho kinachagua wanafunzi wenye sifa wanazozihitaji,
inashangaza kuona Udom imefanyiwa kazi hiyo, baraza na seneti wanapaswa
kuwajibika kwanza, TCU haiwezi kukichagulia chuo wanafunzi,” alisema Profesa Mkumbo.
Hata
hivyo, alitoa angalizo kwa Serikali kutodharau mfumo huo wa udahili kwa
wanafunzi ambao hawakuhitimu Kidato cha Sita kama ilivyoamriwa na
Serikali ya Awamu ya Nne, kuwa upo na unatumika duniani kote.
“Ila
kama Rais (John) Magufuli hautaki na ameona turudi kwenye mfumo wa
zamani ambao mwanafunzi anapaswa kufaulu kidato cha sita ndiyo ajiunge
na chuo kikuu sawa, lakini atambue kuwa kuna hasara na faida zake, vyuo
vingi vinaweza kufungwa,” alisema Mkumbo
Mbali
ya mfumo huo, profesa huyo alisema upo mfumo mwingine wa udahili kwa
mtu yeyote mwenye umahili katika taaluma yake kusoma shahada kwa
kuzingatia vigezo maalumu vilivyowekwa.
“Ila hakuna jinsi, nadhani TCU wamemsikia Rais kuwa hataki njia za mkato tena.”
Mei
29, Udom iliwasimamisha masomo zaidi ya wanafunzi 7,000 wa kozi maalumu
ya ualimu wa sayansi kwa ngazi ya stashahada na kuwataka waondoke
chuoni mara moja.
Amri
hiyo iliyotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya
Ufundi, ilisema Serikali imeamua warejee kwao na wataelezwa mustakabali
wao mapema iwezekanavyo.
Hata
hivyo, Rais John Magufuli juzi alisema baadhi yao walikuwa vilaza,
hivyo wajitafutie mahali pa kwenda huku wenye ufaulu wa daraja la kwanza
na pili aliahaidi kuwa wataandaliwa utaratibu.
Wabunge wa CCM Wapinga Shinikizo la Wapinzani Kutaka Kumng'oa Naibu Spika, Dk.Tulia Ackson
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Kakunda alisema anaamini pia kuwa maamuzi hayo ya kambi ya upinzani yana msukumo wa kisiasa kwa sababu hoja zao hazina msingi
WABUNGE
watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiongozwa na Dk Abdallah Possi
ambaye ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,Kazi,
Ajira, Vijana na Walemavu), wameutaka umma uelewe kuwa shinikizo la
wapinzani bungeni kuhusu utendaji wa Naibu Spika, Dk Tulia Ackson lina
uonevu wa kijinsia.
Katika
mkutano huo na wanahabari uliofanyika ofisi za Waandishi wa Habari,
bungeni mjini Dodoma jana, Dk Possi aliongozana na Mbunge wa Muleba
Kusini, Profesa Anna Tibaijuka na Mbunge wa Sikonge, Joseph Kakunda.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti, walisema hawakubaliani na mkakati wa kambi ya
upinzani kutaka kumng’oa Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, kwa sababu ni
mkakati wenye shinikizo la kisiasa na ubaguzi dhidi ya wanawake.
Dk
Possi alisema wabunge wa kambi ya upinzani hawana hoja za msingi kutaka
kutekeleza mkakati wao huo kwa sababu si mara ya kwanza kwa wanaokiuka
kanuni na taratibu za Bunge kutolewa au kusimamishwa.
“Tunaamini
kinachotokea sasa ni msukumo wa kisiasa kwa kuwa wabunge wana njia ya
kufanya kuwasilisha malalamiko yao, ikiwa wanaona wameonewa na si
kupanga mkakati wa kumtoa madarakani wanayeamini anawakosea. Wana nafasi
ya kukata rufaa,” alisema Dk Possi.
Profesa
Tibaijuka alisema wakati Samwel Sitta akiwa Spika aliwatoa wabunge
wasiofuata kanuni na hakukuwa na yanayotokea sasa, jambo linaloonesha
kuwa wanamlenga Dk Tulia kwa sababu ni mwanamke.
waziri Mpango Aomba Apewe Majina ya MAJIPU BoT
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
WAZIRI
wa Fedha, Dk Phillip Mpango, amemtaka Mbunge wa Tabora Kaskazini, Almas
Maige (CCM) kumpa ushahidi ikiwemo majina ya wafanyakazi wa Benki Kuu
ya Tanzania (BoT), aliowatuhumu kufanya biashara na mwajiri wao.
Dk
Mpango alisema hayo Jumatano usiku alipokuwa akijibu hoja za wabunge
kuhusu Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango na kuongeza kuwa akipewa
ushahidi huo, ataufanyia kazi.
Awali
katika mchango wake, Maige alisema anao ushahidi wa maandishi (huku
akiwa ameushika), unaoonesha kuwa kati ya mashirika ya umma yanayovunja
Sheria ya Manunuzi, BoT ipo.
Alidai
kuwa Sheria ya Manunuzi imetoa fursa ya kuanzishwa kwa vitengo na idara
za manunuzi (PMU), lakini fursa hiyo imekuwa ikitumiwa vibaya na vijana
wa vitengo, hivyo kuiibia Serikali.
Kwa
mujibu wa madai ya Maige, katika benki hiyo kuna vijana wamefungua
makampuni ambao wamekuwa wakiyatumia kuomba zabuni za benki hiyo na
kuyalipa.
Mbali
na tuhuma hiyo, Maige ambaye alitangaza maslahi kuwa yeye ni mkandarasi
wa daraja la kwanza, alidai pia kuna vijana wengine wamekuwa wakitoa
zabuni kwa kampuni za nje ya nchi, ili watumie zabuni hiyo kupata safari
za nje.
Alidai
kuwa vijana hao baada ya kutoa zabuni kwa kampuni za nje, hutengeneza
safari za kwenda kufanya uhakiki (due diligence) katika nchi zinakotoka
kampuni hizo, ambako huko hupokea rushwa.
Katika
kuthibitisha hilo, Maige alidai kuwa vijana hao wamediriki kutoa zabuni
kwa kampuni iliyofungiwa na Mamlaka ya Manunuzi ya Umma Tanzania
(PPRA).
Akijibu
hoja hiyo, Dk Mpango alisema tuhuma hizo ndio kazisikia bungeni, hivyo
hana uhakika ila akipewa ushahidi ataufanyia kazi kwa kuwa, utumbuaji
majipu umesaidia kuongeza mapato na kutoka mfano wa makusanyo ya Sh
trilioni moja kila mwezi.
Hivi
karibuni, Serikali ilisitisha utoaji wa Sh bilioni 925 zilizokuwa
zimeidhishwa na BoT kwa ajili ya kulipa malimbikizo ya madeni ya
Serikali.
Mbali
na hilo, Serikali iliagiza Kitengo cha Madeni ya Nje ambacho awali
kilikuwa chini ya BoT na baadaye kupelekwa wizarani, kirejeshwe mara
moja ili kuimarisha udhibiti wa ukopaji na ulipaji wa madeni.
Kabla
ya agizo hilo, ilielezwa kuwa malipo hayo yalikuwa yameidhinishwa na
BoT kwa ajili ya kulipa malimbikizo ya madeni mbalimbali lakini Serikali
ikaagiza fedha hizo zirejeshwe Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya
kufanyiwa uhakiki upya.
Vitisho Kwa Njia ya Simu Vyamfikisha Mahakamani.
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mkazi
wa Kijiji cha Misasi Mariamu Nestory (20) amefikishwa Mahakama ya
Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kujibu shtaka la kutoa lugha ya vitisho
kwa njia ya simu.
Mwendesha
Mashtaka wa Polisi, Doroth Mgenyi alidai kuwa Mei 2 saa 8:15 mchana,
mshtakiwa huyo kwa kutumia simu aliandika ujumbe wa vitisho kwa Diana
Kabula kinyume cha sheria ya makosa ya mtandao kifungu 18 (1) ya mwaka
2015.
Alinukuu ujumbe huyo akidai: “Ujiandae
siku utakayoingia anga zangu, sali sala ya mwisho, ulisikia kisa cha
Sengerema ndivyo nitakavyokufanya... ikishindikana kukuua kwa mikono
yangu nitakuroga uwe kichaa.”
Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana shtaka.
Kauli za Rais Magufuli Zawa Gumzo Nchini
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Kauli mbalimbali zinazoendelea kutolewa na Rais John Magufuli, zimezua mjadala miongoni mwa wasomi nchini.
Kwa
mfano, wanasema kauli ya kukosoa udahili wa wanafunzi katika Chuo Kikuu
cha Dodoma (Udom) na ile ya kuelekeza hatua za kuchukua dhidi ya watu
wanaotumia kimakosa barabara za Mabasi Yaendayo Haraka (Udart),
inaashiria kuna tatizo kubwa la utendaji serikalini.
Walisema
ni jambo lisiloingia akilini, wanafunzi wadahiliwe na kuanza masomo
kisha baadaye wafukuzwe kwa maelezo kuwa Serikali haiwezi kulipia ada
wanafunzi ‘vilaza’.
Akizungumzia kauli hizo jana, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk James Jesse alisema hakuna sheria za usalama barabarani zinazotamka mtu akifanya kosa gari lake litolewe magurudumu.
Juzi
wakati akiweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa maktaba ya kisasa
ya UDSM, Rais Magufuli alisema mpango maalumu uliopitishwa na Serikali
ya Awamu ya Nne wa wanafunzi kusoma diploma ya ualimu Udom, unajumuisha
waliofeli.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Hamad Salim alihoji: “Rais
amesema wanafunzi waliopo Udom ni vilaza ila waziri wa elimu (Profesa
Joyce Ndalichako) alisema wanafunzi wanaosoma mafunzo hayo hakuna
aliyepata daraja la nne. Sasa hapo nani mkweli.”
“Kupishana huku kwa kauli kunatupa mashaka na utendaji kazi wa baadhi ya viongozi serikalini."
Hamad alisema suala kama hilo lilipaswa kutolewa ufafanuzi na waziri husika na si Rais.
Alisema umefikia wakati wa kiongozi huyo mkuu wa nchi kubaini changamoto na kutoa maelekezo na si kuzungumzia kila kitu.