Monday, 23 June 2014
MGIMWA ATUMIA USAFIRI WA BAISKELI KUWATEMBELEA WANANCHI WAKE,SOMA HAPA
Mbunge wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa Godfrey Mgimwa akitumia usafiri wa Baiskeli kuwafikia
"KONDOMU" ZANASWA UKUMBI WA BUNGE,SPIKA ASHITUSHWA
Inaweza
kuonekana ni kituko cha aina yake, lakini ni kweli kimetokea kwenye
Ukumbi wa Bunge la Kaunti ya Nairobi na kuwaacha wabunge vinywa wazi.
Katika hali isiyo ya kawaida,
boksi la kondomu lilikutwa ndani ya ukumbi huo na kuwashtua wabunge wote akiwamo spika wa bunge hilo.
Mwakilishi
wa eneo la Karura, Kamau Thuo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuliona boksi
hilo na kuwashtua wabunge wengine hali iliyoibua mjadala mzito.
Kutokana
na sintofahamu hiyo Spika Alex Ole Magelo aliwataka wahudumu kufungua
boksi hilo kujua kilichomo ndani yake ndipo walipokuta kondomu.
MMUME WA FLORA MBASHA:MWAKA WA MAJANGA KWANGU NIMETAPELIWA HATI YA NYUMBA NA VIWANJA
MAJANGA! Siku
chache baada ya kuachiwa kwa dhamana katika kesi ya kudaiwa kumbaka
shemejiye, mwimbaji wa Injili na mfanyabiashara Bongo, Emmanuel Mbasha
amedaiwa kuibiwa hati za nyumba na viwanja.
Mfanyabiashara Bongo, Emmanuel Mbasha mume wa Flora Mbasha.
Sunday, 22 June 2014
KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU PROFESA MCHOME AZINDUA OFISI ZA NACTE MIKOANI
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome
(kulia) akimkabidhi Edward Mneda nyaraka za utendaji kazi kufuatia
kuteuliwa kuwa Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Kanda
ya Kati. Kushoto ni Mkuu wa Kanda Msaidizi wa Kanda ya Ziwa Beatrice
Mpanda. Baraza hilo limefungua ofisi katika kanda tano Dodoma, Arusha,
Zanzibar, Mbeya na Mwanza kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake.
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) YAJA NA MBINU YA KUDHIBITI MITANDAO
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), inajipanga kuja na mfumo wa kompyuta
utakaoratibu taarifa zote zinazopakiwa mtandaoni ili kukabiliana na
vitendo vya udhalilishaji vinavyofanywa na watu wasio na maadili ya
uandishi wa habari.
LOWASSA ATANGAZA"UAMUZI MGUMU"
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Monduli. Waziri Mkuu wa zamani
na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa ametangaza kuanza kwa
hatua za kuyarejesha kwenye Mamlaka za Serikali za Vijiji mashamba 21 ya
wawekezaji yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 10,000, ambayo
hayajaendelezwa.
Mapendekezo ya Kamati za Bunge Maalumu yanayodhoofisha Muungano – 2
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Makala haya ni mwendelezo wa makala yaliyoanza
wiki iliyopita. Madhumuni ya makala hizi ni kupitia kamati zote za Bunge
Maalumu kiuchambuzi ili kubaini mapendekezo ambayo yanadhoofisha
Muungano. Aidha, uchambuzi huu utawawezesha wadau wote katika mchakato
wa kuandika Katiba Mpya ya Tanzania ikiwamo wajumbe wa Bunge Maalumu la
Katiba kuwa na utambuzi wa kina kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya.
Kamati namba 1 katika ukurasa wake wa 8 inasema
“kiutawala na kimamlaka” Serikali ya Muungano kama ilivyopendekezwa
katika Rasimu inatenganishwa na wananchi kwa sababu haihusiki na mambo
yanayowagusa wananchi moja kwa moja. Hoja hii ya Kamati haina mashiko na
haiakisi uhalisia sasa wa namna Serikali inaevyoenenda kiutawala na
kimamlaka, lakini pia huu sio uhalisia wa yaliyomo katika Rasimu ya
Katiba Mpya Toleo la Pili.
VYAMA VYA SIASA TANZANIA VYAIPINGA NEC
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Hatua ya
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuandika upya daftari la kudumu la
wapiga kura, imeendelea kupingwa kwamba haijavishirikisha vyama vya
siasa nchini kama wadau muhimu.Katika mahojiano na Tanzania Daima
Jumapili, Katibu Mkuu wa NCCR – Mageuzi, Mosena Nyambabe, alisema NEC
itegemee changamoto nyingi kujitokeza katika mchakato ambao wameupanga
na Serikali ya CCM.
JAHAZI MODERN TAARAB: YAZINDUA ALBAMU MPYA IITWAYO 'CHOZI LA MAMA'
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Meneja
wa Jahazi Modern Taarab, Mohammed Rashid Mauji 'Father Mauji' pamoja na
shabiki wa Jahazi wakizindua albamu mpya iitwayo Chozi la Mama
Saturday, 21 June 2014
WIZARA YA AFYA YATANGAZA:MAOMBI YA NAFASI ZA MAFUNZO 2014/2015
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
WIZARA YA AFYA INATANGAZA NAFASI ZA MAFUNZO MWAKA WA MASOMO
WIZARA YA AFYA INATANGAZA NAFASI ZA MAFUNZO MWAKA WA MASOMO
ASKARI MAGEREZA WAPO FITI:ANGALIA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAGEREZA NCHINI CHUO CHA UKONGA DAR!
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY