Kichanga kikiwa kimetupwa eneo la mto Ng'ombe Tandale jijini Dar.
Wakazi wa Tandale wakiwa eneo la mto Ng'ombe kushuhudia tukio hilo.
MWILI wa kichanga kinachokadiriwa kuwa na miezi kati ya saba au nane
umeokotwa ukiwa umetupwa eneo la mto Ng'ombe jirani na Alasco,
Mwananyamala jijini Dar.Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, kichanga hicho cha kiume kimekutwa eneo hilo leo asubuhi kikiwa kwenye mfuko wa Rambo.
Mtandao huu ulifanikiwa kuongea na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Makumbusho, Bi. Husna aliyetoa rai kwa wananchi wa eneo lake kutojihusisha na vitendo viovu kama hiki, huku akiwasihi kutumia njia za uzazi wa mpango kujikinga na matatizo kama hayo.
"Nina masikitiko makubwa kwa kitendo hiki, ni bora kichanga hiki kingeletwa serikalini tukilee kuliko kutupwa eneo hili. Kama wananchi mkishindwa kuvumilia bora mtumie uzazi wa mpango," alisema Bi. Husna huku akiahidi kufanya uchunguzi wa kina kumtafuta muhusika!