Sunday 5 November 2023

WALIMU WAIOMBA SERIKALI KUZUIA SHEREHE ZA SIKU YA MWALIMU

...
Rais wa Chama cha walimu Tanzania (CWT)Leah Ulaya

Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Wakati Uongozi wa Chama cha walimu Tanzania (CWT)ukiwa kwenye maandalizi ya Sherehe ya Siku ya Mwalimu inayotarajiwa kufanyika Desemba 13,2023 Jijini Mwanza,baadhi ya wanachama wake wametilia Shaka Sherehe hizo na kueleza kuwa ni batili . 

Wakizungumza na malunde Blog jijini Dodoma,
Wamesema jumla ya Bilioni Tano zinatarajiwa kutumika kukamilisha mkutano huo kwa mgawanyo wa posho ,vinywaji na chakula na kuwaacha walimu ambao kimsingi ndiyo wenye fedha wakifa maskini jambo linalotafsiriwa kuwa ni upigaji. 

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Iyumbu, Halmashauri ya Jiji la Dodoma Maxson Maboje ameeleza kuwa Sherehe hizo hazipaswi kuwepo kulingana na kanuni za chama hicho na kwamba zinafanyika kwa ajili ya viongozi kujinufaisha na kufuja fedha za wanachama. 

Mwalimu Maboje ametumia nafasi hiyo  kuiomba Serikali kuingilia kati kumaliza mgogoro ndani ya Chama hicho kwa maslahi ya walimu nchini kwani wamekuwa wakitumia muda mwingi kuzungumzia migogoro ya Chama kuliko kufanya kazi. 

Amesema kikanuni CWT kilipaswa kufanya Sherehe hizo kitaifa Oktoba 5,2023 lakini cha ajabu haikufanyika japo kuna baadhi ya maeneo walifanya ikiwemo wilaya ya Bukombe na kutaja sababu ya kutofanya hivyo ni kuandaa mazingira ya upigaji wa fedha za walimu. 

"Hii ni kutudharau sisi walimu, Madame Leah na Maganga wametudharau kwa kutosha, kama Sherehe zilitakiwa kufanyika Oktoba 5 mwaka huu iweje ifanyike Desemba, huu ni mwanya wa upigaji, kinachoniuma ni kuwa pesa hiyo inatokana na mishahara yetu, tunakuwa tunamhudumia Leah na Maganga badala ya kuhudumia Chama, " Amesema

Wakati haya yakiendelea ikumbukwe 
Septemba 25,2023 wakati wa mkutano wa dharula Rais wa Chama hicho Leah Ulaya aliionya Serikali kutoingilia Mambo yao
na kwamba Serikali inapaswa kujua  kuna uhuru wa vyama vya wafanyakazi, hivyo wana uhuru wa kukutana popote na kufanya kazi bila ya kuzuiliwa . 

Kitendo hicho kilitafsiriwa na baadhi ya walimu kama ni ukosefu wa nidhami na kuwa na Uhuru uliopitiliza hasa ikizingatiwa viongozi hao wa ngazi  ya juu wa CWT  walipaswa kuendelea na majukumu waliyopangiwa na Rais. 

Athman Kihinga ameeleza kuwa ifike wakati Serikali ione haja ya kuingilia matatizo yaliyopo ndani ya CWT kwani yakiendelea yanaweza kusababisha walimu kutokuwa na ari ya kufanya kazi kwa bidii na kushusha hadhi yao. 

"Nashindwa kuamini kwamba kelele zote tunazopiga kuomba msaada hazisikiki,tunatambua kuwa usajili wa CWT upo chini ya Serikali kwanini mamlaka husika inaogopa kutushughulikia au kutoa tamko lolote ili tujue tupo upande gani, " Anaeleza Kihinga
na kuongeza;

"Viongizi hawa wamekuwa wanatudharau walimu pamoja na Serikaki,nakumbuka Mnamo Januari 25, mwaka huu, Makamu wa Rais wa CWT, Dinna Mathaman,Katibu Mkuu wa CWT Maganga na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Wakuu wa Wilaya lakini Maganga na Ulaya hawakufika kuapa, hii ni dharau, "amesema 

Amesema,"uhuru ukizidi unakuwa mwenda wazimu,Viongozi hao wakati wenzao wakiapishwa, wao walionekana kuendelea na majukumu ya Chama jambo linalotufanya tukitafsiri kitendo hicho kuwa  wamegomea uteuzi wa Rais Samia, ni dharau," amesema

Amefafanua kuwa licha ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kufanya mchakato wa kufungua shauri la nidhamu dhidi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japhet Maganga baada ya kutorejea katika kituo chake cha kazi tangu alipotakiwa kufanya hivyo Oktoba Mosi mwaka huu hakuna mabadiliko yoyote. 

"Maganga ni Mwalimu Mwandamizi katika Manispaa ya Temeke, aliomba kibali cha kuazimwa kuitumikia CWT Agosti 2017 hadi Septemba 30, 2020, akaomba tena Juni 1, 2020 na kumalizika Septemba 30, 2023, na baadaye aliomba kibali hicho kwa mara ya tatu, tunaomba aachie madaraka kwa hiari aache kujidharirisha, " amesisitiza

Maganga alichaguliwa Desemba 2022 na Mkutano Mkuu wa CWT kuwa Katibu Mkuu akichukua nafasi ya Deus Seif
ambapo awali alikwa akitumikia nafasi ya Naibu Katibu Mkuu.






Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger