Sunday 5 November 2023

GGML ILIVYONG’ARA USIKU WA MADINI, YATWAA TUZO 2

...
Waziri wa Madini wa Malawi, Monica Chang'anamuno (kushoto) akimkabidhi tuzo ya mshindi wa jumla katika kipengele cha uhifadhi mazingira, afya na usalama mahala pa kazi, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong. Kulia ni Waziri wa Madini, Anthony Mavunde. Hafla hiyo iliyofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Madini wa Malawi, Monica Chang'anamuno (kushoto) akimkabidhi tuzo ya mshindi wa jumla katika kipengele cha Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR), Makamu Rais wa AngloGold Ashati- GGML anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo. Kulia ni Waziri wa Madini, Anthony Mavunde. Hafla hiyo iliyofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam
Waziri wa Madini wa Malawi, Monica Chang'anamuno (mwenye nguo nyekundu katikati) akiwa amebeba tuzo yake ya heshima ya ushiriki wa kongamano la Kimataifa la Madini na Uwekezaji Tanzania 2023. Wengine ni viongozi na wafanyakazi wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) walioshiriki katika hafla ya usikun wa madini.

Baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) wakifurahia ushindi wa kampuni hiyo iliyonyaku tuzo mbili katika hafla ya usiku wa madini iliyofanyikawiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Mchango wa Kampuni ya AngloGold Ashanti - Geita Gold Mining Limited (GGML) umeendelea kutambuliwa na wadau mbalimbali wa sekta ya madini kupitia Kongamano la Kimafaifa la Uwekezaji na Madini Tanzania 2023 kutokana na jitihada zake katika uwajibikaji kwa jamii pamoja na kuzingatia afya na usalama mahala pa kazi.

Hatua hiyo inatokana na Kampuni hiyo kushinda tuzo mbili ambazo ni mshindi wa jumla katika kipengele cha Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) pamoja na uhifadhi wa mazingira, afya na usalama kazini. Tuzo hizo zilizotolewa na Wizara ya Madini  zimeendelea kudhihirisha hadhi ya GGML kuwa mfano wa kuigwa katika masuala hayo ya afya na usalama kazini pamoja na kukuza uchumi wa Taifa.

Waziri wa Madini wa Serikali ya Malawi, Monica Chang'anamuno akiongozana na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde alikabidhi tuzo hizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong pamoja na Makamu Rais wa AngloGold Ashanti- GGML anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo.

Hafla hiyo iliyopewa jina la Usiku wa Madini, ilifanyika tarehe 25 Oktoba 2023 jijini Dar es salaam.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger