Wednesday 2 August 2023

WIKI YA UNYONYESHAJI YAZINDULIWA, DK. MOLLEL ATAKA AKINA MAMA KUEPUKA MSONGO WA MAWAZO MAZIWA YATOKE

...


Na Mariam Kagenda - Kagera
Akina mama wajawazito nchini wametakiwa kukaa katika mazingira yasiyowaletea msongo wa mawazo kwa  kipindi chote cha ujauzito na unyonyeshaji ili kufanya maziwa yatoke vizuri na mtoto kupata lishe bora na kukua vizuri. 

Wito huo umetolewa leo na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati wa uzinduzi wa wiki ya unyonyeshaji inayoadhimishwa kila mwaka kuanzia tarehe 1 hadi 8 kwenye ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mollel amesema kuwa, mama mjamzito anahitaji matunzo kwaajili ya lishe ya mtoto katika siku 1000 Yaani tangu kutungwa kwa mimba hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka miwili kwani ndio msingi bora wa ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili.

“Katika siku hizi 1000 madhara ya lishe duni hasa udumavu yanaathiri sana maendeleo ya rasilimali watu ya nchi, hivyo ni muhimu mtoto kunyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo na kuendelea kunyonyeshwa huku akipatiwa chakula cha nyongeza hadi anapotimiza miaka miwili au zaidi” ,mesema Dkt. Mollel

Aidha, Dkt. Mollel amesema, watoto wadogo na watu wazima wanapaswa kula lishe bora ili kuwaepusha na magonjwa yanayotokana na kutokula lishe isiyokamilika.

Amesema Kuna magonjwa mengi yanayotokana na kutokula lishe kamili ni vyema watoto na watu wazima kuzingatia hilo  pia lishe inayozidi inasababisha uzito uliozidi na hivyo kusababisha magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Figo na moyo.

Kuhusu takwimu za lishe Naibu Waziri alisema, asilimia ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee imeongezeka kutoka 58% mwaka 2018 hadi kufikia 64% mwaka 2022.

Vile vile takwimu ya watoto wanaonyonyeshwa ndani ya saa 1 baada ya kuzaliwa imeongezeka kutoka 53.5% mwaka 2018 hadi kufikia 70% mwaka 2022.

Hata hivyo Dkt. Mollel amewahimiza waajiri katika Sekta rasmi na zisizo rasmi na jamii kwa ujumla kuwasaidia wanawake waweze kunyonyesha watoto wao huku wakiendelea kufanya kazi na kuwakumbusha viongozi, wasimamizi, Wataalamu na watendaji kuendelea  kuelimisha umma kuhusu sheria ya kulinda haki za uzazi kwa wanawake pamoja na kuwahimiza waajiri kutenga sehemu maalum kwa ajili ya wafanyakazi wanawake wanaonyonyesha ili waweze kuendelea kufanya hivyo wakiwa kazini.

Naye Mwakilishi wa wadau wa Lishe nchini kutoka UNICEF Bwana  Patrick Codjia ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa dhamira ya dhati ya kuboresha lishe, afya na maisha ya wananchi wake ikiwa ni pamoja na watoto.

Wakati huo huo Mwakilishi kutoka Shirika la Kimatifa la Kazi(ILO) Bi. Chiku Semfuko ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kutoa muda kwa wanawake kwenda kunyonyesha pia kutenga vyumba maalumu vya kunyonyesha ili kuwapa nafasi wanaonyonyesha.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger