Thursday 31 August 2023

SERIKALI KUANDAA MWONGOZO WA UWIANO WA KIJINSIA ILI KUONDOA UKATILI

...


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju, akizungumza wakati wa Semina Elekezi ya Usambazaji wa Mwongozo wa Mafunzo ya uwiano wa Kijinsia na Ujumuishaji Jamii katika huduma za ustawi wa Jami kwa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Wizara za Kisekta, Taasisi za Umma na wadau yaliyofanyika leo Agosti 31,2023jijini Dodoma.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Nandera Mhando,akizungumza wakati wa Semina Elekezi ya Usambazaji wa Mwongozo wa Mafunzo ya uwiano wa Kijinsia na Ujumuishaji Jamii katika huduma za ustawi wa Jami kwa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Wizara za Kisekta, Taasisi za Umma na wadau yaliyofanyika leo Agosti 31,2023jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi huduma za Ustawi wa jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi.Subisya Kabuje ,akizungumza wakati wa Semina Elekezi ya Usambazaji wa Mwongozo wa Mafunzo ya uwiano wa Kijinsia na Ujumuishaji Jamii katika huduma za ustawi wa Jami kwa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Wizara za Kisekta, Taasisi za Umma na wadau yaliyofanyika leo Agosti 31,2023jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju (hayupo pichani) akizungumza wakati wa Semina Elekezi ya Usambazaji wa Mwongozo wa Mafunzo ya uwiano wa Kijinsia na Ujumuishaji Jamii katika huduma za ustawi wa Jami kwa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Wizara za Kisekta, Taasisi za Umma na wadau yaliyofanyika leo Agosti 31,2023jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Semina Elekezi ya Usambazaji wa Mwongozo wa Mafunzo ya uwiano wa Kijinsia na Ujumuishaji Jamii katika huduma za ustawi wa Jami kwa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Wizara za Kisekta, Taasisi za Umma na wadau yaliyofanyika leo Agosti 31,2023jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju,akiteta jambo na Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Nandera Mhando, mara baada ya kufungua Semina Elekezi ya Usambazaji wa Mwongozo wa Mafunzo ya uwiano wa Kijinsia na Ujumuishaji Jamii katika huduma za ustawi wa Jami kwa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Wizara za Kisekta, Taasisi za Umma na wadau yaliyofanyika leo Agosti 31,2023jijini Dodoma.

PICHA ZOTE NA ALEX SONNA



Na WMJJWM- Dodoma

Serikali imesema ili kuhakikisha kuna uwiano wa kijinsia katika upatikanaji wa huduma imeandaa mwongozo wa uwiano wa kijinsia ili makundi yote yashiriki katika maendeleo ya jamii lakini pia kuondoa ukatili.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju wakati akizungumza na Maafisa Ustawi wa Jamii wa Wizara za Kisekta, Taasisi za Umma na wadau kwenye mafunzo ya utoaji wa huduma kwa kuzingatia uwiano wa kijinsia ili kufikia kizazi cha usawa, yaliyofanyika jijini Dodoma Agosti 31,2023.

“Mwongozo huu umelenga kutekeleza makubaliano ambayo Tanzania imeridhia katika mikataba yake ya kimataifa lakini pia katiba yetu ya Tanzania inaelekeza kutoa huduma kwa watu wote bila ubaguzi wowote“ amesema Mpanju.

Wakili Mpanju amewasisitiza Maafisa Ustawi hao kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika mafunzo hayo ili maarifa yote yanayopatikana yatumike nchi nzima ili lengo la Serikali kuwa na jamii yenye usawa litimie.

Kwa upande wake, Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Nandera Mhando amesema mwongozo huo umeandaliwa kupitia hatua kadhaa ikiwemo vikao kadhaa na kufanyiwa majaribio kadhaa na wadau na kupitia mafunzo mbalimbali hadi kufikia hatua ya ukamilishaji.

“Malengo ya Semina hii ni kutoa uenezi wa mwongozo huu kwa maafisa ustawi ili utumike nchi nzima na ukazibe mapengo yote yaliyokuwepo kwenye uwiano wa kijinsia nchi nzima” amesema Dkt. Nandera.

Naye Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Subisya Kabuje amesema mwongozo huo utafanikiwa zaidi endapo utasambazwa kwa Maafisa Ustawi wote kutoka mikoa yote na Halmashauri zote na kusaidia kutatua changaoto zilizokuwepo.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Shirika la PACT Tanzania Flora Nyagawa amesema Shirika hilo litaendelea kushirikiana kikamilifu na Wizara kuhakikisha afua zote zinatekelezwa ili kuwa na Taifa lenye uwiano wa jinsia.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger