Saturday 26 August 2023

WAZIRI MABULA AWASILISHA VIPAUMBELE VYA SEKTA YA ARDHI KATIKA SEMINA YA MA-RC NA MA-RAS KIBAHA

...
Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao cha wakuu wa mikoa na makatibu tawala kinachoendelea katika chuo cha uongozi cha Mwalimu J K Nyerere kibaha mkoani Pwani tarehe 26 Agosti 2023.

*******************

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maedeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amewasilisha vipaumbele vya wizara yake kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika semina ya uongozi katika Chuo cha Mwalimu Nyerere kilichopo kibaha mkoani Pwani.

Katika wasilisho lake leo tarehe 26 Agosti 202, Waziri Mabula alizungumzia masuala ya ukusanyaji mapato yatokanayo na sekta ya ardhi, mipango miji pamoja na maeneo ya uwekezaji ambayo yote wakuu hao wa mikoa wanalo jukumu la kusimamia kwenye mikoa yao.

Dkt Mabula aliwataka wakuu wa mikoa kusaidia katika kuongeza hamasa katika suala la ukusanyaji mapato ya serikali yatokanayo na sekta ya ardhi.

"Niwaombe mkasimamie mikakati ya ukusanyaji maduhuli hayo ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha wananchi waliopo katika maeneo kulipa kodi ya pango la ardhi.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula Rais Samia alitoa msamaha wa riba ya kodi kwa miezi 10 mafanikio yalionekana japo si kwa kiwango kilicho tarajiwa.

Pia aliwataka wakuu wa mikoa kuzisimamia halmashauri katika kutenga fedha katika bajeti za maendeleo ya sekta ya ardhi ili kuhakikisha ardhi inapangwa, kupimwa na kumilikisjwa.

"Halmashauri zitambue kuwa jukumu hilo bado ni la kwao na wanahitaji kuendelea kushiriki kikamilifu katika kutenga fedha ili kutekeleza majukumu yao na kuwezesha watumishi waliopo katika halmashauri kufanya kazi" alisema Dkt Mabula.

Sehemu ya washiriki semina ya uongozi inayofanyika katika chuo cha uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kibaha mkoa wa Pwani.
Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao cha wakuu wa mikoa na makatibu tawala kinachoendelea katika chuo cha uongozi cha Mwalimu J K Nyerere kibaha mkoani Pwani tarehe 26 Agosti 2023.

Baadhi ya wakuu wa mikoa wakifuatilia wasilisho la Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula wakati wa semina ya uongozi inayofanyika katika chuo cha uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kibaha mkoa wa Pwani. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger