Wednesday 28 June 2023

WATOTO WAFARIKI DUNIA KWA KUPONDWA MAWE

...

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Watoto wawili wa familia moja wamekutwa wamefariki dunia  baada ya kufukiwa/kupondwa na mawe wakati wakichimba mchanga katika eneo la Marahara kijiji cha magata kata ya Karutanga wilayani Muleba mkoani Kagera .

Diwani wa Kata ya Magata Karutanga  Alhaji Yakubu Mahamudu amesema kuwa watoto hao  walipotea  Juni 26 ,2023 na walitafutwa maeneo yote hawakuweza kupatikana na June 27 watoto hao walipatikana wakiwa tayari wamefariki dunia baada ya kufukiwa  na mawe wakati wakichimba mchanga.

Alhaji Yakubu amewataja watoto hao kuwa ni Samsoni Eliud mwenye umri wa miaka 13 na Emmanuel Eliud mwenye umri wa miaka 10 ambapo wote walikuwa wanafunzi wa shule ya Msingi Magata   na kuongeza kuwa watoto hao waliterekezwa na baba yao  mzazi na kubaki na mama yao pekee .

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga  amefika katika eneo hilo ambapo amepiga marufuku na kuzuia mtu yoyote yule kufanya shughuli za uchimbaji wa mchanga kwani eneo hilo sio salama na kuagiza kukaguliwa maeneo yote ya uchimbaji wa mchanga katika wilaya hiyo ili kudhibiti maafa yasiendelee kutokea.

Nao baadhi ya wananchi ambao ni Ashimu Salimu na Godfrey Joel wamesikitishwa na tukio hilo na kuwahimiza wazazi kuendelea kuwalea watoto wao katika maadili mema na kuwahimiza wanaume kutowatelekeza watoto.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger