Saturday 24 June 2023

MBUNGE JIMBO LA LUPEMBE AOMBA SERIKALI KUANZA UJENZI WA LAMI KUTOKA KIBENA LUPEMBE HADI MADEKE

...
 

Mbunge wa Jimbo la  Lupembe mkoa wa Njombe Edwin Swale ameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa barabara ya Lami kutoka Kibena Lupembe hadi Madeke ikiwa ni maagizo ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.


Swale ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia bajeti ya serikali 2023/24 ambapo amesema kufufuliwa kwa mashamba ya chai jimboni kwake kunatakiwa kwenda sambamba na kuanza kwa ujenzi wa barabara hiyo muhimu inayo unganisha Mkoa wa Njombe na Morogoro.


Amesema kama serikali haina uwezo wa kuajiri watu wote wanaingia kwenye soko la ajira ni vyema ukafanyika mpango wa kufufua viwanda kikiwemo Kiwanda cha Maziwa cha Njombe ,Kiwanda cha Olivado na kisha kuimarisha viwanda vya chai vinavyosuasua mkoani Njombe ili kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wengi.


Swale amesema takwimu zilizopo zinaonyesha watu milioni moja huingia kwenye soko la ajira kila mwaka ili hali ilani ya chama imeahidi kutoa ajira mil 8 kila mwaka jambo ambalo linashindikana na kuishia kuajiri watu elfu 70 tu hivyo serikali ichukue hatua za lazima za kukabiliana na changamoto ya ajira kwa kufufua sekta ya viwanda.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger