Tuesday 20 June 2023

WAFANYABIASHARA MAARUFU 'JAMBO - JAMUKAYA' GILITU WANG'AKA SAKATA LA BANDARI

...
Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania Salum Mbuzi maarufu Jambo/ Jamukaya akizungumza wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania Salum Mbuzi maarufu Jambo/ Jamukaya amesema wafanyabiashara nchini ndiyo waathirika wakubwa wa Bandari ya Dar es salaam kutokana mizigo yao kuchukua muda mrefu mpaka siku 16 akisisitiza kuwa anatamani kama mkataba wa uwekezaji katika Bandari wangeruhusiwa kuusaini wangekuwa tayari wameshausaini.

Jambo ametoa kauli hiyo leo Jumanne Juni 20,2023 wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga.


“Sisi wafanyabiashara tunaijua bandari kuliko mtu yeyote yule. Mngeturuhusu sisi tungeenda kuusaini huo Mkataba mara moja. Huu siyo mkataba wa kwanza katika Bandari, huu ni mkataba uliofanyiwa marekebisho baada ya wawekezaji waliopita”,
 amesema.

“Wafanyabiashara tunauhitaji huu mkataba huu kuliko kitu chochote….Nawashangaa hao wanaoshangaa mkataba wa uwekezaji. Mimi ningeomba nyinyi serikali muangalie hao wanaopinga ni akina nani. Wafanyabiashara tunataka makontena yetu yawe yanatoka haraka bandarini, tuyachukue haraka. Tunatumia gharama kubwa kucheleweshewa mizigo yetu bandarini. Hizi gharama sasa zinatosha”,amesema Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Jambo Food Products.

“Sisi wafanyabiashara msihusishe na wanasiasa, wanasiasa hawana mizigo bandarini, Sisi wenye mizigo tunataka uwekezaji katika bandari, kwani mizigo yetu inachukua mpaka siku 16”,ameongeza Jambo/Jamukaya.

Kwa upande wake mfanyabiashara maarufu Gilitu Makula amesema amefuatilia na kubaini kuwa wengi wanaopinga uwekezaji katika bandari hawajawahi hata kuwa na kontena bandarini.


“Usumbufu uliopo bandarini ni mkubwa sana. Mkataba huu utasaidia sana mizigo itoke haraka. Hakuna mtu anayetaka kuuza nchi, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kuleta fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ni mzalendo. Hawa wanaopinga ni kutafuta umaarufu tu wa kisiasa”,ameongeza Gilitu.
Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania Salum Mbuzi maarufu Jambo/ Jamukaya akizungumza wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga.  Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania Salum Mbuzi maarufu Jambo/ Jamukaya akizungumza wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga. 

Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania Gilitu Makula akizungumza wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga. 
Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania Gilitu Makula akizungumza wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga. 

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
 
Soma pia



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger