Friday, 30 June 2023

UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA WANAOHUDUMIWA NA MTAMBO WA RUVU JUU


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia wateja na Wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu juu kuwa, kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa muda wa saa 24 kwa siku ya Jumamosi 1/07/2023 kuanzia saa 12 jioni hadi Jumapili 02/07/2023 saa 12 jioni.

Sababu: Kuruhusu matengenezo za pampu za kusukuma majisafi kutoka mtamboni kwenda kwa wananchi.

Maeneo yatakayoathirika ni;
Ruvu darajani, Ruvu JKT, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Mile 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Pichandege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi inn, Mbezi, Kimara,Tabata, Kinyerezi, Kisukuru, Msigani, Maramba mawili, Tabata, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, pamoja na Ubungo

Tafadhali kumbuka kuhifadhi maji ili kuwa na hifadhi ya kutosha kipindi chote cha matengenezo.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au
0735 202 121(WhatsApp tu)

Tovuti: www.dawasa.go.tz

Mitandao ya kijamii.

Facebook: https://ift.tt/7953Guh

Instagram: https://ift.tt/pPN7GR2

Twitter: https://twitter.com/dawasatz?s=08

YouTube: https://youtube.com/channel/UCCVyHKIvUwDFG1tUyWhd7fQ

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Share:

KUMEKUCHA MGODI WA ALMASI MWADUI....WAZIRI BITEKO AAGIZA UZALISHAJI UANZE BWAWA JIPYA LA TOPE LIMEJENGWA


Mhandisi Mwelekezi wa Mradi wa Ujenzi wa bwawa la tope katika mgodi wa Williamson Diamond Limited, Mhandisi Anael Macha akimuonesha eneo la bwawa jipya katika Mgodi wa Mwadui Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ameagiza Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga kuanza shughuli za Uzalishaji kuanzia Julai 15 baada ya kuridhishwa na hatua mbalimbali zilizochukuliwa baada ya kingo za Bwawa la Maji Tope kubomoka.

Novemba 7,2022 Bwawa la tope la mgodini katika mgodi wa Mwadui lilipasuka na kuharibu makazi na mashamba ya wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze vilivyopo katika Kata ya Mwadui Luhumbo  wilayani Kishapu kwa kufunikwa na tope.


Akiwa katika Mgodi huo leo Ijumaa Juni 30, 2023 kwenye ziara yake ya kikazi, Waziri Dkt. Biteko ametoa agizo la uzalishaji kuanza baada ya kujionea hali halisi ya ujenzi wa bwawa la kuhifadhi tope laini la mgodini ambalo ujenzi wake umefikia 97% na bwawa la maji la wananchi la Ng’wang’holo ambalo ujenzi wake umefikia 98% pamoja asilimia 98% ya ulipaji fidia.
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko

“Ulipaji wa fidia mbalimbali umefikia asilimia 96%. Kulikuwa na malalamiko 66 yameshashughulikiwa 61 bado matano ambapo tunaamini wiki inayokuja tutakuwa watakuwa wameyamaliza. Nimefurahi kuwa ujenzi wa bwawa la maji tope umekamilika tena limejengwa kwa Engineering tofauti na lililopasuka. Tutatoa vibali wiki inayokuja ili mgodi huu uanze mara moja”,amesema Waziri Biteko.

“Nachukua nafasi hii kumuomba Mhe. Mkuu wa Mkoa pengine tarehe 15 Julai 2023 kama ana nafasi aje ashuhudie kuanza kwa uzalishaji wa mgodi huu. Madini tunayoyategemea sana ni dhahabu aina ya pili tunayoyategemea kwa mapato ni almasi sasa kwa kipindi cha miezi sita tulisimama kwa sababu mara ya mwisho tumeenda sokoni ilikuwa Desemba hatujawahi kwenda tena kwa hiyo tumepotea sokoni kwa muda mrefu, tunatamani huu mgodi uanze mara moja ili turudishe mapato tuliyokuwa tunayapata lakini muhimu sana ajira za Watanzania ambao wapo kwenye mgodi huu zisipotee”,ameeleza Mhe. Biteko.

Ametoa kwa wito kwa mgodi huo uanze uzalishaji mara moja lakini waanze baada ya kuwa wamekamilisha taratibu zote za kuhakikisha kwamba linakuwa na bwawa imara.
Muonekano wa sehemu ya bwawa jipya katika Mgodi wa Mwadui

“Tunataka kuhakikisha kwamba tunakuwa na bwawa imara zaidi kuliko lililokuwepo na watuandikie kabisa commitment letter kwamba hili bwawa tunathibitisha na utalaamu halitaweza kuleta madhara, likileta madhara tujue tunawashughulikia kwa namna gani”,amesema Waziri Biteko.


“Namshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alichukua muda kukutana na Mtendaji Mkuu wa Williamson Diamond Limited,alieleza matatizo yaliyopo katika Mgodi na Mhe. Rais akaahidi kwamba sisi tuyasimamie kwa haraka tuyamalize ili mgodi uanze kufanya kazi. Nataka nimhakikishie Mhe. Rais kwamba maelekezo yake tunayafanyia kazi na huu mgodi sasa unarudi kwenye Operation na sisi Wizara ya Madini ndiyo wasimamizi wa sekta hii tutahakikisha kila aina ya uchimbaji wa kufuata sheria na taratibu ili watu wabaki salama na fedha tuzipate, ajira zibaki, kodi tupate vyote vinazingatiwa”,ameongeza.


Amewashukuru wananchi kwa utulivu wao pamoja na Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, serikali ya Mkoa , Wilaya kwa usimamizi wa karibu wa jambo hilo vinginevyo lingezua matatizo mengi na mijadala mingi.


Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda amesema wapo tayari kuanza uzalishaji muda wowote wanachosubiri ni kibali tu.
“Ujenzi wa bwawa la maji ya wananchi Ng’wang’holo umefikia asilimia 98, bwawa la kuhifadhi tope laini la mgodini asilimia 97 na 96% ya utoaji fidia mbalimbali kwa wananchi ambazo ni mali, vitega uchumi, chakula na kodi kwa walioathirika kwenye makazi. Makazi 47 yatajengwa kuanzia mwezi Julai 2023 kipindi cha miezi 6”,amesema Mhandisi Mwenda.


“Baada ya kutokea kwa tukio hili taharuki ilitoke lakini serikali imekuwa karibu nasi kulishughulikia, na tunashukuru pia wananchi wamekuwa watulivu. Tangu bwawa lipasuke hatukuwahi kufanya uzalishaji, kwa kweli hili ni pigo kwetu na wafanyakazi wetu. Tunashukuru sana shughuli za uzalishaji kurejea na tunaahidi hadi kufikia Julai 15 tutakuwa tumeanza kufanya kazi”,amesema Mhandisi Mwenda.


Naye Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Modest Mkude wamesema kuanza kwa uzalishaji katika mgodi huo kutasaidia kurudisha ajira na mapato yaliyokuwa yamepotea huku wakiomba wananchi waendeleee kutoa ushirikiano ili amani na mshikamano uendelee kuwepo.


Katibu wa Chama cha Wachimbaji wa Wadogo wa Madini Mkoa wa Shinyanga (SHIREMA), Gregory Kigosi wameuomba mgodi wa Almasi Mwadui uwapatie kituo cha maji (DP) katika mgodi wa Ng’wang’holo ambapo mgodi huo umekubali ombi hilo.
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza katika bwawa jipya la tope laini la mgodini katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga leo Ijumaa Juni 30,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza katika bwawa jipya la tope laini la mgodini katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga leo Ijumaa Juni 30,2023.
Mhandisi Mwelekezi wa Mradi wa Ujenzi wa bwawa la tope katika mgodi wa Williamson Diamond Limited, Mhandisi Anael Macha akimuonesha eneo la bwawa jipya katika Mgodi wa Mwadui Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza katika bwawa jipya la tope laini la mgodini katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga leo Ijumaa Juni 30,2023.
Muonekano wa sehemu bwawa jipya la tope laini la mgodini katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga leo Ijumaa Juni 30,2023.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda  ( wa kwanza kushoto) akimwelezea Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kuhusu ujenzi wa bwawa jipya la tope laini la mgodini katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) 
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza katika bwawa jipya la tope laini la mgodini katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga leo Ijumaa Juni 30,2023.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda akimwelezea Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kuhusu ujenzi wa bwawa jipya la tope laini la mgodini katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) 
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda  (katikati) akimwelezea Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kuhusu ujenzi wa bwawa jipya la tope laini la mgodini katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) 


Mbunge wa Kishapu Mhe. Boniphace Butondo akizungumza wakati Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akitembelea Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Modest Mkude akizungumza wakati Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akitembelea Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) 
Katibu wa Chama cha Wachimbaji wa Wadogo wa Madini Mkoa wa Shinyanga (SHIREMA), Gregory Kigosi  akizungumza wakati Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akitembelea Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) 
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu akizungumza wakati Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akitembelea Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) 
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akiangalia bwawa la wananchi Ng'wang'holo katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga leo Ijumaa Juni 30,2023.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda akimwelezea Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kuhusu ujenzi bwawa la wananchi Ng'wang'holo katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited)

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda  akimwelezea Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kuhusu ujenzi sehemu ya kuchotea maji katika bwawa la wananchi Ng'wang'holo katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited)
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda  akimwelezea Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kuhusu ujenzi sehemu ya kuchotea maji katika bwawa la wananchi Ng'wang'holo katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited)
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda  akimwelezea Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kuhusu ujenzi sehemu ya kuchotea maji katika bwawa la wananchi Ng'wang'holo katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited)
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza katika eneo la ujenzi sehemu ya kuchotea maji katika bwawa la wananchi Ng'wang'holo katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited)
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akiondoka katika eneo la ujenzi sehemu ya kuchotea maji katika bwawa la wananchi Ng'wang'holo katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited)
Sehemu ya bwawa la wananchi Ng'wang'holo katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited)
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda  akimuonesha Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kitalu cha kuoteshea miti katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited).

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog



Share:

CHEZA MIZUNGUKO 100 UPATE 50 YA BURE MERIDIANBET KASINO

Hii ni promosheni nyingine kutoka kasino ya mtandaoni ya Meridianbet haswa sloti ya God of Coins iliyotengenezwa na Expanse Studios moja ya wataalam wa michezo ya kasino ya mtandaoni.


Meridianbet wanatoa nafasi nyingine kwa wachezaji wa sloti na michezo ya kasino ya mtandaoni, unaambiwa hivi ukicheza mizunguko 100 kwenye mchezo wa God of Coins unapewa zawadi ya mizunguko 50 ya bure haijalishi ulicheza ukashinda au kupoteza kikubwa uwe umekamilisha mizunguko 100 ya kucheza kasino ya mtandaoni.


Promosheni hii imeanza Juni 27 na itadumu mpaka Julai 15, 2023 na ni kwa wateja wote waliojisajili na Meridianbet, endapo hujajisajili bonyeza hapa kujisajili kisha utapewa zawadi ya mizunguko ya bure kucheza kasino ya mtandaoni.

Fahamu Kuhusu God of Coins

Sloti ya God of Coins inawalenga wapenzi kindakindaki wa historia ya kale, kasino ya mtandaoni hii inawasafirisha wachezaji wake hadi ulimwengu wa Misri ya kale kupitia picha zake za kuvutia na nyimbo zinazoendana na zama za enzi hizo.

Ikiwa na mpangilio maalum wa mistari ya 4x5, God of Coins Sloti ina ishara za alama 8 ikiwa ni pamoja na alama ya WILD. Katika mistari 20 ya malipo una uwezo wa kushinda mpaka mara 1000 ya dau lako katika kila mzunguko, mchezo huu wa kasino ya mtandaoni unawafanya wachezaji kufurahia na kucheza kwa muda mrefu bila kuchoka. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet sasa!


Share:

MAMA WA WATOTO WATATU AOLEWA NA SHABABI LA KISIWANI



Rafiki yangu wa karibu ambaye tumekuwa tukicheza naye kuanzia utotoni mwangu ndiye aliyenifichulia siri kubwa juu yangu na kunifanya nipate mume aliye kubali kunioa pamoja na kuwa na watoto watatu ambao nliwazaa nikiwa nje kabla ya mimi kufahamiana nayeye , ni daktari BAKONGWA mwenye nambari za whatsapp +243990627777 na tovuti zake  https://bakongwadoctors.com ambaye alinifungia kidawa na kunitumia huku niliko baaada ya kukitumia kwa siku tatu tayari nilikuwa nimejipata na kumuona mume wangu.

Mwanzoni mwangu ilikuwa ni shida sana hakuna mwanaume ambaye alikubali kuishi na mimi pamoja na watoto wangu ambao yeye hakuwazaa lakini kwa Leornard kwake hilo halikuwa ni shida wala changamoto kabisa , aliliona ni la kawaida tu na watoto wangu akawalelea.Awamu ya kwanza nilipata mapacha ambao nilijifunguwa mara tu ya kumaliza masomo yangu ya chuo kikuu huko iringa lakini kwa bahati mbaya mwanaume yule alinitelekeza hakuwahi kujuwa lolote kuhusu watoto wala kuhusu mimi tea.

Nilipambana kivyangu nikalea watoto wakakua nikawa mama mwenye nyumba kila jukumu ni langu walipofikisha umri wa miaka minne nikapata mwanaume mwingine ambaye alinilaghai akasema maneno mazuri na kuahidi kunilelea wanangu ni kamuamini nikampa nafasi lakini huyo pia hakuniacha vizuri nilipomwambia tu kuwa na mimba yake alianza kubadilika hakuwa kama yeye yule wa zamani.


 Nilipojifungua ndipo alikatisha kila shughuli na hata ahadi za kunioa ziliiishia palepale akawa ni mzazi mwenzangu wa kusaidiana kumlea mwanaye tu lakini ahadi za ndoa zote zikapotea moja kwa moja.


Nilijua kuwa sitoweza kamwe kupata mwanaume ambaye atakubali kunioa kwa idadi ile ya watoto ambayo nilikuwa nayo, nilivurugika sana kiakili nikaweka nguvu kubwa kwenye ulezi wa wanangu na majukumu ya kila siku umri wangu ulizidi kusonga mbele nikawa najiondolea na nafasi ya kuwa kwenye ndoa kwanza kwa idadi ya watoto niliozaa nje na kwa umri wangu ulivyosegea na kuwa mkubwa zaidi.


Kujipa moyo na kushindwa kupoteza matumaini kukawa ni ngumu sana kwa hali ambayo nilikuwa nayo , niliporudi nyumbani kipindi fulani kwa wazazi kuwasalimu kwakweli nawao waliliona hilo wakijua wazi hakuna mwanaume ambaye anaweza kubali kunioa kwa idadi ya watoto ambao sikuwa nimezaa naye.

 Nikashauriwa na wazazi niweke nguvu nyingi kwenye maombi ili angalau mmoja wa wale wanaume walionizalisha ajitokeze na kunioa badala ya kuishia kuwa mzazi mwenzao.

Hakuna lililotokea jipya yote yalikuwa ya kipindi kilekile hakuna alyekubali kunioa sio hata wale walionizalisha hakuwepo wa kunioa pamoj a na elimu yangu ya juu ambayo nilikuwa nayo.


Rafiki yangu huyo wa mufindi ambaye kwa bahati yeye alikuwa akiishi nje ya nchi ndiye aliyenipa mwanga na kumfahamu daktari , nilipomtafuta daktari na kuongea naye yeye akanisikiliza kwa umakini na kunipa maelekezo juu ya dawa atakayoituma kwangu nilipoipokea na kumaliza kuitumia masaa ishirini na saba , wanaume walianza kujitokeza watatu ambao wote walikuja kwa ahadi za kunioa awamu hii nilisema sitompa mtu mwili wangu mpaka anioe.


Sasa ikawa ni zamu yangu kujichagulia niliyempenda shababi wa kisiwani huko unguja na yeye hakutaka kuchelewesha lolote tukafanya maandalizi ya ndoa ya mkeka na kisha tukawa baba na mama kwa msaada wa daktari asante sana bakongwa sasa nimeolewa pamoja na idadi ya watoto ambao nilikuwa nao nje.



Share:

SERIKALI WADAU WAIPONGEZA BENKI YA CRDB KUKUSANYA SH 700 BILIONI KUWAWEZESHA WAJASIRIAMALI NCHINI


Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Abdalla Hussein Kombo (katikati), Afisa Biashara Mkuu Benki ya CRDB, Boma Raballa (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati Benki ya CRDB, Bonaventura Paul (wapili kulia), Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Benki ya CRDB, Yolanda Uriyo (wakwanza kushoto), na Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara, Agnes Kisinini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wateja wajasiriamali wa Benki hiyo wakati wa hafla maalum ya kuadhimisha Siku ya Wajasiriamali Duniani iliyoandaliwa iliyofanyika 27 Juni 2023 Makao Makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam.

====== ===== =====


Serikali imeipongeza Benki ya CRDB kwa kukusanya zaidi ya Sh700 bilioni za kuwakopesha wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini katika maadhimisho ya Siku ya Wajasiriamali Duniani (World MSME Day).


Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Abdalla Hussein Kombo aliyekuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo akisema jitihada zinazofanywa na Benki hiyo zinaonyesha dhamira ya dhati iliyonayo katika kuchochea sekta ya ujasiriamali nchini.


“Takwimu zinaonyesha ni asilimia 96 ya biashara nchini ni biashara ndogo na za kati, ambapo watu milioni 24 wameajiriwa katika sekta hii. Hivyo jitihada hizi zinazofanywa na Benki ya CRDB ni muhimu sana katika kuboresha sekta hii ambayo inatoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Taifa letu,” amesema Kombo.
Waziri Kombo amebainisha kuwa, sekta ya ujasiriamali inachangia asilimia 33 kwenye pato la Taifa yaani Gross Domestic Product (GDP). Hii ikimaanisha kuwa, katika kila shilingi 100 basi shilingi 33 ambazo ni sawa na theluthi moja, zinachangiwa na biashara ndogo.


Benki ya CRDB inatajwa kuwa kinara katika uwezeshaji wa wajasiriamali nchini huku mwaka huu ikitunikiwa tuzo ya Benki Bora kwa uwezeshaji wa Wajasiriamali na jarida maarafu la nchini marekani la “Global Finance”.
Kwa upande wa Zanzibar, Waziri Kombo amesema Serikali inajivunia ushirikiano na Benki ya CRDB kupitia programu ya “INUKA NA UCHUMI WA BLUU” kuwainua wajasiriamaili ambapo shilingi bilioni 60 zimetengwa.


Programu hiyo ambayo inatoa ufadhili wa mitaji kwa wajasiriamali bila riba inatajwa kuwa moja ya programu bunifu zenye msukumo mkubwa wa kuwainua wajasiriamali nchini. “Wizara yangu ni miongoni mwa sekta zilizonufaika na mikopo inayotolewa na Benki ya CRDB kupitia programu ya INUKA kwani imetengewa Sh36.5 bilioni kila mwaka kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo wanaojihusisha na fursa zilizopo kwenye uchumi wa buluu. Kwa kweli naipongeza sana Benki ya CRDB kwa juhudi hizi muhimu kwa uchumi wa Taifa na maendeleo ya watu wetu,” amesema Waziri Kombo.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa Benki ya CRDB inatambua na kuthamini shughuli za kijasiriamali katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla jambo ambalo limeifanya benki hiyo kushirikiana na wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi katika kuboresha sekta hiyo.


“Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita wakati dunia ikishuhudia misukosuko ya kiuchumi iliyochangiwa na janga la UVIKO-19 na vita vya Ukraine, Benki yetu kwa kushirikiana na washirika wa kimataifa ilikusanya zaidi ya Sh 700 bilioni ambazo zinaendelea kusaidia biashara za wajasiriamali ambazo nyingi ziliziathirika kwa kiasi kikubwa,” amesema Raballa.
Katika kipindi hicho, Raballa amesema wameshirikiana na wadau wa ndani na kimataifa likiwamo Shirika la Fedha la Ufaransa Proparco, Shirika la Fedha Kimataifa (IFC), Mashirika ya Marekani ya Maendeleo ya Kimataifa USAID na DFC, Benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya, Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), na Mfuko wa Dhamana Afrika (AGF) kukusanya kiasi hicho cha fedha.


Raballa amesema ili sekta ya ujasiriamali iweze kutoa mchango wake kikamilifu katika kukuza uchumi wa Taifa, kunahitajika huduma na mifumo shirikishi itakayowasaidia wajasiriamali kufanikisha malengo yao.


Kwa kutambua hilo, Benki ya CRDB ilikuwa benki ya kwanza nchini kuanzisha huduma kwa ajili ya wajasiriamali mwaka 2005 ambapo tokea kipindi hicho imekuwa ikiwekeza kwa kiasi kikubwa katika bidhaa na huduma bunifu za wajasiriamli.


Huduma na bidhaa hizo zinajumuisha akaunti maalumu ya Hodari ambayo ni mahsusi kwa ajili ya wajasiriamali, mifumo ya kidijitali ya usimamizi wa biashara, mafunzo ya ujasiriamali ndani na nje ya nchi, na kutoa mikopo ya mtaji kwa wajasiriamali walio katika sekta tofauti za uchumi.


“Najivunia kuwajulisha kuwa kupitia jitihada hizi, Benki yetu imekuwa kinara katika kuwawezesha wajasiriamali kwani hadi Mei 2023 tulikuwa tumetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya Sh3.4 trilioni kwa wajasiriamali zaidi ya 200,000, na wengine zaidi ya 50,000 wakinufaika kwa mafunzo tuliyoyatoa,” amesema Raballa.


Raballa amesema hivi karibuni Benki ya CRDB kupitia Taasisi yake ya CRDB Bank Foundation imeendelea kupanua wigo wa kuwainua wajasiriamali wadogo kupitia programu endelevu ya “IMBEJU” inayolenga kufanya uwezeshaji wa biashara changa na wajasiriamali vijana na wanawake kupitia mafunzo, ushauri, na mitaji wezeshi.

Akizungumza kwenye mjadala wa maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Mwajuma Hamza ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa mdau mkubwa wa sekta ya ujasiriamali hususan kwa kuweka mbele uwezeshaji wa wajasiriamali wanawake kupitia CRDB Malkia inayojumuisha Akaunti ya Malkia na Mikopo maalum ya kinamama ijulikanayo kama WAFI (Women Access to Finance Initiatives), huku akibainisha wanawake wajasiriamali wengi wameweza kunufaika na Sh 700 bilioni zilizokusanywa na Benki ya CRDB kusaidia wajasiriamali baada ya changamoto za janga la UVIKO-19.


“TWCC ni chama chenye matawi kila wilaya nchini. Tunashirikiana na wadau kusaidia kutatua changamoto zilizopo. Benki ya CRDB ni miongoni mwa wadau wetu muhimu kwani, licha ya kutukopesha ili nasi tuwawezeshe wanachama wetu, wao ni walezi wazuri. Benki ya CRDB inazo programu nyingi zinazomlenga mwanamke ambaye akizitumia fursa hizo inakuwa rahisi kwake kuboresha biashara yake," amesema Mwajuma.




Share:

KUELEKEA SIKU YA USHIRIKA DUNIANI JULAI MOSI BONANZA LAFANYIKA



Wachezaji wa Timu za Mpira wa Pete wakichuano vikali ambapo Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) kimeibuka na ushindi wa kishindo wa magoli 30-10 dhidi ya TCDC mchezo uliofanyika katika uwanja wa Chuo cha Uhazini mkoani Tabora kuelekea maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani Julai Mosi mwaka huu.



Na.Alex Sonna-TABORA KUELEKEA Maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani Julai mosi mwaka 2023 kumefanyika michezo mbalimbali katika Viwanja vya Chuo cha Utumishi wa Umma.

Michezo ambayo imepigwa ni soka,netiboli kuvuta kamba na kukimbiza Kuku ikiwakutanisha wafanyakazi na watumishi wa ushirika na Shirikisho la vyama vya Ushirika.

Mwenyekiti wa Kamati ya ndogo ya Michezo,Burudani na Matangazo ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya ushirika Duniani,Ibrahim Kadudu amesema michezo hiyo ilifanyika katika uwanja wa Chuo cha Uhazini mkoani Tabora.

Amesema timu zilizoshiriki michezo hiyo ikijumuisha wachezaji kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Sheila la Ukaguzi la Vyama vya Ushirika (COASCO) na Chuo cha Ushirika Moshi (MoCU).

Amesema michezo hiyo ni maalum kwa ajili ya kuadhimisha siku ya ushirika inayotarajiwa kufanyika Julai mosi mwaka huu.

"Ushirika asili yake ni mashirikino na michezo yote asili yake ni mashirikino hakuna mchezo ambao unaweza kuchezwa na mtu mmoja inachezwa na zaidi ya moja,"amesema Mwenyekiti huyo.

Amesema faida zinazopatikana ni pamoja na mahusiano na uchumi kwa watu mbalimbali.

"Niwasisitize wanaushirika michezo ni eneo la muhimu kuimarisha afya na watumishi tuendelee kufanya mazoezi hata baada ya bonanza hili,"amesema Bw.Kadudu

Pia ametoa rai kwa wachezaji iwe chachu kuendeleza kile ambacho wamekianzisha ili kuimarisha afya.

Pamoja na mambo mengine washindi walioibuka kukimbia kwenye gunia no Issa Ahamed na Agustino Abdul Karim kutoka TCDC, kukimbia kuku Issa ameendelea kubaki mshindi akifuatiwa na Raphael. Nae Adolf Ndunguru akifuatiwa na Noel Steven washindi kipindi cha pili wakitokea TCDC.

Aidha, mchezo wa mpora wa Pete Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) ilishambulia magoli 30 dhidi ya TCDC Kwa goli 10. Mgeni Rasmi Mrajis Msaidizi wa Geita Doreen Mwanri ametoa zawadi ya mipira Kwa timu za Netiboli kuunga mkono juhudi za wanamichezo.


Wachezaji wa Timu za Mpira wa Pete wakichuano vikali ambapo Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) kimeibuka na ushindi wa kishindo wa magoli 30-10 dhidi ya TCDC mchezo uliofanyika katika uwanja wa Chuo cha Uhazini mkoani Tabora kuelekea maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani Julai Mosi mwaka huu.


Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Michezo,Burudani na Matangazo ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya ushirika Duniani,Bw.Ibrahim Kadudu,akizungumza wakati wa Michezo ya Soka,Netiboli, kuvuta kamba na kukimbiza Kuku michezo hiyo ikijumuisha wachezaji kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Sheila la Ukaguzi la Vyama vya Ushirika (COASCO) na Chuo cha Ushirika Moshi (MoCU) lililofanyika katika uwanja wa Chuo cha Uhazini mkoani Tabora kuelekea maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani Julai Mosi mwaka huu.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger