******************
Na Mwandishi Wetu
KATIKA kuelekea siku ya wanawake duniani mkoani Mbeya,Kampuni ya Oryx Gas kwa kushirikiana na Mfuko wa Tulia leo wameandaa tamasha kubwa ambapo Oryx Gas wameshindanisha vikundi 50 vya wanawake wanaojishughulisha na biashara za vyakula kupika vyakula mbalimbali vya kiasili na washindi wa kila kikundi wataondoka na zawadi ya majiko ya gesi na pesa jumla ya shilingi milioni tano.
Hatua ya kuandaa mashindano hayo ya vyakula kwa wanawake wanaojihusisha na biashara ya vyakula ni mojawapo ya jitihada kampuni hiyo inafanya katika kuelimisha Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia kama mbadala wa kuni na mkaa.
Akizingumza mkoani Mbeya kuelekea Siku ya Mwanamke Dunia ambapo wameamua kuandaa mashindano hayo ya mapishi yaliyofanyika Machi 4,2023 , Meneja Masoko wa Kampuni ya Oryx Peter Ndomba ameelezea kwamba kumekuwepo na madhara makubwa ya kiafya,mazingira na kuichumi kutokana na jamii kutumia kuni na mkaa katika kupikia.
Hivyo amesema moja ya jitihada wanazofanya ni kuungana na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ili kuondokana na madhara na kuishi maisha bora.
"Tunaamini jitihada ambazo tumekuwa tunazifanya pia ni katika kutekeleza nia ya Rais Samia kuwa ifikapo mwaka 2030 angependa kuona zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia.Hivyo kwetu sisi tumeamua kuyabeba maono ya Rais na Serikali yake Kwa vitendo.
"Kwani tumekuwa tukitoa elimu kuhamasisha matumizi ya nishati ya gesi katika kupikia na tumekuwa tukigawa bure mitungi na majiko ya gesi kwa wananchi wa mikoa mbalimbali na leo tuko kwenye mashindano haya kwa lengo lile la kuendelea kuhimiza matumizi ya nishati safi katika kupikia,"amesema Ndomba.
Kuhusu ujumbe wao Kampuni hiyo kwa umma, Ndomba amesema wanawaomba wananchi walinde sana afya kwa kuepuka matumizi ya nishati chafu huku akifafanua katika kutoa hamasa mbalimbali wameanza kuona mabadiliko hasa kwa yale maeneo yaliyoathilika na ukataji miti.
"Hivyo basi tunazidi kuhamasisha wengi watumie gesi na ukweli ni kwamba Oryx Gas tunajivunia sana kukubalika na pia kuaminika na jamii na hii imetuwezesha kufikisha huduma sahihi ya gesi kila katika kila kijij cha Tanzania Bara na Zanzibar."
0 comments:
Post a Comment