Waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu kazi,ajira,vijana na watu wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari akitoa taarifa ya mwelekeo wa utekelezaji wa mipango ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2022/2023.(Picha na Fadhili Abdallah)
waandishi wa habari wa mkoa Kigoma wakisikiliza taarifa iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu kazi,ajira,vijana na watu wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako kuhusu mwelekeo wa utekelezaji wa mipango ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2022/2023
****
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi,vijana, ajira na watu wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa serikali imeanza kutekeleza mpango kabambe wa uwezeshaji kiuchumi kwa vijana kwa kuwapatia mafunzo na mitaji ili waweze kujiajiri na kutoa ajira kwa vijana wenzao.
Waziri Ndalichako alisema hayo mjini katika mkutano na waandishi wa habari na kueleza kuwa vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa na hivyo ni lazima kundi hili liweze kuwekewa mazingira mazuri ambayo yatawafanya kutoa mchango wao kwa taifa.
Moja ya mipango hiyo ameitaja inafanywa na wizara hiyo ni kutenga kiasi cha shilingi bilioni moja ambazo zitatolewa mikopo kwa vijana na kwa sasa kiwango kimeongezwa kutoka shilingi milioni 10 kwa kiwango cha juu na kufikia shilingi milioni 50 ambazo zitawezesha kuanzisha au kuendeleza miradi yenye tija kubwa.
“Sambamba na mikopo inayotolewa kupitia wizara ya kazi inayosimamia na ofisi ya Waziri Mkuu pia tutasimamia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri ambapo vijana wanapata asilimia nne hivyo vijana wanapaswa wajipange vizuri kuhakikisha wanatumia fursa hiyo,”Alisema waziri Ndalichako.
Sambamba na hilo alisema kuwa wizara imeanza kutoa mafunzo ya ujuzi na uana genzi kwa vijana 22,200 katika fani mbalimbali ili waweze kuwa na ujuzi ambao watatutumia kuanzisha miradi ikiwa ni mpango wa serikali kuwafanya vijana kujajiri na kuajiri vijana wenzao kwa wingi.
Alisema vijana 1500 waliopata ujuzi nje ya mfumo rasmi watatathminiwa na kuthibitishwa ujuzi wao, vijana 3000 watapata mafunzo ya ujuzi wa uana genzi, vijana 2400 watapatiwa mafunzo ya kitalu nyumba na vijana 500 watapatiwa mafunzo ya uchumi wa bluu ambapo wataweza kuanzisha miradi ya uvuvi na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.
Akizungumzia suala la watu wenye ulemavu Waziri Ndalichako alisema kuwa kwa mwaka huu wa fedha Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi,ajira na watu wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa serikali imeanza kutekeleza mpango kabambe wa kusaidia watu wenye ulemavu kwa kujenga vyuo vipya vitatu vya ufundi stadi na marekebisho ili kuwewezesha kujikwamua na kuwa na uwezo wa kujitegemea kiuchumi.
Vyuo hivyo alisema kuwa vitajengwa katika mikoa ya Mwanza, Kigoma na Songwe ambavyo vitaenda sambamba na ukarabati wa vyuo vinne katika mikoa ya Dar es Salaam,Tabora,Singida na Mtwara ambavyo vitasaidia watu hao.
Katika taarifa yake Waziri Ndalichako alisema kuwa serikali inachukua hatua mahsusi ya kuhakikisha mafao ya wastaa yanalipwa kwa wakati sambamba na kuboresha mifuko ya jamii na kuhakikisha pensheni za wastaafu hao zinalipwa kwa wakati.
Amesema kuwa serikali ya raisi Samia Suluhu imelipa kiasi cha shilingi bilioni 500 la deni la serikali kwa mifuko ya pensheni jambo ambalo linatoa taswira sahihi ya kuhakikisha mifuko hiyo inalipa pensheni za wastaafu kwa wakati.
Alisema kuwa hali hiyo pia inachangiwa na serikali kutoa hati fungani ya shilingi trilioni 2.1 ili kupunguza deni la shilingi trilioni 4.6 ambapo wanachama walikuwa hawachangii tangu mwaka 1999 na kwamba malipo hayo yanaimarisha utendaji wa mifuko hiyo kulipa wastaafu.
Waziri Ndalichako aliwataka watumishi kutumia mfumo wa simu kiganjani katika kuhakiki taarifa za uchangiaji zinazotolewa na waajiri ili kujua kama wamechangia jambo litakalowafanya kupunguza usumbufu wa kwenda ofisini kufuatilia taarifa hizo
0 comments:
Post a Comment