Friday, 5 August 2022

HER DIGNITY, AGAPE KUPAMBANA NA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO MAENEO YA MGODI WA MWADUI

...

Mkurugenzi wa Taasisi ya HER DIGNITY Annagrace Rwehumbiza akizungumza kwenye kuhitimisha mafunzo ya MTAKUWWA ngazi ya vijiji kwenye maeneo ambayo yanazungukwa na Mgodi wa Mwadui. 
 
Na Michael Abel, KISHAPU 
 
TAASISI YA  HER DIGNITY, na Shirika la AGAPE wamekutana na Kamati ya Mpango Mkakati wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) ngazi ya vijiji, kutoka kwenye vijiji 11 ambavyo vinazunguka Mgodi wa Almasi Mwadui wilayani Kishapu, kutoa mafunzo na kujadili namna ya kupunguza matukio ya ukatili.

Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa mwezi mmoja, na yamehitimishwa leo Agost 4, 2022 katika ukumbi wa Mikutano ndani ya Mgodi wa Mwadui.

Mkurugenzi wa taasisi ya HER DIGNITY Annagrace Rwehumbiza, akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo, amesema kwenye maeneo ya Migodi kumekuwa na matukio mengi ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, na ndiyo maana wamekutana na kamati hizo za MTAKUWWA Ngazi vya vijiji ili kutoa elimu na kujadiliana namna ya kupunguza matuko hayo au kuyamaliza kabisa.

“Maeneo ya Migodi hua kuna matukio mengi ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto sababu ya muingiliano wa watu wengi, ndiyo maana Shirika letu la HER DIGNITY na AGAPE, tumeamua kutoa elimu kwenye Kamati hizi za MTAKUWWA ngazi ya vijiji kwenye maeneo ambayo yanazungukwa na Mgodi wa Mwadui ili kupunguza ukatili huo,”amesema Rwehumbiza.

“Kamati hizi za MTAKUWWA zinajumuisha viongozi mbalimbali wakiwamo wa kidini, Serikali, na Jeshi la Jadi Sungusungu hivyo tunaimani kabisa kupitia mafunzo hayo ambayo mmeyapata ndani ya mwezi mzima tunaimani mtakwenda kuyafanyia kazi kwa vitendo na kupunguza vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto,”ameongeza.

Naye Mkufunzi wa Mafunzo hayo Rose Shao, amesema changamoto kubwa ambayo amekuwa akiiona kwenye maeneo ambayo yanazungukwa na Migodi, hasa kwenye Masuala ya ukatili dhidi ya watoto, ni wazazi kushindwa kutekeleza majukumu yao katika familia na kusababisha watoto kujiingiza kwenye ajira za migodini katika umri mdogo.

Baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo akiwamo Magreth Ngeleja, amesema mafunzo yamewajengea uwezo mkubwa namna ya kupambana na matukio ya ukatili wa jinsia dhidi ya wanawake na watoto

"Mafunzo haya yametuelimisha juu ya masuala ya ukatili kwetu sisi wanawake na watoto, ukizingatia hali ya matukio haya kwetu sisi ambao tunaoishi kwenye maeneo ya Migodi familia nyingi zimetekezwa na wazazi kusahau majukumu na kusababisha familia nyingi watoto wao kujiendesha wenyewe, hivyo kupitia elimu hii nitakwenda kutoa elimu pia kwa familia na jamii inayonizunguka".amesema Ngeleja.
Mkurugenzi wa taasisi ya HER DIGNITY Annagrace Rwehumbiza akizungumza kwenye kuhitimisha mafunzo ya MTAKUWWA ngazi ya vijiji kwenye maeneo ambayo yanazungumwa na Mgodi wa Mwadui.

Mwezeshaji Lukia Masawanyika akitoa elimu kwenye mafunzo ya kamati ya MTAKUWWA.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye kazi ya makundi.

Washiriki wakiwa kwenye kazi ya makundi.

Washiriki wakiwa kwenye kazi ya makundi.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger