Saturday 24 July 2021

WAZIRI ALLY AFARIKI DUNIA, MAZISHI KUFANYIKA KESHO KWAO PONGWE

...

Waziri Ally wakati wa uhai wake

Aliyekuwa mwanamuziki mkongwe wa Kilimanjaro Band maarufu kama Njenje Waziri Ally amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.

Taarifa kamili kuhusu ratiba ya mazishi yake iliyotolewa na Aboubakary Liongo kwa niaba ya familia inaeleza kuwa.

"Ndugu na jamaa wote kukutana Mwananyamala Hospitali asubuhi hii, tunatarajia mwili utasafirishwa leo saa tano asubuhi kwenda Tanga ambako msiba utakuwa barabara ya 21 karibu na kiwanda cha Chuma zamani na mazishi yatakuwa kesho Jumapili kijijini kwao Pongwe".
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger