Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani(Kulia) akizungumza na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango(kushoto) wakati wa uzinduzi wa Mradi wa umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili A Ngazi ya Mkoa uliofanyika wilayani Same, Julai 29,2021.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Kalemane baada ya kuwakabidhi kifaa cha UMETA kwa ajili ya kuunganishiwa umeme katika shule yao wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili A ngazi ya Mkoa uliofanyika katika kitongoji cha Mheza wilayani Same, Julai 29,2021.
Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili A ngazi ya Mkoa uliofanyika wilayani Same, Julai 29,2021 uliozinduliwa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani.
Baadhi ya wanafunzi na wananchi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati akizundua Mradi wa umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili A ngazi ya Mkoa uliofanyika wilayani Same, Julai 29,2021.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiwa na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango,wanafunzi pamoja na viongozi wa wilaya ya Same wakikata utepe kuwasha umeme katika Kijiji cha Kifaru wakati wa ziara ya uzinduzi wa Mradi wa umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili ngazi ya Mkoa wa Kilimanjaro uliofanyika wilayani Same, Julai 29,2021.
Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango akisoma maelezo ya jiwe la msingi baada ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani kuzindua Mradi wa umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili ngazi ya Mkoa uliofanyika wilayani Same, Julai 29,2021.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akipongezwa na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango mara baada ya kuzindua Mradi wa umeme wa Ujazilizi Fungu la Pili A Ngazi ya Mkoa Uliofanyika katika kitongoji cha Mheza, Julai 29,2021.
...............................
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani amewaagiza wakandarasi wanaojenga miundombinu ya kusambaza umeme vijijini kupeleka umeme katika maeoneo maalum ambayo yametengwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda.
Dkt. Kalemani alitoa agizo hilo wakati akizindua Mradi wa Ujazilizi Umeme Vijijini Fungu la Pili A ngazi ya mkoa uliofanyika Julai 29,2021 katika kijiji cha Mheza wilaya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro.
Aidha, amewakumbusha viongozi wa Serikali za Mitaa katika ngazi ya kata na vijiji kutenga maeneo maalum ya uwekezaji wa viwanda ili yaweze kupelekewa miundombinu ya umeme wakati wa utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini. “Tumieni umeme kufanya biashara muongeze thamani ya mazao ya kilimo na mifugo kwa kuanzisha viwanda” alisisitiza.
Waziri Kalemani amesema Mradi huo utatekelezwa kwa muda miezi 12 na Serikali imetenga kiasi cha takribani Shilingi Bilioni 8.59 kwa ajili ya kuvifikishia umeme vitongoji ambavyo havina umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro katika fedha hizo Wilaya ya Same imetengewa zaidi ya Shilingi Bilioni 3.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Mhe. Anne Kilango Malecela ameishukuru Serikali kwa kupelekewa miradi hiyo ya kusambaza umeme vijijini na kuomba maeneo ambayo bado hayajafikishiwa umeme yapatiwe nishati hiyo.
0 comments:
Post a Comment