Tuesday, 6 July 2021

TRILIONI 2.03/- KUWATOA KWENYE UMASKINI WALENGWA WA TASAF

...

 


Samson Kagwe kutoka TASAF Makao makuu akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa wawezeshaji wa kuratibu kaya maskini Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu, Shinyanga

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii wa Kunusuru kaya maskini TASAF III awamu ya pili ,unatarajia kunufaisha kaya milioni 1.4 nchi nzima kuwatoa walengwa wa mfuko huo kwenye umaskini.

Hayo yamebainishwa leo na Samson Kagwe kutoka TASAF makao makuu, wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi wa TASAF, kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wawezeshaji ambao watakwenda kuratibu zoezi la kubaini kaya maskini katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Amesema mpango huo wa TASAF 111 awamu ya pili, utatekelezwa ndani ya miaka Minne, na ulianza rasmi 2020- 2023, ambao utanufaisha kaya Milioni 1.4 sawa na wakazi Milioni 7, ambao wataondokana na umaskini.

"Mpango huu wa TASAF 111 awamu ya pili, utatekelezwa katika Halmashauri zote nchi nzima ikiwamo na Zanzibar, kwa kuziwesha Kaya Maskini kuinuka kiuchumi, na gharama za mpango huu kwa kipindi hiki ni Sh.Trilioni 2.03," amesema Kagwe.

"Mambo ambayo yatazingatiwa kwenye mpango huu, ili kuwatoa walengwa kwenye umaskini, ni kuongeza Rasilimali za uzalishaji mali, ikiwamo ufugaji wa mifugo, kilimo,uvuvi, na shughuli mbalimbali za kijasiriamali," ameongeza.

Pia ameongeza mambo mengine ambayo yatatekelezwa, ni kuboresha upatikanaji wa huduma za msingi, ikiwamo upatikanaji wa huduma ya maji, afya, na elimu.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Edward Maduhu, amewataka waratibu ambao watakwenda kubaini kaya hizo maskini wilayani humo, wakalifanye zoezi hilo kwa uaminifu mkubwa, na kutoingiza kaya zisizo kuwa na sifa.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi, amesisitiza zoezi hilo likafanyike kwa uaminifu mkubwa ili kusiwepo na kaya hewa.

Tazama picha hapa chini
Samson Kagwe kutoka TASAF Makao makuu akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa wawezeshaji wa kuratibu kaya maskini Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Katibu tawala wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Edward Maduhu, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Isack Sengerema akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Wawezeshaji wa kuratibu Kaya maskini Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya kwenda kuratibu zoezi hilo la kubaini kaya maskini.
Wawezeshaji wa kuratibu kaya maskini Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya kwenda kuratibu zoezi hilo la kubaini kaya maskini.
Wawezeshaji wa kuratibu kaya maskini Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya kwenda kuratibu zoezi hilo la kubaini Kaya maskini.
Wakuu wa Idara Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ,wakifuatilia mafunzo ya wawezeshaji ambao watakwenda kuratibu zoezi la kubaini Kaya Maskini wilayani humo.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ,wakifuatilia mafunzo ya wawezeshaji ambao watakwenda kuratibu zoezi la kubaini kaya maskini wilayani humo.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ,wakifuatilia mafunzo ya wawezeshaji ambao watakwenda kuratibu zoezi la kubaini kaya maskini wilayani humo.
Picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mafunzo siku ya kwanza.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger