Sunday 25 July 2021

STAMIGOLD YANOGESHA MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA....YASHUKURU SERIKALI KUWAPA UMEME

...


Afisa Utumishi wa Kampuni ya STAMIGOLD, Mhunda Nyakiroto (kulia) akimwelezea Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (wa pili kushoto) shughuli wanazofanya kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kampuni ya STAMIGOLD ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kupitia mgodi wake wa Stamigold Biharamulo (Stamigold Biharamulo Mine - SBM) uliopo wilayani Biharamulo mkoa wa Kagera umeishukuru serikali kwa kupeleka huduma ya umeme wa TANESCO hali ambayo itapunguza gharama za uendeshaji kutoka shilingi Bilioni 1.2 hadi shilingi milioni 400 au 300 kwa mwezi.

Shukrani hizo zimetolewa na Afisa Utumishi wa Kampuni ya STAMIGOLD, Mhunda Nyakiroto leo Jumapili wakati Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya akitembelea banda la Kampuni ya STAMIGOLD kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika Uwanja wa Zainab Telack katika kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Afisa Utumishi wa Kampuni ya STAMIGOLD, Mhunda Nyakiroto amesema wanaishukuru serikali kwa kuwapelekea huduma ya umeme wa TANESCO kutoka Geita hali ambayo itasaidia gharama kubwa ya uzalishaji wa madini ya dhahabu ambapo wamekuwa wakitumia genereta za dizeli.

"Tangu mgodi huu uwe chini ya Serikali mwaka (2014), na kuanza uzalishaji rasmi 2015, umekuwa ukiingia kwenye gharama kubwa ya kutumia Genereta na mafuta ya Diesel yenye gharama za Shilingi Bilioni 1.2 kwa mwezi na baada ya kupata huduma ya umeme gharama itapungua na tutatumia shilingi Milioni 300 au 400",amesema Nyakiroto.

Katika hatua nyingine, Nyakiroto amesema wanashiriki maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuonesha jinsi wanavyofanya shughuli za uchimbaji madini ya dhahabu pamoja kueleza manufaa ya mgodi wao kwa wananchi.

“Miongoni mwa manufaa wanayopata wananchi kupitia mgodi wa Stamigold chini ya Meneja Mkuu wa mgodi Mhandisi Gilay Shamika ni pamoja na ajira. Tumeajiri Watanzania 610. Pia tumesaidia ujenzi wa miundo mbinu na miradi kwa jamii ikiwemo zahanati ya Nampalahala, barabara za vijiji vya Mavota, Mkunkwa na Msalabani vilivyopo katika kata ya Kaniha wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera”,ameeleza Nyakiroto.

“Hali kadhalika tunatumia maonesho haya kuonesha zao jipya la mkaa mbadala unaotumia makaa ya mawe ‘Rafiki Briquate’ ili kutunza mazingira. Bei ya mkaa huu mbadala ni rafiki lakini pia mkaa huu hautoi moshi. Tutaanza uzalishaji kamili wa mkaa huu mwishoni mwa mwezi Julai,2021”,amesema.

Amesema mgodi wa STAMIGOLD pia unaendelea kusaidia wajasirimali kwa kununua bidhaa zao kama vile ng’ombe, mboga mboga, matunda na samaki katika masoko ya Runzewe na Chato

Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya ameupongeza mgodi wa STAMIGOLD hatua inayoendelea nazo katika uzalishaji wa madini akieleza kuwa faida imekuwa ikipanda kila Mwaka na kusaidia STAMICO kulipa gawio Serikalini.
Afisa Utumishi wa Kampuni ya STAMIGOLD, Mhunda Nyakiroto (kulia) akimwelezea Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (wa pili kushoto) shughuli wanazofanya kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika Uwanja wa Zainab Telack katika kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Utumishi wa Kampuni ya STAMIGOLD, Mhunda Nyakiroto (kulia) akimwelezea Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (wa pili kushoto) shughuli wanazofanya kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
Afisa Utumishi wa Kampuni ya STAMIGOLD, Mhunda Nyakiroto (kulia) akimwelezea Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (katikati) shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya(katikati) akiangalia vipeperushi na bidhaa mbalimbali kwenye banda la Kampuni ya STAMIGOLD katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya(katikati) akiondoka kwenye banda la Kampuni ya STAMIGOLD katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya(kushoto) akiondoka kwenye banda la Kampuni ya STAMIGOLD katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger