Friday, 9 July 2021

Mji Wa Serikali Mtumba Kuwa Na Miundombinu Ya Kisasa

...


Na Mwandishi wetu-  Dodoma
Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma umeendelea kuwekewa  miundombinu ya kisasa itakayosaidia na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi wanaofika katika Ofisi zote zilizopo katika eneo hilo.

Hayo yamesemwa  hivi karibuni  na   Katibu wa Kikosi Kazi cha  Kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na ujenzi wa mji wa Serikali  Bw.Meshack Bandawe wakati akiongoza kikao cha Timu ya wataalam wanaosimamia ujenzi wa miundombinu ya kudumu ya Mji wa Serikali inayohusu maji safi na maji taka,umeme, mawasiliano, usalama, ujenzi wa majengo marefu ya wizara awamu ya pili, barabara za lami, zimamoto na uokoaji, gesi na upandaji miti  ya matunda.  

“Mji wa Serikali hapa Mtumba  utakuwa wa kisasa  kutokana na miundombinu iliyojengwa na inayoendelea kujengwa hapa kama vile barabara za lami, uwekaji taa za barabarani, majengo ya kisasa na miundombinu mingine itakayoufanya mji huu kuwa na mvuto wa kipekee  kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Kwa upande wa miundombinu mingine Bandawe amesema kuwa itawekwa chini ya ardhi ili kuweka mandhari ya mji huo kuwa ya kisasa na  ya kuvutia.

Akieleza kuhusu ujenzi wa barabara za lami Bandawe amesema kazi hiyo inaendelea  na imefikia zaidi ya asilimia 70 na kazi yakuweka miundombinu mingine inaendelea kama ilivyopangwa.

Ujenzi wa Mji wa Serikali awamu ya pili inatarajiwa kuhusisha ujenzi wa majengo makubwa ya gorofa  kwa kila Wizara. Aidha katika mji wa Serikali Mtumba kutapandwa miti ya aina mbalimbali ya matunda.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger