Friday 23 July 2021

ALIYEIBA GARI NA KUTAMBA NALO MTAANI AGONGA NA KUUA WANAWAKE WANNE

...
Wanawake waliofariki dunia kwa kugongwa na gari
**
 Wakazi wa Kiharu katika huko Murang'a nchini Kenya wanaomboleza kifo cha wanawake wanne waliofariki dunia walipokuwa wakirudi nyumbani kutoka kanisani na gari lililokuwa limepoteza mwelekeo likiendesha na kijana mdogo aliyeiba gari hilo nyumbani kwao bila idhini ya wazazi wake.

Tukio hilo la kusikitisha ambalo lilipelekea kifo cha Jane Waiego, Mary Njeri, Margret Karura Waithaka na Mary Waithera limetokea Jumapili, Julai 18,2021.

 Ripoti ya NTV ilionyesha kuwa gari hilo lilikuwa likiendeshwa kundi la vijana ambao walitoweka pindi tu baada ya kutokea kwa ajaili hiyo kwenye ya barabara ya Murang'a- Kangema.

 Ripoti hiyo pia ilionesha kwamba mvulana aliyekuwa mdogo zaidi kati ya wenzake alikuwa amelichukua gari hilo kwao bila idhini ya wazazi wake.

Wanawake watatu walifariki dunia papo hapo naye mmoja alipoteza maisha yake akipokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Murang'a. 

Gari hilo lilipelekewa katika kituo cha polisi cha Murang'a huku uchunguzi ukianza rasmi.

 Familia zao zinaomba msaada wa kuandaa mazishi ya wanne hao.

 Tukio hilo linajiri takriban mwezi mmoja baada ya maafisa wa polisi kumkamata jamaa ambaye mtoto wake alinaswa kwenye kamera akiendesha gari la Toyota Prado TX katika eneo la Delview Park huko Thika.

 Kwenye video iliyosamba Jumapili, Juni 13, kijana huyo wa miaka saba alionekana akiendesha gari hilo la kifahari bila wasiwasi wowote huku akibadilisha gia kama mtaalamu.

 Kulingana na ripoti ya polisi, Ayub Kinyanjui Muigai alikamatwa katika eneo la Gatanga na maafisa wa trafiki kutoka Kikwara wakishirikiana na makachero wa DCI.

Chanzo - Tuko News
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger