Friday, 26 February 2021

WATANZANIA WANAVYOVUNA MAMILIONI YA BIKOSPORTS

...

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kwa wanaofahamu umuhimu wa michezo ya kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali duniani, ukiwamo huu wa Bikosports, huwezi kuwaeleza lolote linaloharibu sifa madhubuti ya mchezo huo.

Hii ni kwa sababu watu wengi nchini Tanzania yakiwamo makundi makubwa ya vijana wanapata mitaji ya kifedha na kijikwamua kiuchumi kwa kupitia mchezo wa Bikosports unaoongoza kutoa washindi wengi sanjari na kukabidhi zawadi haraka muda mfupi baada ya kupatikana mshindi kwa wanaocheza kwa kutumia mitindo yote ikiwa ni pamoja kwa wanaotumia mtandao wa www.bikosports.co.tz.

Kwa Dunia ya leo yenye changamoto kubwa za ukosefu wa ajira, ni jambo baya kuamini kwamba wote wanaoamua kucheza mchezo wa kubashiri matokeo wanapoteza muda. Sio tu ushindi wa fedha za zawadi kutoka Bikosports, bali pia kuna faida nyingi za kucheza ikiwamo ya kutumia akili, maarifa na muda wa kufuatilia michezo mbalimbali duniani.

Mtu anayejihusisha na sekta ya kubeti, kamwe huwezi kumkuta amelowea kwenye pombe. Muda wake mwingi huutumia kwa kuwaza namna ya kushinda, hivyo akili yake huchangamka mara dufu. 

Kwa wanaojua namna ya kubeti watakubaliana na mimi kwamba sio lazima uwe na mtaji mkubwa ili mtu aweze kushinda mamilioni ya Bikosports. Mtu anaweza kubeti hata kwa shilingi mia tano huku akiweza kunyakua fedha nyingi kila siku.

Mtu mwenye shilingi mia tano ni nzuri zaidi kuitumia kwa kubeti Bikosports kuliko kuinunulia sigara au bando kwa ajili ya kuangalia vitu visivyokuwa na faida katika maisha yake. Suala hili linapaswa lijadiliwe bila kificho ili kwa pamoja tuweze kuinua uchumi wa Watanzania wote.

Katika mazungumzo na mtandao huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Bikosports, Charles Mgeta anasema uchezaji wa mchezo wa kubashiri matokeo sio upotezaji wa muda na wengi wanaoshiriki ni wale wenye mwamko vichwani mwao, wakiwa na ndoto kubwa za kujiondoa kwenye umasikini.

"Michezo hii inashirikisha wasomi na wasiosoma, wanawake kwa wanaume, wenye ajira rasmi na hata wale ambao hawana ajira rasmi za kujipatia kipato tofauti na mitazamo ya wengi.

"Kwenye sekta hii, sisi Bikosports tunaamini fedha zetu zipo wazi na kila mmoja anaweza kuzipata endapo ataamua kucheza kwa malengo kwa kiasi chochote alichokuwa nacho ndio maana ukumbi wa uchezaji ukiwa ni mpana ukiwamo mtandao wetu wa www.bikosports.co.tz", alisema Mgeta.

Kwa mujibu wa Mgeta, mbinu nzuri za ushindi wa Bikosports ni kujitoa kwa nguvu zote kubashiri matokeo sanjari na utumiaji wa akili na bahati huku akisema pia sio tu wanaocheza Bikosports kwa kutumia mtandao wa www.bikosports.co.tz , pia watu wanaweza kubeti kwa kutumia namba ya Kampuni ambayo ni 101010.

Anasema hata wale wasiokuwa na uwezo wa kutumia simu kubwa (smartphone) wanaweza pia kucheza kwa kuingia kwa kutumia simu ndogo kwa namba *149*89# ikiwa ni njia rahisi za ubashiri matokeo ya michezo kwa kupitia kampuni pendwa ya Bikosports.

Watanzania wanaweza kucheza Bikosports pia kwa kuanzia sh moja tu, huku kiasi hicho cha fedha kikimuwezesha kuvuna hadi sh milioni 50 huku ushindi wake ukiwa mwepesi na kila mtu anaweza kushinda kwa kupitia Bikosports.

Kwa kupitia sekta hiyo ya michezo ya kubahatisha, watu mbalimbali wanajivunia mamilioni ya fedha kila siku, huku serikali wakinufaika kwa kupata kodi zinazoendesha nchi yetu. 

Kijana mwenye umri mdogo wa miaka 19 anayekwenda kwa jina la Salum Hassan Shaban anaipongeza kwa kurahisisha namna bora ya kubeti, ikiwa ni baada ya kunyakua sh milioni 16.8 kutoka kwenye kampuni ya Bikosports.

"Mimi ni mdau haswa wa michezo hii, lakini Bikosports ndio Kampuni inayoeleweka katika sekta hii kiasi kwamba nashawishika na kuwashauri Watanzania kucheza kwa wingi ili wavune kama nilivyofanikiwa kwa wanaotumia simu ndogo na wanaobeti kwa kupitia mtandao wa www.bikosports.co.tz.

"Sekta ya ubashiri matokeo ni ajira inayolipa, hivyo harakati zozote za kuidumaza michezo hii inawaweka njia panda watu wengi wanaoamini hapa ndio ukumbi unaoweza kuchanganya watu wote bila kuangalia tofauti zetu za kipato na kielimu pia," alisema.

Naye mshindi wa sh milioni 4.8 kutoka Newala, Yusuph Mkota, anasema ni kheri wanaocheza Bikosports ili wapate pesa wajimudu kiuchumi, kuliko wale wanaotumia sh mia tano zao kwa masuala ya pombe na anasa nyingine.

"Nawashukuru Bikosports kwa kunipa zawadi zangu mapema siku moja tu baada ya kuibuka na ushindi, nawashauri vijana wenzangu tutumie fursa nzuri ya uvunaji wa pesa kwa kupitia Bikosports.

"Huu ni mchezo mzuri wa kuweza kuziwinda fedha za Bikosports, huku nikiamini nitaendelea kucheza ili niendelee kupata fedha kwa ajili ya kurahisisha maisha yangu na uchumi wangu kwa ujumla,"alisema Mkota huku akitabasamu.

Wengine waliozungumzia umuhimu wa michezo ya kubashiri matokeo kwa kupitia www.bikosports.co.tz ni pamoja na Sharifu Juma (Mtwara) sh milioni 2.8, Priscus Mboya (Dodoma) sh milioni 5.4, Gabri Shayo (Moshi) sh milioni mbili na Boay Axwesso (Karatu) sh milioni 3.2.

Wote hao waliishukuru Bikosports kwa kuendesha mchezo huo bila ubabaishaji hali inayowavutia Watanzania wengi kushiriki kucheza www.bikosports.co.tz. ikiwa ni mwelekeo mzuri wa ukuzaji wa uchumi wa Watanzania.

Pia Watanzania wanaweza kuifuatilia Bikosports kwenye page zao za Facebook na Instagram sanjari na kuonyesha picha za washindi na Watanzania kwa ujumla wanavyoiongelea Bikosports.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger