WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu ameagiza watu ambao watabainika kutumia vifungashio vya mifuko ya Plastic baada ya miezi mitatu aliyoitoa kupita wakamatwe na kuchukuliwa hatua.
Ummy alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake katika Jiji la Tanga kubwa ni kutokana na malalamiko yanayotoka kwenye Jiji hilo kuhusu uchafuzi wa mazingira unaotokana na viwanda vilivyopo vya kuzalisha saruji na chokaa.
Alisema kwamba suala la vifungashio alikwisha kutoa miezi mitatu ambapo mwezi Aprili mwaka huu ndio litakuwa limekwisha hivyo hategemei kuona baada ya kumalizika watu wataendelea kutumia vifungashio vya namna hiyo.
“Nisisitize suala la vifungashio nilitoa miezi mitatu mwezi wanne litakuwa limekwisha baada ya miezi mitatu kwisha tutatoa agizo la kuwaambia mkamatwe kwa yeyote ambaye anatumia vifungashio maana mifuko ya plastic imerudi kwa kigezo cha vifungashio”Alisema Waziri Ummy.
Aidha alisema kwamba hivi sasa unaona watu wameweka karoti wamezifunga kwenye mifuko kwamba wamerudisha mifuko ya plastic kwa kigezo cha vifungashio hivyo endele kuzibidi mifuko hiyo.
“Lakini ikiisha miezi mitatu niliyoitoa mtakayemkuta anaendelea kutumia mifuko ya plastic endeleeni kuchukua hatua stahiki dhidi yao “Alisema .
Hata hivyo Waziri Ummy alizitaka Halmashauri ziandae mpango kazi wa Mazingira ambao utakuwa na tija kubwa katika kusimamia na utekelezaji wa kazi hizo kwenye maeneo yao.
Alisema mpango huo lazima utengewe bajeti kwa sababu ni suala muhimu kama yalivyo masuala mengine ambayo yamekuwa yakifanyiwa hivyo katika maeneo husika.
“Pia tuhakikishe Halamshauri zote zinaweka vipaumbele na bajeti ya kutekeleza shughuli za utunzaji na uhifadhi mazingira lakini pia suala la uteuzi wa maafisa mazingira kwenye mamlaka ya serikali za mitaa waendelee nalo”Alisema
Waziri Ummy Ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga alisema lakini changamoto zilizopo bado hakuna mfumo mzuri wa ngazi ya halmashauri ya Usimamizi wa shughuli za Mazingira.
Kutokana na uwepo wa changamoto hiyo Waziri Ummy alimuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Kukaa na Katibu Mkuu Tamisemi ili kutengeneza mfumo mzuri .
Alisema kwa sababu wanaweze kuwa wanapiga kelele mkoani lakini kama Halmashauri hazitakuwa na mfumo nzuri wa kusimamia shughuli za mazingira hataweza kupata hayo matokeo ambayo wameyapata ili tufanikishe lazima warekebishe muundo kwenye ngazi ya Halamshauri za Serikali za Mitaa.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo,Afisa Mazingira Mkoa wa Tanga Thimotheo Sosiya alisema mkoa huu unatekeleza kampeni ya mazingira kwa pamoja kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi na imeleta mafanikio makubwa kwenye kutkomeza uchafuzi maeneo korofi na mazingira.
Aisema lakini katika suala hilo changamoto kubwa ni uwezo mdogo wa Halmashauri kuondosha taka ngumu ikiwemo mwitiko mdogo wananchi kufanya usafi kwa hiari huku akieleza mkoa umejipanga.
Alisema kujipanga huko ni kuunda vikosi kazi kwenye Halmashauri ambavyo vitakuwa na kazi ya kusimamia mazingira na kwamba wanaotupa taka sasa wawepo watu ambao wanakuwa tayari kuwakamata na kuwapiga faini.
0 comments:
Post a Comment