Sunday, 28 February 2021

SHIRIKA LA GCI LATOA ELIMU YA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO KWA WANAUME WANYWA KAHAWA SHINYANGA MJINI

...

Meneja Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Mtoto wa Shirika la GCI, Victoria Emmanuel (kulia) akizungumza wakati akitoa elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wanaume wanaokunywa Kahawa katika eneo la Nguzo Nane Mjini Shinyanga.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Shirika la Green Community Initiatives (GCI) linalojihusisha na utetezi wa Haki za Wanawake na Watoto, Vijana, Wazee, Watu wenye ulemavu naWanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi limetoa elimu ya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kwa Wanaume wanaokunywa Kahawa katika Kijiwe cha Nguzo Nane Mjini Shinyanga.

Shirika hilo lenye makao yake makuu Mjlimetoa elimu ya Ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wanaume wanaokunywa Kahawa Jumamosi Februari 27,2021 kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 8,2021 na utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA).

Meneja Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Mtoto wa Shirika la GCI, Victoria Emmanuel alisema wanatoa elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wanaume kwani ni kundi linalolaumiwa kutenda ukatili kwa watoto na wanawake na kwamba pia watayafikia makundi ya wanawake na mikusanyiko ya kijamii ili wananchi wahamasike kushiriki kutokomeza vitendo vya ukatili.

“Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Mwezi Machi 8 lakini pia sisi GCI kama miongoni mwa watekelezaji wa Mpango Mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, tunaendelea kutoa elimu ya masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto “,alieleza Victoria.

Alieleza kuwa shirika la GCI limeanzisha kampeni ya Sauti ya Mwanamke na Mtoto likitumia kauli mbiu ya 'Tokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto' kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusu madhara yatokanayo na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto mkoani Shinyanga ambao ni miongoni mwa mikoa vinara wa matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Aliyataja matukio ya ukatili kuwa ni pamoja na ndoa za utotoni,mimba za utotoni,utekelezaji wa familia,malezi duni ya watoto, watoto kuchomwa moto,kunyimwa chakula,kubakwa,kulawitiwa,kutelekezwa,kuitwa majina mabaya na ukatili wa kiuchumi,vipigo kwa wanawake na watoto kutoka kwa watu wao wa karibu mfano mume,mjomba,baba n.k.

Wakichangia mada ya ‘Nani alaumiwe kuwa chanzo cha ukatili dhidi ya wanawake na watoto’, wanaume hao waliokuwa katika Kijiwe cha Kahawa cha bwana Athumani Ibrahim kilichopo Mkabala na Zahanati ya Miti Mirefu Nguzo Nane Mjini Shinyanga, wanaume hao walisema migogoro ndani ya familia ni chanzo kikubwa cha vitendo vya ukatili.

Deogratius Moya alisema kutoelewana ndani ya familia ni chanzo kikubwa cha vitendo vya ukatili hali inasababisha wanaume wasiopenda maneno maneno huamua kuchelewa kurudi nyumbani, kutelekeza familia na kuendelea na maisha mengine hali inayosababisha watoto kukosa haki za msingi.

“Malezi ni changamoto kubwa, mfumo wa kuiga maisha kwa wanawake na watoto umetuletea balaa. Wanakuwa na tamaa ya kuiga maisha ya watu wengine na kupenda vitu vidogo vidogo. Vitu vya rahisi rahisi vinasumbua watoto wetu matokeo yake wanaambulia kupewa mimba na kukatishwa masomo yao”,alisema.

“Ndoa ni chanzo kikubwa cha ukatili. Wanaoana tu hawafanyi uchunguzi ndiyo maana tunaona leo harusi kubwa lakini baada ya siku chache ndoa chalii au mwanaume anabadilika,anaanza kupiga mke wake au unashangaa tu amepata mke mdogo anatekeleza mke wa kwanza,watoto na mke wanaanza kuteseka”,aliongeza.

Katika hatua nyingine aliwatupia lawama wanawake watumishi wa umma na wafanyabiashara kuwa chanzo cha matukio ya ukatili dhidi ya watoto kutokana na kuwa na muda wa kukaa na watoto badala yake wanawaachia wafanyakazi wa ndani kuhudumia watoto.

Elisha Philipo alisema baadhi ya wanawake wanawatumikisha watoto kwa kuwapa kazi ya kuuza vitafunwa,chai na kuokota chupa/makopo ya maji nyakati za masomo.

Naye Alex Elias na Adam Hussein walisema kitendo cha kukurupuka kuoa au kuolewa ni tatizo jingine kwani wanaoana kutokana na tama za kimwili, bila kuchunguzana tabia kwa kina matokeo yake wakioana migogoro inaanza,ndoa inavunjika watoto wanakosa uelekeo na kujikuta wakifanyiwa ukatili.

Kwa upande wake, Stephen Wilson alisema Utandawazi ni janga jingine ambapo sasa wanawake wengine hawataki kuwaheshimu waume zao wakidai haki sawa ambapo wanaume wasiopenda ugomvi huamua kutelekeza familia.

"Utandawazi unachangia sana wanawake kujiona wapo juu zaidi ya wanaume, wanadai haki sawa kwa kila kitu hawataki kuulizwa na waume zao. Hizi ganji zinasababisha ukatili, mwanaume akiacha pesa za mahitaji nyumbani hayanunuliwi, akimuuliza mke wake kulikoni hujawanunulia chakula watoto wakati wakati pesa nimekuachia mwanamke anapanda juu,ukimpiga makofi anakimbilia polisi anaonewa. Ndiyo maana wanaume wasiopenda ujinga/ugomvi wanaamua kuendelea na maisha mengine wanaacha familia au kuongeza mke",alieleza. 

Adam Hussein alisema mavazi yasiyofaa kwa wanawake ‘yakionesha maumbo yao’ yanachochea vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuwaingiza wanaume katika tamaa ya kimapenzi ,hakuna ndoa tena na matokeo yake kuwapa ujauzito na kutelekeza mimba na watoto.

Kwa upande wake, Shaban Martin aliiomba serikali kukataza mavazi yasiyofaa kwani sasa baadhi ya wanawake wanavaa mavazi yanayoonesha viungo vyao na kuchochea vitendo vya kingono huku Adam Hussein akisisitiza watoto wafundishwe maadili.

Wanaume hao pia waliomba serikali mkoani Shinyanga kuchukua hatua dhidi ya wanawake wanaofanya biashara ya ngono katika baadhi ya maeneo kwani inamomonyoa maadili.

Mwakilishi wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Jeshi la Polisi wilaya ya Shinyanga, Bryson John aliwataka wazazi kuacha tabia ya kuwalaza watoto chumba kimoja na wageni kwani baadhi yao siyo wema wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya ukatili ikiwemo kuwalawiti na kuwabaka.

Aidha aliwasihi wanandoa kupendana na kuhakikisha wanaepuka migogoro huku akiwasisitiza wanaume wanaofanyiwa ukatili watoe taarifa kwenye dawati la jinsia na watoto.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Mtoto wa Shirika la GCI, Victoria Emmanuel akizungumza wakati akitoa elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wanaume wanaokunywa Kahawa katika Kijiwe cha Athumani Ibrahimu kilichopo mkabala na Zanahati ya Miti Mirefu Nguzo Nane Mjini Shinyanga Jumamosi Februari 27,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Mtoto wa Shirika la GCI, Victoria Emmanuel akizungumza wakati akitoa elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wanaume wanaokunywa Kahawa katika Kijiwe cha Athumani Ibrahimu kilichopo mkabala na Zanahati ya Miti Mirefu Nguzo Nane Mjini Shinyanga
Muonekano wa kijiwe cha Kahawa cha bwana Athumani Ibrahim kilichopo Nguzo Nane Mjini Shinyanga
Wanaume wakiwa katika Kijiwe cha Kahawa cha Athumani Ibrahim Nguzo Nane Mjini Shinyanga wakipata elimu ya madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Wanaume wakiwa katika Kijiwe cha Kahawa cha Athumani Ibrahim Nguzo Nane Mjini Shinyanga wakipata elimu ya madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Meneja Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Mtoto wa Shirika la GCI, Victoria Emmanuel (kulia) akitoa elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wanaume wanaokunywa Kahawa katika Kijiwe cha Athumani Ibrahimu Nguzo Nane Mjini Shinyanga. Katikati ni Mhasibu wa shirika la GCI Mongo akiwa na mfanyakazi mwenzake, Elizabeth Samson
Mhasibu wa Shirika la GCI, Victoria Emmanuel akitoa elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wanaume wanaokunywa Kahawa katika Kijiwe cha Athumani Ibrahimu kilichopo mkabala na Zanahati ya Miti Mirefu Nguzo Nane Mjini Shinyanga
Mfanyakazi wa Shirika la GCI, Elizabeth Samsonakitoa elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wanaume wanaokunywa Kahawa katika Kijiwe cha Athumani Ibrahimu kilichopo mkabala na Zanahati ya Miti Mirefu Nguzo Nane Mjini Shinyanga
Mwakilishi wa Dawati la Jinsia na Watoto wilaya ya Shinyanga, Bryson John akitoa elimu kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wanaume wanaokunywa Kahawa katika Kijiwe cha Athumani Ibrahimu Nguzo Nane Mjini Shinyanga
Mwakilishi wa Dawati la Jinsia na Watoto wilaya ya Shinyanga, Bryson John akitoa elimu kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wanaume wanaokunywa Kahawa katika Kijiwe cha Athumani Ibrahimu Nguzo Nane Mjini Shinyanga
Deogratius Moya akichangia hoja kuhusu vyanzo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na nini kifanyike kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii wakati Shirika la GCI lilikitoa elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wanaume katika Kijiwe cha Kahawa Nguzo Nane Mjini Shinyanga
Alex Elias akichangia hoja kuhusu vyanzo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na nini kifanyike kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii wakati Shirika la GCI lilikitoa elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wanaume katika Kijiwe cha Kahawa Nguzo Nane Mjini Shinyanga
Wadau wakiendelea kupata huduma ya kahawa na kusikiliza maoni kuhusu masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Stephen Wilson akichangia hoja kuhusu vyanzo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na nini kifanyike kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii wakati Shirika la GCI lilikitoa elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wanaume katika Kijiwe cha Kahawa Nguzo Nane Mjini Shinyanga
Shaban Martin akichangia hoja kuhusu vyanzo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na nini kifanyike kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii wakati Shirika la GCI lilikitoa elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wanaume katika Kijiwe cha Kahawa Nguzo Nane Mjini Shinyanga
Elisha Philipo akichangia hoja kuhusu vyanzo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na nini kifanyike kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii wakati Shirika la GCI lilikitoa elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wanaume katika Kijiwe cha Kahawa Nguzo Nane Mjini Shinyanga
John George akichangia hoja kuhusu vyanzo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na nini kifanyike kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii wakati Shirika la GCI lilikitoa elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wanaume katika Kijiwe cha Kahawa Nguzo Nane Mjini Shinyanga
Wadau wakiwa katika kijiwe cha Kahawa
Adam Hussein akichangia hoja kuhusu vyanzo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na nini kifanyike kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii wakati Shirika la GCI lilikitoa elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wanaume katika Kijiwe cha Kahawa Nguzo Nane Mjini Shinyanga
Wadau wa kahawa wakifuatilia majadiliano yaliyokuwa yanaendelea kuhusu masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Wafanyakazi wa Shirika la GCI wakifuatilia mjadala kuhusu masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Huduma ya kahawa ikiendelea
Wadau wakiwa katika kijiwe cha Kahawa Nguzo nane Mjini Shinyanga
Mwakilishi wa Dawati la Jinsia na Watoto wilaya ya Shinyanga, Bryson John na wafanyakazi wa Shirika la GCI katika Kijiwe cha Kahawa cha Athumani Ibrahimu kilichopo Nguzo Nane Mjini Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger