Monday, 22 February 2021

WANNE WAKAMATWA KUZUSHA VIFO VYA CORONA TANZANIA

...


Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watu wanne kwa tuhuma ya kutumia mitandao ya kijamii kueneza uvumi wa vifo vya watu wakidai wamekufa kwa Corona na kutia hofu wananchi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amewataja watuhumiwa hao kuwa  ni Frank  Almatia Nyange (47), Moses Goodluck Mgao (34) Mohamedi Lutambi (47) na Bumija Moses Senkondo (55) ambao walikamatwa Februari 18,2021 na Februari 19,2021.

“Watuhumiwa hawa wanne tuliowakamata na wengine ambao tunaendelea kuwatafuta wanasambaza taarifa za uvumi za vifo vya Watu wakidai wamekufa kwa Corona na pia wanapendekeza majina ya Viongozi wa Serikali ambao walitamani wafe haraka kwa Corona”,amesema Kamanda Nyigesa

Amesema watuhumiwa hawa wanne Frank Nyange na wenzake pamoja na wengine ambao wanatafutwa licha ya kueneza uvumi wa vifo vya watu wakidai wamekufa kwa Corona  pia wanatia hofu Mitandaoni kwa kudai Watanzania walio wengi watakufa kwa sababu serikali haichukui tahadhari dhidi ya wananchi wake.

“Polisi Mkoani Pwani tunatoa rai kwa Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona kwa kufuata maelekezo ya Wataalamu wa Afya na kujiepusha na matumizi mabaya ya Mitandao ikiwemo kutoa taarifa za uvumi kuhusu vifo vya Watu ambazo zinatia hofu Wananchi wengi, hatua za Kisheria zitachukuliwa kwa watakaofanya hivyo”,ameongeza
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger