Monday, 22 February 2021

HALMASHAURI ZATAKIWA KUWA NA MASHAMBA DARASA YA MALISHO YA MIFUGO

...

Baadhi ya mifugo wanaopatikana katika kituo cha utafiti wa Mifugo cha TALIRI Mpwawa mkoani Dodoma.

Na Faustine Gimu Galafoni, Dodoma.

Halmashauri zote nchini zimetakiwa ziwe na shamba darasa ya malisho ya mifugo ili kupunguza migogoro ya ardhi kutokana na wafugaji kuvamia maeneo ya wakulima kwa lengo la kutafuta malisho.

 Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Idara ya Utafiti Wizara ya Mifugo Dk. Anjelo Mwilawa wakati akizungumza na waandishi wa  habari  katika kituo cha  utafiti wa mifugo [TALIRI] Mpwapwa  ambapo alibainisha kuwa  licha ya  nchi ya Tanzania kuwa na wingi wa mifugo lakini maeneo ya malisho ni ya tangu   miaka ya nyuma .

“Malisho haya ya nyasi yanatuletea virutubisho vya wanga kwenye vyakula vya wanyama ,katika maeneo haya ya nyanda kame tuhimize wafugaji wetu wastawishe malisho ambayo yatakuwa chanzo cha chakula bora kwa mifugo yao ,wizara yetu imehimiza halmashauri kuwa na mashamba darasa ya malisho ili wafugaji waweze kupata mbegu bora na kuepika migogoro ya ardhi”,alisema.

Msimamizi wa shamba Darasa la malisho ya mifugo Mpwapwa Erick Kimaro amesema shamba hilo limekuwa na tija kubwa kwa malisho ya mifugo.

“Tumepanda nyasi hizi ambazo ni muhimu sana kwa malisho ya mifugo na eneo lina ukubwa wa hekta 120 sawa na wastani wa ekari 240 na tumekuwa tukipokea wafugaji kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo ya Kiteto”,amesema.

 Kaimu Mkurugenzi Taasisi ya utafiti mifugo nchini [TALIRI]  DK. Jonas Kizima amezungumzia majukumu ya taasisi hiyo kuwa ni pamoja na kutatua changamoto za wafugaji na kufanya tafiti mbalimbali.

“Taasisi ya utafiti wa mifugo Tanzania [TALIRI]ipo chini ya wizara ya mifugo na Uvuvi na imeundwa kwa sheria Na.4  2012 ,na inayo majukumu ambayo ni kufanya tafiti na kutatua changamoto za wafugaji na inaundwa na kanda saba kote nchini ”,amesema.

 

Kaimu Meneja wa  Idara ya Utafiti  wa Mifugo  TALIRI  kituo cha Mpwapwa Deogratius Massawe ameelezea  historia ya josho la Nunge  Mpwapwa ni tangu mwaka 1905  ambapo wakoloni waliona eneo hilo ni muhimu kwa sababu ya ufugaji.

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania [TALIRI ]tayari imefanya utafiti wa malisho ya mifugo katika kituo chake cha Mpwapwa na wizara ya mifugo na uvuvi imeshauri ni vyema utafiti ufanyike kwa kutumia halmashauri ili ku punguza migogoro ya ardhi ambapo  Kituo cha Utafiti wa Mifugo Mpwapwa ni kituo cha kwanza kuanzishwa nchini chini ya utawala wa wakoloni wa Kijerumani 1905 na hadi kufikia sasa ni zaidi ya miaka 115.

 Baadhi ya mifugo wanaopatikana katika kituo cha utafiti wa Mifugo cha TALIRI Mpwawa mkoani Dodoma.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger