MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi wa Kata ya Majengo kwenye uwanja wa Lamore Jijini Tanga
Msanii wa Mziki wa Bongofleva Kassim Mganga akitumbuiza wakati mkutano huo wa kampeni WANANCHI wa Kata ya Majengo wakiwa kwenye mkutano wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
WANANCHI wa Kata ya Majengo wakiwa kwenye mkutano wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu WANANCHI wa Kata ya Majengo wakiwa kwenye mkutano wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema atahimiza uwekezaji ili kuwezesha ujenzi wa viwanda vipya kwenye Jiji la Tanga ikiwemo vile kuvifufua vya zamani ili kuongeza fursa za ajira na vipato kwa wananchi.
Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto aliyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi wa Kata ya Majengo Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika uwanja wa Lamore.
Alisema endapo wananchi watamchague hawataweza kujutia kutokana na mipango mizuri aliyonayo kuhakikisha wanawake, vijana na wanaume wanaweza kuinuka kiuchumi na hivyo kuweza kuongeza vipato vyao.
“Binafsi ninaamini endapo tutakuwa na viwanda Tanga itachangamka vijana, wakina mama na wanaume watapata ajira na hivyo kuchochea kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi kwenye Jiji la Tanga “Alisema
Aidha alisema mkakati wa pili ambao utawezesha kuwajaza manoti wakazi wa Tanga ni kupigania maboresho ya awamu ya pili ya bandari ya Tanga ili kufungua furza za kiuchumi na kipato kwa wana Tanga.
“Mkakati wangu wa tatu ni kuhakikisha ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga unakamilika na katika hili namshukuru Rais Dkt John Magufuli ambaye amewezesha bomba hilo kujengwa kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga”Alisema
“Hivyo ninawaomba mnipe kura zenu zote za ndio, wanawake wenzengu naombeni mninyanye mwanamke mwezengu kwa kunipa kura za ndio ili tukaweke historia jimbo la Tanga kuongoizwa na mwanamke pia niwaomba mpe kura za ndio Rais Dkt Magufuli
Aliwaomba wananchi hao wamchague Rais Dkt John Magufuli ili aweze kuendelea kuwa Rais kazi yake kwenye Jiji la tanga katika kata ya Majengo inaonekana amewezesha utolewaji elimu bure kwa watoto kwenye kata za Majengo tumpe kura zetu zote za ndio”Alisema
Ummy aliwaomba wamchague ili aweze kusimamia suala hilo kwani anauhakika wataweza kupata ajira nyingi kwa wakazi wa Jiji la Tanga na Kata ya Majengo ikiwemo kuwawezesha kiuchumi vijana kwa kuwapigania mikopo vijana.
“Katika kata ya Majengo vijana wengi wanajishuhughulisha na dawa ya kulevya lakini kwa sababu hawana shughuli za kufanya ninawaomba mnichague ili niweze kuanzisha program mbalimbali za kuwawezesha vijana kuweza kujiajiri na kufanya shughuli nyengine za kujiongea vipato”Alisema
Hata hivyo alisema pia endapo akichaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo ataanzisha ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kata ya Majengo ili kuwasaidia watoto wasiende kwenye shule za mbali.
0 comments:
Post a Comment