Monday, 5 October 2020

Taifa Stars Kuivaa Burundi....Samatta kuwasili nchini kesho

...

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta anatarajiwa kuwasili nchini kesho kujiunga na kambi ya timu hiyo inayojiandaa na mechi ya kifariki ya kalenda ya FIFA dhidi ya Burundi itakayochewa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Samatta ndiye aliyefunga mabao yote mawili ya ushindi ya Fernebahce dhidi ya Fatih Karagumluk katika mechi ya ligi kuu nchini Uturuki iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ikumbukwe timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars inaingia kambini leo Oktoba 5 huku baadhi ya wachezaji walioitwa na kocha Etienne Ndayiragije wamewasili kambini kujiwinda na mchezo huo.

Wachezaji wengine wa kimataifa ni pamoja na Thomas Ulimwengu anayetarajiwa kuwasili leo akitokea Congo DR, Himid Mao, Simon Msuva na Nickson Kibabage kutokea Misri na Morocco watawasili Jumatano naye Ally Msengi tayari amewasili akitokea Afrika Kusini.

Etienne Ndayiragije, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania amesema kuwa wana imani ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo huo  wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya FIFA unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 11 Uwanja wa Mkapa.

Ndayiragije amesema kuwa:"Tupo vizuri na imani ni kwamba tutafanya vizuri kwa kuwa wachezaji ambao wapo kwenye kikosi wana uzoefu mkubwa na wanajua kutimiza majukumu yao.

"Kabla ya kuwaita kwenye kikosi huwa ninakuwa na tabia ya kuwafuatilia kwa ukaribu hivyo tunaamini kwamba licha ya ushindani ambao tutakutana nao tutapata matokeo."


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger