Wednesday, 7 October 2020

RC Kigoma awajulia hali Zitto Kabwe na wenzake Waliopata Ajali

...

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amemtembelea na kutoa pole kwa Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma baada ya kupata ajali ya gari hapo jana wakati akiwa katika shughuli zake za kampeni.


Zitto Kabwe amepata ajali katika kata ya Kalya baada ya gari alilokuwa amepanda kugongwa na gari lingine kwa nyuma na kusababisha majeruhi kwa Watu waliokuwa katika gari hilo ambapo huduma ya kwanza walipatiwa katika Kituo cha Afya Kalya.

Zitto amesema gari lililowagonga na kusababisha ajali yao ni la Mgombea Ubunge Jimbo la Kigoma Kusini kwa Ticket ya ACT, chanzo kikiwa ni vumbi lililokuwa limetanda Barabarani, ambapo amesema hali yake inaendelea kuimarika.

“Kwa mujibu wa taarifa za wataalamu wa afya nimeambiwa kuwa bega langu la mkono wa kushoto lina tatizo ambapo kuna mfupa ambao umevunjika, lakini naendelea vizuri kwa sasa,” amesema Zitto

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dkt. Saimon Chacha ameeleza kuwa huduma zinaendelea kutolewa kwa majeruhi wote na kuwa Zitto anatarijiwa kusafirishwa kwenda Dar es salaam kwa ajili ya matibabu pamoja na vipimo zaidi




Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger