Saturday, 17 October 2020

Mwanafunzi Ajinyonga Kisa Kugombezwa kwa Kuchelewa Kurudi Nyumbani

...

 

Mwanafunzi aliyemaliza darasa la 7 wiki iliyopita katika shule ya msingi Njungwa, Kijiji cha  Ngayaki wilayani Gairo, amekutwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kanga huku chanzo kikitajwa ni ugomvi kati yake na mama yake mzazi aliyekuwa akimkataza kurudi nyumbani usiku.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, amesema tukio hilo limetokea Oktoba 15 mwaka huu, na akatoa wito kwa wale watu wanaoona njia ya bora ya kutatua changamoto wanazokutana nazo kwenye maisha ni kukatisha uhai wao, kuwa siyo sahihi na badala yake watafute ufumbuzi wa changamoto zao kwa wataalam.

"Aligombezwa na mama yake kwa kosa la kurudi nyumbani mara kwa mara usiku na alitoweka nyumbani na ndipo alipokutwa amejinyoga vichakani, nitoe wito kwa watu ambao wanafikiri 'shortcuts' ya changamoto wanazokutana nazo kwenye maisha ni kuamua kujinyonga, hiyo si sahihi ni bora ukutane na wataalam wa kisaikolojia ili wakusaidie", amesema Kamanda Mutafungwa.

Mwili wa mtoto huyo mara baada ya kufanyiwa uchunguzi ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.




Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger