Wednesday, 21 October 2020

Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Dk Salim Ahmed Salim Kuzikwa Kesho

...


 Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim, Amne Salim anatarajiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya Kisutu ,jijini Dar es Salaam.

Amne alifariki dunia usiku wa kuamkia jana baada ya kulazwa katika hospitali ya Aga Khan kwa muda.

Amne alijaliwa kupata watoto watatu na Dk Salim aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Jumuiya ya Umoja wa Afrika (OAU). Watoto hao ni Maryam, Ali na Ahmed.

Mbali na kuwa kiongozi wa OAU, Dk Salim aliyekuwa mwanasiasa tangu miaka ya 1960 pia amewahi kuwa Waziri Mkuu, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Balozi katika nchi mbalimbali.





Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger