Saturday, 3 October 2020

Kamati ya Maadili - NEC Yasisitiza Adhabu Aliyopewa Tundu Lissu ni SAHIHI na ni Lazima Aitekeleze

...


Kamati ya maadili ya taifa imesisitiza kuwa adhabu iliyotolewa na kamati hiyo kwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Mhe.Tundu Lissu ni sahihi na haruhusiwi kupanda kwenye jukwaa lolote la siasa hadi adhabu hiyo iishe.

Hayo yamesemwa leo Jumamosi, Oktoba 3, 2020 na Katibu Kamati ya Maadili ya Kitaifa, Emmanuel Kawishe wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelezea sakata hilo ikiwa ni siku moja tangu Lissu asimamishwe kufanya kampeni zake kwa siku saba kwa madai ya kukiuka taratibu na kanuni za uchaguzi.

“Kwa kuzingatia taratibu, Tume hupeleka taarifa kwa Katibu wa chama husika, Tume haimpelekei taarifa mgombea mmoja mmoja, Tume inawasiliana na Katibu Mkuu na si vinginevyo. 

"Katibu Mkuu CHADEMA ndiye aliyemdhamini Tundu Lissu kuwa mwanachama na mgombea wa kiti cha rais kupitia chadema kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977.

Hivyo, Adhabu hiyo inatakiwa kutekelezwa kwa kuwa imetolewa na chombo chenye mamlaka ya kisheria na kwa kuzingatia utaratibu, mgombea urais wa CHADEMA  anatakiwa kuheshimu na kutekeleza adhabu hiyo kama ilivyotolewa

"Endapo mgombea huyo atadharau uamuzi wa kamati na kufanya kampeni, atambue kuwa kamati imepewa mamlaka ya kuelekeza makosa mengine kwenye vyombo vingine kadri itakavyoona inafaa"- Emmanuel Kawishe, Katibu wa Kamati ya Maadili ya Kitaifa.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger