Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha uuzaji wa madini Kalalani wilayani Korogwe kulia ni Mwenyekiti wa Tawoma Eunice Negelo |
Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo akisisistiza jambo wakati wa uzinduzi wa kituo cha ununuzi wa madini Kalalani wilayani Korogwe
|
Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Rahel Mhando akieleza jambo wakati wa uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa na kulia ni Katibu wa Tawoma Salma Kundi
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo wa kituo cha Ununuzi wa Madini Kalalani Korogwe |
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo wa kituo cha Ununuzi wa Madini Kalalani Korogwe katikati ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa na kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Rahel Mhando na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo na wa kwanza kulia ni Katibu wa Chama hicho Salma Kundi |
Shughuli za utambuzi wa madini zikiendelea wakati wa uzinduzi wa kituo cha kuuzia madini Kalalani wilayani Korogwe kama inavyoonekana |
Shughuli za utambuzi wa madini zikiendelea wakati wa uzinduzi wa kituo cha kuuzia madini Kalalani wilayani Korogwe kama inavyoonekana |
MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Kissa Gwakisa amewaonya wachimbaji wa madini wenye tabia ya kutorosha madini waache mara moja badala yake wafuateni taratibu zilizowekwa na Serikali.
Kissa aliyasema hayo wakati akifungua kituo cha uuzaji Madini eneo la Kalalani wilayani Korogwe ambapo alisema serikali inaruhusu mtu kuuza madini sehemu yoyote anapotaka lakini tabia ya utoroshaji haitakiwa na wasijaribu kufanya hivyo.
Katika ufunguzi wa kituo hicho kilihudhuria na Afisa Madini mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho na maafisa wengine wa ofisi na Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo wakiwemo wauzaji na wanunuzi.
Alisema lazima wachimbaji kubadilika na kuacha na tabia za namna hiyo kwa kuhakikisha wanafuata taratibu zilizokwekwa kwa mujibu wa sheria kuweze kuwa na manufaa kati ya wachimbaji, serikali na jamii kwa ujumla.
“Labda niwaambie kwamba Mkuu wa Polisi wilaya ya Korogwe (OCD) ndio atakuwa na jukumu la kulinda kituo hiki kipya ambacho kinaanzishwa hapa cha ununuzi na uuzaji pamoja na jeshi la akiba watoe vijana kila siku ya soko ambao watakuja kuwasindikiza wanunuzi mpaka watakapotoka nje ya wilaya hiyo na ndio maana kamati ya ulinzi ipo hapa”Alisema DC Kissa
Aidha alibainisha kwamba kwenye wilaya hiyo wana jumla ya leseni za wachimbaji 153 lakini zinazooneka na zinafanya kazi ni 25 hivyo uanzishwaji wa kituo hicho utakuwa ni kuchochea cha wale wenye leseni ambazo hawafanyi kazi kufanya kazi ili leseni hizo ziweze kuleta tija kwa wananchi wa wilaya ya Korogwe na wanunuzi,.
“Lakini pia niwaambie kwamba tunafikiria kuanzisha kituo kikubwa Korogwe mjini cha Soko la Madini ni mipango wanaendelea nayo na tunaamini utakuwa na tija hivyo na kuwawezesha wachimbaji kuuza madini yao “Alisema
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba anaamini jambo linalofanyika halijakiuka sheria za nchi na limefuata miongozi hivyo ni vuzuri uendeshaji wake na jinsi soko litakavyokuwa linakwenda lifuate sheria ili serikali iweze kupata manufaa yake na wananchi mtu mmoja mmoja waweze kupata na wanunuizi wanaokwenda kununua wasijutie uanzishwaji wake.
“Tunatambua tunao brokers ambao wanakuja kununua madini kwa wachimbaji wadogo naawaomba sana wasimamizi hapo, ofisi ya madini mkoa ambayo ipo chini ya wizara ya madini watusaidie kuangalia kwamba kunakuwa na uwanja uliopo sawa kwa ajili ya watu wote kati ya muuzaji na mnunuzi ili soko hilo liweza kuwa na maisha marefu”Alisema
Alisema kwa sababu ikitokea mmoja analalamika au kuna upande unaumizwa soko litakuwa halina maisha marefu huku akieleza kituo hicho hatakuwa cha madini yanayotoka kalalani pekee bali madini yote ya vito yanayotoka wilayani humo yatauzwa hapo.
“Kama mtakumbuka Serikali chini ya Rais Dkt John Magufuli ilianzisha masoko na vituo vya uuzwaji wa madini kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini na nyie wenyewe mmeshughudia RC Martine Shigella amekwisha kuzindua masoko mawili Handeni na Mkinga leo ni muendelezo wa yake masoko na vituo vilivyoanzishwa rasmi kwa miongozo na maelekezo wa Rais “Alisema
“Tunafungua tukifuatia kifungu cha sheria namba 17 cha sheria ya madini ya mwaka 2010 ambayo imekuwa ikifanyiwa marekebisho mwaka 2017,2018 na 2019 na kanuni zake za uanzishwaji wa masoko lakini pia niwapongeze Tawoma,Tarema na wadau Moyo Gems kwa juhudi kubwa mnazozifanya”Alisema
Awali akizungumza katika ufunguzi huo Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho aliwataka wachimbaji wa madini kuhakikisha wanafuata taratibu na sheria huku akieleza wadau wa kalalani watauza madini yao hapa hapo kwenye kituo hicho.
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo alisema wana mshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa jinsi alivyowasaidia wanawake wachimbaji kwa kuweza kuwathamini,kuwaamini na kuwawezesha na wameweza kufanya miradi mbalimbali wakiwa huru na amani kwa sababu ya uongozi wake bora.
“Kwa kweli tunamshukuru Rais Dkt John Magufuli kutokana na kuwathamini na kuwaelewa wachimbaji leo hii tumeweza kuuza madini kwa uhuru na amani na lakini pia uwepo wa masoko ya madini yaliyoanzishwa na wakina mama Tawoma wakiungana na Chama cha Pact na kuzalisha kitu kinachoitwa Moyo Gems”Alisema Mwenyekiti huyo.
0 comments:
Post a Comment