Sunday, 4 October 2020

CHADEMA Wambadilishia Majukumu Tundu Lissu

...
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema, kitambadilishia majukumu Tundu Lissu, Mgombea wake wa Urais wa Tanzania wakati akiitumikia adhabu ya kutofanya kampeni kwa muda wa siku saba kuanzia jana tarehe 3 hadi 9 Oktoba 2020.

 Akizungumza na waandishi wa habari  leo jumapili tarehe 4 Oktoba 2020 jijini Dar es Salaam, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema amesema, mbadala wa Lissu kutofanya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020 katika kipindi hicho, mwanasiasa huyo atapangiwa kazi maalum kama Makamu Mwenyekiti wa Chadema

 “Tundu Lissu siyo tu ni mgombea wa Urais wa chama chetu, huyu ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hivyo hatakosa cha kufanya kwa kipindi cha siku 7.

"Chama kitampangia program mahususi kama Makamu Mwenyekiti kufanya majukumu ya kijamii na kisiasa.”-Amesema

Amesema, Watanzania hawatapata ujumbe wa mgombea wa Urais, lakini wataupata ule wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.

Aidha, Mbowe amesema, Kamati Kuu ya Chadema imeelekeza Kitengo cha Sheria cha chama hicho kuandaa hati ya dharura kwa ajili ya kufungua kesi mahakamani kuipinga adhabu hiyo.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger