Tuesday, 11 February 2020

Wakenya kunywa maziwa, soda na vitafunio mazishi ya Rais wa zamani wa Kenya Daniel arap Moi

...
Waombolezaji  katika mazishi ya Rais wa zamani wa Kenya Daniel arap Moi wamehimizwa kuwahi mapema kwenye mazishi ili wapate maziwa na viburudisho vingine.

Serikali ya Kenya imesema itatoa viburudisho kwa watu 30,000 wa kwanza kufika katika mazishi  hayo yatakayofanyika leo.

Mratibu wa jimbo la Rift Valley,  George Natembeya amesema kuwa kutakuwa na viti, soda, maziwa na mikate pamoja na maji kwa watu 30,000 wa kwanza kufika kwenye mazishi na pia watakalishwa kwenye hema.

Natembeya amesema waombolezaji waliosalia watakaribishwa tu ndani ya eneo la makazi, lakini hawatapata mahala pa kukaa.

Amesema pia kwamba vitafunio vitatolewa kwa wale wa kwanza watakaohudhuria mazishi.

“Atakayefika kwanza ndiye atakayepewa wa kwanza “, alisema Matembeya huku akiwataka waombolezaji kufika mapema.

Aidha usafiri utatolewa kuanzia mji wa Nakuru hadi katika makazi ya Moi ya Kabarak yapata kilomita 20 (sawa na maili 12.4) kutoka Nakuru mjini.

Rais mstaafu Moi aliaga dunia katika hospitali ya Nairobi Jumanne wiki iliyopita na Wakenya mbalimbali wamekua wakipata fursa ya kwenda kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa kiongozi huyo aliyeliongoza taifa lao kwa muda wa miaka 27.

Mwili wa Hayati Moi utazikwa katika makazi yake ya Kabarak eneo la Nakuru siku ya Jumanne.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger