Leo Februari 11, 2020, Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera, itatajwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam
Kesi hiyo ilikuwa inatajwa jana katika Mahakama ya Hàkimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Janeth Mtega na kuahirishwa hadi leo.
Wakili wa Serikali, Faraji Nguka akiiwakilisha Jamhuri, alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, akaomba iahirishwe hadi leo.
Januari 27, mwaka huu wakati kesi hiyo inatajwa, upande wa Jamhuri ulidai majadiliano na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ya jinsi ya kumaliza kesi hiyo yanaendelea.
Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwamo la utakatishaji wa zaidi ya Sh milioni 173.
0 comments:
Post a Comment