Serikali imesema haiwezi kuongeza adhabu kali kwa wabakaji zikiwemo adhabu za kuhasiwa kwani zilizopo ni kali na zinatosha.
Hayo yamesemwa leo Feb.4.2020 jijini Dodoma na Waziri wa katiba na sheria Balozi.Dkt.Augustne Mahiga wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti Maalum [CCM]Mhe.Zainab Katimba aliyehoji kutokana na vitendo vya ukatili dhidi ya mtoto wa kike hususan ubakaji kuendelea kuripotiwa mara kwa mara ,je,serikali haioni namna ya kuongeza adhabu kali dhidi ya watu wanaofanya vitendo hivyo.
Akijibu swali hilo,Waziri wa Katiba na Sheria ,Balozi.Dkt.Augustine Mahiga amesema adhabu zilizopo kwa sasa ni kali kwani mtu aliyefanya kosa la ubakaji ni miaka 30 mpaka wengine wanafia magerezani.
Akilitolea ufafanuzi zaidi juu ya suala hilo,Mwanasheria mkuu wa Serikali Dkt.Adelardus Kilangi amesema pendekezo la kuhasiwa litapekekea kuvunja katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ibara ya 13,ibara ndogo ya 6 ambapo inaeleza ni marufuku kwa mtu kuteswa,kuadhibiwa kwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtesa au kumdhalilisha .
Naye Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto ,Mhe.Ummy Mwalimu amesema sheria peke yake hazitoshi na kinachotakiwa ni wazazi na walezi kutimiza wajibu katika ulinzi na malezi kwa watoto.
0 comments:
Post a Comment