Wednesday, 22 February 2017

WANAWAKE 13 WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 2 KWA KOSA LA KUJIUZA HUKO MOROGORO

...

 Dada poa hao wakitoka  ser
o ya Mahakama ya Nunge wakipanda Difenda  kuelekea Magereza.


 Dada poa huyu baada ya kutoanm kwenye sero na kumshuhudia Mwandishi wa habari hizi akiwapiga picha mahakani hapo alificha sura yake.
 

 Warembo hao baada ya kukamtwa jumatano iliyopita usiku mnene wakiwa wamevaa vinguo vya vya mitege'Vimini' siku iliyofuta ndugu zao waliwaletea nguo za heshima na kutinga nazo mahakamani kama wanavyooneka pichani.
Ukiwa kwenye windo ukivaa mavazi haya utampata nani? 
 








Difenda hilo likiwapeleka Magereza wakaanze maisha Mapya huku baadhi ya ndugu zao wakiwashuhudia 
 
       Na Dustan Shekidele,Morogoro.
ILI Kuonyesha serikali ya sasa hailazi damu na kwamba moto unawaka kila kona ili Mambo yaende sawa na kwa spidi kubwa warembo wapatao 13  wamejikuta wakihukumiwa kwenda jela miaka miwili[2] kila mmoja baada ya kukiri kosa lao mbele ya Mahakama.

Katika sakata hilo lililoshuhudia na Mwandishi wa habari hizi  mwiashoni mwa wiki iliyopita  warembo hao walipigwa mvua hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha na biashara haramu ya kuuza mwili na kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzi ya Nunge Mkoani hapa.

Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo  wanawake hao walikamatwa na Polisi usiku mnene wakiuza Miili yao kwenye kambi korofi ya Ufuska ya ltigi iliyopo Msamvu Kata ya Mwembesongo  Mjini hapa ambapo walifunguliwa kesi namba 155 ya mwaka 2017.

Hukumu hiyo ilitolewa na hakimu ya Mahakama hiyo  Emelia Halosi Mwambagi baada ya watuhumiwa hao kukiri kosa mbele ya Mahakama hiyo wakidai walifanya hivyo kutokana na ugumu wa Maisha.

Hata hivyo hakimu huyo  alisema aliwahukumu warembo hao kwenda jela miaka 2 kila mmoja  kwa kosa la uzururaji na kujiuza na kujipatia kipata  kwa kuuza mwili ili iwe fundisho kwa wanawake wengine wanaofanya biashara hiyo haramu.

Akizungumza na Mtandao huu katika Mahojiano Maalumu baada ya hukumu hiyo,hakimu huyo alikuwa na haya ya kusema.

"Kuna biashara nyingi za kufanya kama vile Mama Ntilie na Vibarua vya kulima. kuuza mwili  ni kujidharirisha na kudharirisha wanawake wengine nimetoa hukumu hii ili tahadhari kwa wengine wanaofanya hivyo"alisema 

Baada ya kusomewa hukumu hiyo warembo hao walijikuta wakipigwa na butwaa  huku wakishidndwa kuamini kilichotokea kwani walidhani wangepigwa faini ya kiasi kidogo  cha fedha kisha kurejea uraiani lakini ndio kwanza maafande kupanda Difenda kuelekea Gerezani  kuanza kutumikia adhabu hiyo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger