Maelfu
ya wakazi wa mkoa wa Mbeya wamejitokeza katika mazishi ya mchezaji wa
zamani Geoffrey Bonny Mwandanji aliyefariki dunia juzi na kuzikwa katika
makaburi ya kanisa Katoliki Makandana wilayani Rungwe.
Akizungumza wakati wa mazishi baba mzazi wa marehemu,Bonifasi Mashamba
alisema amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mwanae na kuongeza kuwa
aliishi na watu vizuri jambo lililochangia watu wengi kujitokeza
kumuuguza ikiwa ni pamoja na misaada mbali mbali.
Naye Mjomba wa marehemu, Innocent
Sigonda alisema marehemu alikuwa akisumbuliwa na kansa ya mapafu pamoja
sukari ilikuwa ikishuka mara kwa mara.
Mwenyekiti wa tawi la Yanga mkoa wa Mbeya Lusajo Kifamba alisema
marehemu alikuwa mwanachama wao hivyo uongozi unasikitika kumpoteza
mwanachama wake ambaye alikuwa akitoa msaada wa kiufundi kila
alipotakiwa.
Naye mwakilishi wa uongozi wa yanga makao makuu Shadrack Nsajigwa
alisema marehemu aliishi naye kama ndugu kwani walisaidiana na kupeana
ushauri.
Alisema marehemu alikuwa na kipaji cha mpira pia alikuwa anajituma hivyo alikuwa mfano wa kuigwa kwa vijana waliopo.
Aliongeza kuwa wachezaji wa zamani ni hazina kwa taifa hivyo ni vyema wakatunzwa na kuthaminiwa.
Aidha alitoa wito kwa wachezaji wengine kujipanga kimaisha ili baada ya
kustafu wasisubiri kuomba misaada pindi wapatapo matatizo.
Alisema in vyema pia kuanzisha vyama vya kuwasaidia kama wachezaji wastaafu.
0 comments:
Post a Comment